HOTUBA YA BAJETI YA OFISI YA MAKAMU WA KWANZA WA RAIS
MWAKA WA FEDHA 2013/2014
HOTUBA YA WAZIRI WA NCHI
OFISI YA MAKAMU WA KWANZA WA RAIS
MHESHIMIWA FATMA ABDULHABIB FEREJ
KUHUSU MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA OFISI YA MAKAMU WA KWANZA WA RAIS KWA MWAKA WA FEDHA 2013/2014 Hotuba ya bajeti ya Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais 2013/14
UTANGULIZI
1. Mheshimiwa Spika, kwa ruhusa yako naomba kutoa hoja kwamba Baraza lako tukufu sasa likae kama Kamati ya matumizi ili liweze kupokea, kuzingatia, kujadili, kuchangia na hatimae liweze kuidhinisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais kwa mwaka wa Fedha 2013/2014.
2. Mheshimiwa Spika, kwanza kabisa napenda kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutuwezesha kukutana tena katika Baraza hili tukufu, kwa ajili ya kujadili mambo muhimu kwa maendeleo ya nchi yetu.
3. Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya viongozi na watendaji wote wa Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais, napenda kumpongeza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dk. Ali Mohammed Shein kwa kuendeleza utaratibu wa kutenga sehemu ya muda wake kupokea taarifa za utekelezaji wa shughuli mbali mbali zinazotekelezwa kupitia taasisi zetu. Kwa hakika hatua hii imezidisha uwezo wa taasisi wa kutayarisha mipango mizuri pamoja na kuweka kumbukumbu za utekelezaji wa kila siku. Utaratibu huu unachangia juhudi za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika kuhakikisha maendeleo na huduma bora kwa wananchi zinapatikana.
4. Mheshimiwa Spika, napenda kutoa shukurani za dhati kwa Makamu wa Kwanza wa Rais, Mheshimiwa Maalim Seif Sharif Hamad kwa kuweza kusimamia vyema majukumu yake jambo linalotupelekea kuwa
Hotuba ya bajeti ya Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais 2013/14
3
makini katika utendaji wetu, pia napenda kumshukuru Makamu wa Pili wa Rais, Mheshimiwa Balozi Seif Ali Iddi kwa msukumo wa kiutendaji tunaoupata kutokana na usimamizi wake mzuri wa shughuli za Serikali.
5. Mheshimiwa Spika, napenda pia uniruhusu kukushukuru wewe binafsi na wasaidizi wako kwa kazi ngumu ya kuliongoza Baraza hili tukufu, kwa hakika kazi yako unaimudu ipasavyo. Uzoefu ulionao wa kiutendaji unachangia sana kuleta utulivu na ufanisi wa baraza hili tukufu na kuweza kulipatia sifa kwa utendaji wake.
6. Mheshimiwa Spika, napenda kutoa shukrani za dhati kwa Kamati za kudumu za Baraza la Wawakilishi zinazofanya kazi na ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais. Kamati ya Kusimamia Ofisi za Viongozi Wakuu wa Kitaifa inayoongozwa na Mheshimiwa Hamza Hassan Juma, mwakilishi wa wananchi wa jimbo la Kwamtipura na Kamati ya Kusimamia Hesabu za Serikali inayoongozwa na Mheshimiwa Omar Ali Shehe, mwakilishi wa wananchi wa jimbo la Chakechake.
7. Mheshimiwa Spika, nawapongeza Wenyeviti wa Kamati hizi kwa kuchaguliwa kuziongoza tena Kamati hizo, bila ya shaka hii inatokana na umahiri na utendaji bora wa majukumu yao. Pia napenda kuzihakikishia Kamati hizi, kwamba tunathamini sana ushauri na miongozo wanayotupa na hakika inatusaidia kutekeleza majukumu yetu vizuri zaidi.
Hotuba ya bajeti ya Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais 2013/14
4
8. Mheshimiwa Spika, napenda kuwashukuru Waheshimiwa Wajumbe wenzangu wa Baraza la Wawakilishi, kwa kunipa ushirikiano wa dhati tukiwa ndani na nje ya Baraza. Ni imani yangu kuwa ushirikiano wao huo umechangia kwa kiasi kikubwa kuniwezesha kupata heshima ya kutambuliwa na Ubalozi wa Marekani uliopo nchini Tanzania kuwa mmoja kati ya Wanawake wawili Majasiri hapa Tanzania kwa mwaka 2013.
