Kiongozi wa Ujumbe wa Chama cha Ukombozi Cha Kipalestina Taysear Ishled akiagana na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif baadayakumaliza mazungumzo yao.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiwa katika picha ya pamoja na Ujumbe wa Chama cha Ukombozi wa Palestina { PLO } pamoja nawenyeji wao wa Chama cha Mapinduzi.
Katibu wa Sekriterieti ya CCM Uhusiano wa Kimataifa Balozi Asha-Rose Migiro akiteta jambo na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi, alipomtembelea Ofisini kwake akiongozani na ugeni kutoka Chama cha Palestina, waliofika Ofisini kwake Vuga Zanzibar.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi, akizungumza nma Balozi wa Uholanzi Nchini Tanzania Dr. Ad Koekkoek, alipofika Ofisini kwake Vuga kwa ajili ya kuja kumuaga baada ya kumaliza muda wake wa Utumishi Nchini Tanzania.
Makamu wa Pil iwa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akimkabidhi zawadi ya Kasha Balozi wa Uholanzi Nchini Tanzania Dr. Ad Koekkoek kamaishara ya ukumbusho kutokana na utumishi wake mzuri hapa Tanzania. Pichana Hassan Issawa – OMPR – ZNZ.
Na.Othman Khamis Ame
Serikali ya Uholanzi imeipongezaJamuhuri ya Muungano wa Tanzania kwa uamuzi wake wa kuifungua tena Ofisi yake ya Ubalozi iliyopo Nchini Uholanzi kitendo ambacho kitazidisha uhusiano wa karibu kati ya Mataifa hayo mawili.
Pongezi hizo zimetolewa na Balozi wa Uholanzi Nchini Tanzania Dr. Ad Koekkoek wakati akizungumza na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar BaloziSeif Ali Iddi hapo Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar.
Dr. Koekkoek ambae amekuja kuaga akikaribia kumaliza muda wake wa utumishi wa Kidiplomasia akiiwakilisha Nchi yake ya Uholanzi katika Ardhi ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania alisema uamuzi wa Tanzania wa kufungua Ofisi hiyo umekuja wakati muwafaka kutokana na muingiliano wa Kiuchumi wa pande hizo mbili.
Alitolea mfano wa muingiliano huo kuwa ni ile ziara ya Ujumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar uliyoifanya hivi karibuni kutembelea Nchi hiyo na hatimai kuzaliwa wazo la Wataalamu wa Kampuni ya Mafuta ya Shell kushawishika kuja Visiwani kutoaTaaluma katika masuala ya Mafuta na Gesi.
Alisema kwa vile Uholanzi ni moja ya Kituo kikubwa cha mawasiliano ya usafiri wa Anga katika Ukanda wa Bara la Ulaya Tanzania inaweza kuitumia Ofisi ya Ubalozi wake katika harakati za kuimarisha Uchumi wake kupitia Sekta ya Biashara kwa kuwaunganisha wafanyabiashara wa pande hizo mbili.
Balozi Koekkoek alisisitiza kwamba atatumia Taaluma yake ya Kidoplomasia katika kuona anashawishi Makampuni na Wawekezaji wa Uholanzi kutumia fursa zilizotolewa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwenye sekta ya uwekezaji hasa katika eneo la Utalii.
Naye Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alimpongeza Balozi huyo wa Uholanzi Nchini Tanzania Dr. Ad Koekkoek kwa utumishi wake makini uliopelekea kuimarika zaidi kwa uhusiano kati ya Mataifa hayo mawili rafiki.
Balozi Seif alisema fursa kadhaa za masomo wanazoendelea kupatiwaWanafunzi wa Kitanzania Nchini Uholanzi katika Fani tofauti ni ishara ya juhudi za Balozi huyo anayetarajiwa kumaliza muda wake mwezi ujao wa Julai Mwaka huu wa 2013.
Wakati huo huo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alikutana kwa mazungumzo na Ujumbe wa Viongozi Watu watatu wa Chama cha Ukombozi wa Kipalestina { PLO } ukiongozwa na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama hicho Taysear Ishalied.
Katika mazungumzo hayo Balozi Seif aliueleza Ujumbe huo kwamba Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania itaendelea kuunga mkono hatua za Kimataifa za kutafuta amani kati ya Palestina na Israel pamoja na Mashariki ya kat ikwa ujumla.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alifahamisha kuwa mtutu wa bunduki daima utabaki kujenga chuki, uhasama na vita visivyo kwisha huku vikiacha athari kubwa ndani ya mioyo ya wanaadamu.
“ Tanzania kamwe haitopendelea kuona watoto na wanawake wanateseka katika ardhi ya dunia hii kwa sababu ya vita vya kuwania cheo au ukabila ambavyo huondoa imani kwa wanaadamu “. Alisisitiza Balozi Seif.
Akitoa shukrani zake Mjumbe wa Kamati Kuu ya PLO Taysear Ishalied alieleza kwamba Wananchi wa Palestina wana hitaji utulivu na amani suala ambalo wataendelea kulipigania njia zote ikiwemo ile ya Kidiplomasia chini ya usimamizi wa Umoja wa Mataifa.
Alipongeza uhusiano uliopo kati ya Palestina na Tanzania ambao umejengwa na waasisi wa pande hizo mbili Marehemu Mwalimu Julius K. Nyerere na Muanzilishi wa PLO Marehemu Yasser Arafat.
Baadaye Ujumbe huo wa Viongozi watatu wa Chama cha Ukombozi wa Palestina { PLO } ulikutana na Spika wa Baraza la Wawakilishi Mh. Pandu Ameir Kificho na kubadilishana mawazo juu ya uhusiano wa karibu wa pande hizo mbili.
No comments:
Post a Comment