9. Mheshimiwa Spika, napenda kuwapongeza Katibu Mkuu, Naibu Katibu Mkuu na Afisa Mdhamini wa Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais kwa mashirikiano makubwa wanayonipa katika utekelezaji wa majukumu ya Ofisi yetu. Vilevile, napenda kutoa shukrani zangu za dhati kwa Wakurugenzi Watendaji, Wakurugenzi, pamoja na Wafanyakazi wote wa Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais kwa juhudi, bidii na ustahamilivu katika kutekeleza majukumu yao ya kazi na kuleta ufanisi na tija kwa Taifa.
MALENGO MAKUU YA OFISI YA MAKAMU WA KWANZA WA RAIS
10. Mheshimiwa Spika, Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais ina jukumu la kusimamia na kuratibu masuala ya mazingira, watu wenye ulemavu, udhibiti wa dawa za kulevya na UKIMWI. Malengo makuu ya Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais ni :
Hotuba ya bajeti ya Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais 2013/14
5
1. Kuimarisha na kutetea uzingatiaji wa haki za binadamu na fursa sawa kwa watu wenye ulemavu ndani ya jamii.
2. Kuongoza, kuratibu, kufuatilia na kutathmini muitiko wa kitaifa wa kupambana na UKIMWI.
3. Kuimarisha usimamizi wa mazingira na matumizi endelevu ya maliasili.
4. Kuratibu na kudhibiti usafirishaji, uingizwaji, matumizi na biashara haramu ya dawa za kulevya.
11. Mheshimiwa Spika, Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais inatekeleza majukumu yake kupitia Taasisi zifuatazo:-
1. Ofisi ya Faragha
2. Idara ya Mipango, Sera na Utafiti
3. Idara ya Uendeshaji na Utumishi
4. Idara ya Mazingira
5. Idara ya Watu Wenye Ulemavu
6. Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Pemba
7. Tume ya Kuratibu na Udhibiti wa Dawa za Kulevya
8. Tume ya UKIMWI
Hotuba ya bajeti ya Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais 2013/14
6
VIPAUMBELE VYA OFISI YA MAKAMU WA KWANZA WA RAIS KWA MWAKA WA FEDHA 2013/14
12. Mheshimiwa Spika, Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais kwa mwaka wa Fedha 2013/14 imejipangia vipaumbele vifuatavyo:-
Kujenga uwezo wa watendaji katika maeneo ya utafiti
Kufanya tafiti na kukusanya taarifa juu ya shughuli zinazotekelezwa na Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais
Kukabiliana na athari za kuhimili mabadiliko ya tabianchi
Kuandaa Mkakati wa Usimamizi wa taka ambao utatoa vipaumbele vya hatua zinazofaa kuchukuliwa
Kupunguza uchukuaji usiofuata taratibu wa maliasili zisizorejesheka
Kupambana na usafirishaji na matumizi ya dawa za kulevya
Kuwa na mfumo uliokamilika wa taarifa(data base) pamoja na mahitaji kwa ajili ya Watu Wenye Ulemavu
Kutoa huduma maalum kwa Watu Wenye Ulemavu
Kuikinga jamii kwa ujumla na makundi maalum kutokana na mbukizi ya Virusi vya UKIMWI
Kutafuta rasilimali ili kutekeleza shughuli za mapambano dhidi ya UKIMWI
Hotuba ya bajeti ya Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais 2013/14
7
UTEKELEZAJI WA MALENGO YA OFISI YA MAKAMU WA KWANZA WA RAIS KWA MWAKA 2012/13 NA MALENGO 2013/14
OFISI YA FARAGHA
13. Mheshimiwa Spika, Ofisi ya Faragha ina majukumu ya kutoa huduma pamoja na kusimamia na kuratibu shughuli zote zinazofanywa na Makamu wa Kwanza wa Rais.
14. Mheshimiwa Spika, kwa mwaka wa fedha 2012/2013 Ofisi ya Faragha ilijipangia kutekeleza malengo yafuatayo:-
1. Kusimamia na kuratibu shughuli zote za Makamu wa Kwanza wa Rais.
2. Kuimarisha mazingira ya kazi katika kuleta ufanisi wa wafanyakazi.
3. Kuimarisha hudma za Makamu wa Kwanza wa Rais.
15. Mheshimiwa Spika, hadi kufikia Mei 2013 Ofisi ya Faragha imeweza kutekeleza yafuatayo katika malengo iliyojipangia:-
16. Mheshimiwa Spika, taasisi 15 zimesaidiwa katika kutimiza ahadi alizozitoa Makamu wa Kwanza wa Rais. Aidha, jumla ya wananchi 250 vikiwemo vikundi vya jamii na taasisi nyengine walifika ofisini kwa Makamu wa Kwanza wa Rais na kupatiwa huduma mbali mbali. Jumla ya ziara tano zimefanywa na Mheshimiwa
Hotuba ya bajeti ya Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais 2013/14
8
Makamu wa Kwanza wa Rais katika Mikoa ya Tanzania Bara na ziara mbali mbali za kuzitembelea Ofisi za Serikali Zanzibar. Katika ziara hizo, Mheshimiwa Makamu wa Kwanza wa Rais alipata fursa ya kushiriki katika shughuli za kijamii, kuzindua na kuweka mawe ya msingi ya miradi ya maendeleo. Vile vile, Mheshimiwa Makamu wa Kwanza wa Rais alifanya vikao tisa vilivyowashirikisha mawaziri na viongozi wakuu wa taasisi mbalimbali za Serikali kwa lengo la kupata taarifa za utekelezaji wa maagizo aliyoyatoa kuhusiana na matatizo yanayowakabili wananchi kwenye maeneo aliyoyatembelea.
17. Mheshimiwa Spika, katika kuimarisha Ofisi ya faragha vifaa mbali mbali vimenunuliwa likiwemo jenereta moja la KVA 70. Mfanyakazi mmoja amepelekwa masomoni kwa ajili ya kusoma Diploma ya ukatibu muhtasi (angalia kiambatanisho namba 1).
18. Mheshimiwa Spika, kwa mwaka wa fedha 2012/2013, Ofisi ya Faragha ilikadiriwa kutumia jumla ya TZS 511,324,000 kwa kazi za kawaida. Kati ya hizo TZS 300,000,000 kwa kuendeshea kazi na TZS 211,324,000 kwa ajili ya mishahara. Hadi kufikia Mei 2013, Ofisi hii imekwishatumia jumla ya TZS 237,900,000 sawa na asilimia 79 ya makadirio kwa kuendeshea kazi.
Hotuba ya bajeti ya Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais 2013/14
9
MALENGO KWA MWAKA WA FEDHA 2013/2014
19. Mheshimiwa Spika, Ofisi ya Faragha kwa mwaka wa fedha 2013/14 imejipangia kutekeleza malengo yafuatayo:-
1. Kusimamia na kuratibu shughuli zote za Makamu wa Kwanza wa Rais.
2. Kuimarisha utoaji wa huduma kwa Makamu wa Kwanza wa Rais.
3. Kuimarisha mazingira ya kazi katika kuleta ufanisi.
20. Mheshimiwa Spika, ili Ofisi ya Faragha iweze kutekeleza malengo yake, kwa mwaka wa fedha wa 2013/2014, naliomba Baraza lako Tukufu liidhinishe jumla ya TZS 515,150,000 kwa ajili ya kuendeshea kazi.
IDARA YA MIPANGO SERA NA UTAFITI
21. Mheshimiwa Spika, Idara hii ina majukumu ya kuandaa na kusimamia utekelezaji wa sera na mipango ya maendeleo ya Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais; kukusanya, kutunza takwimu; ufuatiliaji na tathmini pamoja na kuratibu shughuli za utafiti kwa Idara zote zilizo chini ya Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais.
22. Mheshimiwa Spika, kwa mwaka wa fedha 2012/2013 Idara ya Mipango, Sera na Utafiti ilijipangia kutekeleza malengo yafuatayo:-
1. Kuratibu utayarishaji na utekelezaji wa sera, mikakati, mipango na bajeti.
Hotuba ya bajeti ya Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais 2013/14
10
2. Kuratibu na kusimamia utekelezaji wa shughuli mtambuka, UKIMWI, dawa za kulevya, mazingira, watu wenye ulemavu, utawala bora, jinsia na idadi ya watu.
3. Kuimarisha mazingira ya kazi na kujenga uwezo kwa watendaji.
4. Kuratibu miradi ya maendeleo ya Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais na kusimamia utekelezaji wake.
23. Mheshimiwa Spika, hadi kufikia Mei 2013 Idara ya Mipango, Sera na Utafiti imeweza kutekeleza mambo yafuatayo katika malengo iliyojipangia:-
24. Mheshimiwa Spika, Idara imeendelea na utekelezaji wake wa kawaida wa kuandaa mipango ya utekelezaji, bajeti, pamoja na kuiwakilisha Ofisi katika vikao vya kitaalamu ili kuhakikisha masuala yaliyo chini ya Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais yanazingatiwa katika mipango mbali mbali ya maendeleo.
25. Mheshimiwa Spika, katika kuimarisha mazingira ya kazi na kujenga uwezo kwa watendaji, mtendaji mmoja amelipiwa sehemu ya gharama ya masomo ya ngazi ya shahada ya pili katika fani ya Uchumi, (rejea kiambatanisho namba 1). Pia, mfanyakazi mmoja amehudhuria mafunzo ya siku tano Dar-es –salaam juu ya namna ya kuingiza masuala ya mabadiliko ya tabianchi katika mipango.
26. Mheshimiwa Spika, Muongozo wa Uzingatiaji wa Mambo Mtambuka (UKIMWI, Watu Wenye Ulemavu na Dawa za Kulevya) yanayotekelezwa na Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais umeandaliwa. Muongozo huu
Hotuba ya bajeti ya Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais 2013/14
11
unatarajiwa kuzielekeza taasisi mbalimbali juu ya namna ya kuingiza mambo mtambuka katika sera na mipango yao. Kufanya kazi kwa muongozo huu kutapelekea kuwa na juhudi za pamoja za utekelezaji wa masuala ya mtambuka.
UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MAENDELEO
27. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2012/2013 Idara ya Mipango, Sera na Utafiti iliratibu utekelezaji wa miradi 5 ya maendeleo kwa fedha za Serikali na miradi 2 kwa fedha za wahisani kama ifuatayo:-
1. Mradi wa kujenga uwezo wa OMKR chini ya UNDAP (unaratibiwa na Ofisi ya Rais Fedha, Uchumi na Mipango ya Maendeleo).
2. Mradi wa kuimarisha usimamizi wa mazingira na kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi kupitia mradi wa UNDAP.
3. Mradi wa kuangamiza kunguru weusi.
4. Mradi wa elimu ya mazingira.
5. Mradi wa majaribio wa kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.
6. Mradi wa kuingiza masuala ya watu wenye ulemavu katika mipango ya maendeleo, na
7. Mradi wa Kujenga Kituo cha Tiba na Marekebisho ya Tabia kwa watumiaji wa dawa za kulevya huko Tunguu (Construction of Treatment and Rehabilitation Center).
28. Mheshimiwa Spika, utekelezaji wa miradi hiyo ni kama ifuatavyo:-
Hotuba ya bajeti ya Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais 2013/14
12
Mradi wa Kujenga Uwezo wa OMKR chini ya UNDAP
29. Mheshimiwa Spika, Kupitia Mradi huu ambao fedha zake hupitia Ofisi ya Rais Fedha Uchumi na Mipango ya Maendeleo, Idara imeandaa Mpango Mkakati wa Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa kipindi cha miaka 7 (2013 - 2020). Mpango huu utakuwa ndio dira kuu ya utekelezaji wa majukumu ya Ofisi. Idara pia imeandaa Mpango Mkuu wa Utafiti ambao umeainisha maeneo makuu yanayohitaji kufanyiwa utafiti kwa kipindi cha miaka 7 (2013-2020). Kwa mwaka wa fedha 2012/2013, OMKR ilitarajia kupata jumla ya TZS 162,973,000. Hadi mwezi wa Mei 2013 Idara ilikwisha kuingiziwa jumla ya TZS 142,000,000 sawa na asilimia 87 kwa utekelezaji wa mradi huu.
Mradi wa Kuimarisha Usimamizi wa Mazingira na Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi
30. Mheshimiwa Spika, Mradi huu unaofadhiliwa na UNDAP na kuratibiwa na OMKR, unatekelezwa na OMKR pamoja na watekelezaji wengine wakiwemo Ofisi ya Rais, Fedha Uchumi na Mipango ya Maendeleo, Wizara ya Ardhi, Makaazi, Maji na Nishati kupitia Idara ya Nishati, Wizara ya Kilimo na Maliasili kupitia Idara ya Misitu na Maliasili zisizorejesheka na Jumuiya ya Maendeleo ya Jamii na uhifadhi wa mazingira Zanzibar (Community Development and Environmental Conservation Zanzibar – CODECOZ).
31. Mheshimiwa Spika, Lengo kuu la mradi huu ni kujenga uwezo kwa taasisi mbalimbali katika kuhakikisha
Hotuba ya bajeti ya Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais 2013/14
13
masuala ya mabadiliko ya tabianchi yanaingizwa katika mipango ya sekta. Aidha mradi huu utaweka mifumo mbali mbali itakayorahisisha utekelezaji wa masuala ya kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi ikiwemo kuandaa Mpango Mkakati wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi pamoja na mpango wa utekelezaji wake.
32. Mheshimiwa Spika, Mpango Mkakati wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi umo katika matayarisho, ripoti ya utangulizi imewasilishwa na mshauri elekezi "Global Climate Adaptation Partnership" kwa kupitiwa na wadau. Rasimu ya kwanza inatarajiwa kuwasilishwa mwezi wa Julai.
33. Mheshimiwa Spika, Aidha, kampuni ya "Global Climate Adaptation Partnership" (GCAP) imepewa kazi ya kuainisha mapungufu katika MKUZA II na kuweka vipaumbele vya fursa za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi. Kampuni ya "Environmental Protection and Management Services" (EPMS) imepewa kazi ya kuandaa Muongozo wa Uzingatiaji wa Mazingira na Mabadiliko ya Tabianchi. Rasimu za awali tayari zimewasilishwa na kupitiwa na wadau, rasimu ya pili inatarajiwa kuwasilisha OMKR katika wiki ya nne ya mwezi wa Juni 2013 kwa mapitio ya mwisho.
34. Mheshimiwa Spika, vikao mbali mbali vya kamati ya wataalamu na uongozi vya mabadiliko ya tabianchi vimefanyika na kutoa ushauri juu ya namna ya kutekeleza kazi za mradi (UNDAP) pamoja na kujadili masuala yanayohusu mabadiliko ya tabianchi Zanzibar. Aidha Mkutano wa siku mbili wa kujenga uwezo wa wadau walioshiriki katika mkutano wa Umoja wa
Hotuba ya bajeti ya Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais 2013/14
14
Mataifa wa kumi na nane wa mabadiliko ya tabianchi (UNFCCC) nchini Qatar na mkutano wa siku mbili wa kutafakari utekelezaji wa mambo yaliyokubalika nchini Qatar umefanyika.
35. Mheshimiwa Spika, kwa mwaka wa fedha 2012/2013 mradi huu ulitegemea kupata fedha za wahisani jumla ya TZS 705,600,000 hadi kufikia mei 2013 jumla ya TZS 616,752,700 sawa na asilimia 87.4 zilikwisha kupatikana. Mgao wa fedha kwa watekelezaji wa Mradi huu ni kama inanvyoonekana kwenye kiambatanisho nam 2
Mradi wa Kuangamiza Kunguru Weusi
36. Mheshimiwa Spika, katika utekelezaji wa mradi huu, hadi kufikia mwezi wa Mei 2013 jumla ya kunguru 10,008 wameuliwa kwa kutumia mitego na sumu. Kwa mwaka 2012/2013, jumla ya TZS 50,000,000 zilipangwa kutumika na hadi kufikia mwezi wa Mei 2013 TZS 30,000,000 sawa na asilimia 60 zilikwisha kupatikana. Mambo yaliyofanyika kwa fedha hizo ni pamoja na kutengeneza mitego 6 na kusambazwa maeneo mbalimbali, kununua sumu ya kuulia kunguru kilo moja na nusu kutoka New Zealand, kununua vifaa mbalimbali vikiwemo mabesini, ndoo, sinia, vijiko, glavu, mapanga na majembe pamoja na kununua chambo cha kutumika kwenye sumu na mitego. Utekelezaji wa mradi huu unatarajiwa kuendelezwa na Wizara ya Kilimo na Maliasili.
Hotuba ya bajeti ya Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais 2013/14
15
Mradi wa Kuendeleza Elimu ya Mazingira
37. Mheshimiwa Spika, katika kutekeleza mradi huu, semina sita kwa kamati sita za polisi jamii za Wilaya ya kati na semina nne kwa Kamati nne za polisi jamii za Wilaya ya Mkoani zimefanyika juu ya kuzielewa na kuzitumia sheria za mazingira. Operesheni 4 za usafi wa Mazingira, zimefanyika na vifaa vya usafi kama vile mabero, mareki, gloves, na mapauro vimetolewa kwa jumuiya za Mazingira. Kwa mwaka 2012/2013, jumla ya TZS 25,000,000 zilitarajiwa kutumika , hadi kufikia mwezi wa Mei 2013 TZS 25,000,000 sawa na asilimia 100 zilikwisha kupatikana.
Mradi wa Majaribio wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi
38. Mheshimiwa Spika, katika kukamilisha utekelezaji wa mradi huu, Serikali kwa mwaka 2012/2013 ilipanga kutumia TZS 25,000,000 kwa ajili ya kulipa fidia kwa Wakulima/wananchi ambao mazao na mali zao zimeathiriwa kutokana na utekelezaji wa mradi kwa kupitisha njia ya umeme pamoja na kuchimba msingi wa kulaza mabomba ya maji. Hadi kufikia Mei 2013 jumla ya TZS 25,000,000 sawa na asilimia 100 zilikwisha kupatikana na kulipwa kwa wananchi 99.
39. Mheshimiwa Spika, Miradi miwili ambayo ni Mradi wa Kuingiza Masuala ya Watu wenye Ulemavu katika Mipango ya Maendeleo uliopangiwa kutumia TZS 25,000,000 na Mradi wa Kujenga Kituo cha Tiba na Marekebisho ya Tabia kwa watumiaji wa dawa za
Hotuba ya bajeti ya Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais 2013/14
16
kulevya huko Tunguu ulipangiwa kutumia TZS 100,000,000 hadi kufikia Mei 2013 miradi haikuingiziwa fedha .
40. Mheshimiwa Spika, Idara ya Mipango, Sera na Utafiti kwa mwaka wa fedha 2012/2013 ilikadiriwa kutumia TZS 176,251,000 kwa kazi za kawaida ambapo TZS 115,000,000 kwa ajili ya kuendeshea kazi na TZS 61,251,000 kwa ajili ya mishahara. Hadi kufikia Mei 2013 ilikwisha kuingiziwa TZS 62,500,000 sawa na asilimia 54 kwa kuendeshea kazi. Idara pia ilikadiria kutumia jumla ya TZS 255,000,000 kwa kazi za maendeleo ikiwa ni mchango wa serikali, hadi kufikia Mei 2013 ilikwisha kuingiziwa TZS 80,000,000 sawa na asilimia 31. Kwa upande wa fedha za wahisani, ilitarajia kutumia jumla ya TZS 705,600,000, hadi Mei 2013 ilikwisha kuingiziwa jumla ya TZS 616,752,700 sawa na asilimia 87.4.
MALENGO KWA MWAKA WA FEDHA 2013/2014
41. Mheshimiwa Spika, Idara ya Mipango, Sera na Utafiti kwa mwaka wa fedha 2013/14 imejipangia kutekeleza malengo yafuatayo:-
1. Kujenga uwezo wa watendaji na kufanya tafiti mbili. Tafiti ya kwanza ni kwa ajili ya kukusanya taarifa za awali juu ya hali halisi ya shughuli zinazotekelezwa na OMKR na ya pili ni utafiti wa kuangalia vikwazo vilivyopo kwa Watu Wenye Ulemavu katika sekta ya elimu na ajira kama Mpango Mkuu wa Utafiti wa OMKR unavyoelekeza.
Hotuba ya bajeti ya Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais 2013/14
17
2. Kusimamia na kutekeleza mambo mtambuka yanayosimamiwa na OMKR.
3. Kuratibu, kusimamia na kutekeleza mipango ya kazi na bajeti ya OMKR.
4. Kuimarisha mazingira ya kazi na kuwajengea uwezo wafanyakazi.
MIRADI YA MAENDELEO KWA MWAKA WA FEDHA 2013/2014
42. Mheshimiwa Spika, kwa upande wa Miradi ya Maendeleo Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais inatarajia kutekeleza miradi 2 kwa kupitia fedha za Serikali na miradi 2 kwa fedha za wahisani kama ifuatavyo:-
1. Mradi wa Kuendeleza Elimu ya Mazingira
Mradi huu una lengo la kuendelea kutoa elimu ya mazingira kwa jamii kwa madhumuni kuongeza uelewa juu ya uhifadhi endevu wa mazingira. Kwa mwaka wa fedha 2013/2014 unatarajiwa kutumia fedha za serikali TZS 50,000,000
2. Mradi wa Ujenzi wa Kituo cha Tiba na Marekebisho ya Tabia kwa watumiaji wa Dawa za Kulevya huko Tunguu
Mradi huu una lengo la kujenga kituo cha kurekebisha tabia kwa watumiaji wa dawa za kulevya ili kuwa na jamii bora. Kwa mwaka wa fedha 2013/2014 unatarajia kutumia fedha za serikali TZS 100,000,000 Hotuba ya bajeti ya Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais 2013/14
18
3. Mradi wa Kuimarisha Usimamizi wa Mazingira na Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi chini ya mradi wa UNDAP.
Mradi huu wa miaka 4 ulioanza kutekelezwa 2011/2012. utaingia katika mwaka wa 3 wa utekelezaji na unategemewa kumalizika mwaka 2014/2015. Lengo lake kuu ni kujenga uwezo kwa taasisi katika kuhakikisha masuala ya mabadiliko ya tabianchi yanaingizwa katika mipango ya sekta na kuweka mifumo mbali mbali itakayorahisisha utekelezaji wa masuala ya kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi. Kwa mwaka wa fedha 2013/2014 mradi unategemea kutumia fedha za wahisani jumla ya TZS 800,000,000.
4. Mradi wa Kujenga Uwezo wa OMKR wa UNDAP unaoratibiwa na Ofisi ya Rais Fedha, Uchumi na Mipango ya Maendeleo.
Mradi huu ni wa miaka 4 na utakuwa unaingia katika mwaka wa 3 wa utekelezaji. Lengo kuu ni kuijengea uwezo OMKR kwa kuisaidia kutengeneza miongozo mbali mbali itakayo saidia katika utekelezaji wa shughuli zake. Kwa mwaka wa fedha 2013/2014 unatarajia kutumia fedha za wahisani jumla ya TZS 200,000,000.
43. Mheshimiwa Spika, ili Idara ya Mipango, Sera na Utafiti iweze kutekeleza malengo iliyojipangia kwa mwaka wa fedha 2013/2014, naliomba Baraza lako Tukufu liidhinishe jumla ya TZS 160,065,000 kwa kuendeshea kazi. Aidha, naliomba Baraza lako Tukufu liidhinishe jumla ya TZS 150,000,000 kwa kazi za maendeleo ikiwa ni mchango wa serikali na jumla ya TZS 800,000,000 ikiwa ni mchango wa wahisani.
Hotuba ya bajeti ya Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais 2013/14
19
IDARA YA UENDESHAJI NA UTUMISHI
44. Mheshimiwa Spika, Idara hii ina majukumu ya kusimamia rasilimali watu na utawala, kusimamia masuala ya nidhamu, uwajibikaji, mafunzo na stahiki za wafanyakazi.
45. Mheshimiwa Spika, kwa mwaka wa fedha 2012/2013 Idara ya Utumishi na Uendeshaji ilijipangia kutekeleza malengo yafuatayo:-
1. Kusimamia majukumu na utendaji wa wafanyakazi.
2. Kuimarisha mazingira ya utendaji kazi.
3. Kuwajengea uwezo wafanyakazi na kuwapatia maslahi.
4. Kukuza na kuimarisha mawasiliano ya habari.
5. Kusimamia utaratibu wa udhibiti wa matumizi ya fedha
46. Mheshimiwa Spika, hadi kufikia Mei, 2013 Idara ya Uendeshaji na Utumishi imeweza kutekeleza majukumu yafuatayo:
47. Mheshimiwa Spika, kwa mwaka wa fedha 2012/13 OMKR imeajiri wafanyakazi 11; kwa kujaza nafasi zilizokuwa wazi, wafanyakazi 5 walistaafu kisheria na wafanyakazi 2 walifariki dunia; Mwenyezi Mungu azilaze roho za marehemu mahala pema peponi amin.
48. Mheshimiwa Spika katika kusimamia majukumu ya utendaji, vikao viwili vya kamati ya uongozi vya
Hotuba ya bajeti ya Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais 2013/14
20
kupitisha muongozo wa nyumba za makaazi (sober houses), Waraka wa sheria ya kukinga na kudhibiti virusi vya UKIMWI pamoja na waraka wa sheria ya marekebisho ya Tume ya UKIMWI vimefanyika. Aidha, wafanyakazi wote wameshapangiwa daraja zao kwa mujibu wa muundo wa utumishi (scheme of service).
49. Mheshimiwa Spika, katika kujenga mazingira mazuri ya ufikiaji kwa watu wenye ulemavu, "ramp" imejengwa katika jengo la OMKR. Gharama za bili mbalimbali zimelipwa; matengenezo ya gari 3, bima ya gari pamoja na ununuzi wa vifaa mbali mbali kwa matumizi ya ofisi umefanyika.
50. Mheshimiwa Spika, Wafanyakazi wawili wanaosoma katika ngazi ya Stashahada na Shahada katika fani ya Sekretari na Ugavi wamelipiwa masomo yao.Wafanyakazi wengine 3 wamesaidiwa gharama za vifaa vya kuandikia na mmoja amelipiwa posho kwa mafunzo mafupi. (rejea kiambatanisho namba 1)
51. Mheshimiwa Spika, kwa kutambua umuhimu wa jamii kupata taarifa juu ya mambo yanayotekelezwa na Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais, Ofisi imenunua televisheni moja na deki kwa ajili ya kutayarisha vipindi. Filamu fundishi moja ya watu wenye ulemavu wanaoishi katika mazingira magumu imeandaliwa na kuoneshwa katika siku ya kuchangia mfuko wa maendeleo kwa ajili ya Watu Wenye Ulemavu. Malipo ya huduma za mtandao, magazeti na uchapishaji zimelipiwa.
Hotuba ya bajeti ya Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais 2013/14
21
52. Mheshimiwa Spika, vikao viwili vya kamati ya ukaguzi wa hesabu za ndani vimefanyika ili kupitia ripoti za fedha. Vikao vinne vya zabuni na matumizi ya fedha vimeratibiwa kwa mujibu wa kanuni za fedha na sheria za manunuzi. Pia kikao kimoja kilichowajumuisha wahasibu, wakaguzi wa ndani, washika fedha na afisa manunuzi kimefanyika kwa madhumuni ya kusimamia vyema matumizi ya rasilimali za Ofisi.
53. Mheshimiwa Spika, Idara ya Uendeshaji na Utumishi kwa mwaka wa Fedha 2012/2013 ilikadiria kutumia jumla ya TZS 616,444,000 kwa kazi za kawaida. Kati ya hizo TZS 254,749,000 kwa kuendeshea kazi na TZS 361,695,000 kwa ajili ya mishahara. Hadi kufikia Mei, 2013 ilikwisha kuingiziwa kiasi cha TZS 189,372,415 sawa na asilimia 74 kwa ajili ya kuendeshea kazi.
MALENGO KWA MWAKA WA FEDHA 2013/2014
54. Mheshimiwa Spika, Idara ya Uendeshaji na Utumishi imepanga kutekeleza malengo yafuatayo:-
1. Kuimarisha mazingira ya utendaji kazi.
2. Kukuza na kuimarisha mawasiliano ya habari
3. Kuwajengea uwezo wafanyakazi na kuwapatia maslahi.
4. Kusimamia utaratibu wa matumizi ya fedha kwa mujibu wa sheria na kanuni za fedha zilizopo.
55. Mheshimiwa Spika, Ili Idara ya Uendeshaji na Utumishi iweze kutekeleza malengo iliyojipangia kwa mwaka wa
Hotuba ya bajeti ya Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais 2013/14
22
fedha 2013/2014, naliomba Baraza lako Tukufu liidhinishe jumla ya TZS 1,615,931,000 kwa kazi za kawaida. Kati ya hizo TZS 292, 427,000 kwa ajili ya kuendeshea kazi na TZS 1,323,504,000 kwa ajili ya mishahara.
IDARA YA MAZINGIRA
56. Mheshimiwa Spika, Idara hii ina majukumu ya kukusanya na kuhifadhi taarifa za kimazingira, kutoa taarifa za kimazingira ili ziweze kusaidia katika kutayarisha na kutekeleza mipango na miradi ya kimaendeleo, kufuatilia mwenendo wa hali ya kimazingira, kukabiliana na matatizo ya kimazingira, kuhamasisha wadau kuchukua hatua za kuhifadhi mazingira pamoja na kutoa elimu ya mazingira kwa jamii.
57. Mheshimiwa Spika, kwa mwaka wa fedha 2012/2013 Idara ya Mazingira ilijipangia kutekeleza malengo yafuatayo:-
1. Kusimamia uingizwaji wa masuala ya mazingira katika miradi ya maendeleo.
2. Kuongeza uwezo na kuimarisha muundo wa kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi.
3. Kuimarisha usimamizi endelevu wa maliasili.
4. Kuongeza uwelewa wa elimu ya mazingira kwa jamii na wadau wengine.
5. Kuimarisha utekelezaji wa Sera, Sheria na Kanuni za mazingira.
6. Kuimarisha mazingira ya kazi na kuwajengea uwezo wafanyakazi.
Hotuba ya bajeti ya Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais 2013/14
23
58. Mheshimiwa Spika, hadi kufikia Mei 2013 Idara imeweza kutekeleza yafuatayo katika malengo iliyojipangia:-
59. Mheshimiwa Spika, jumla ya miradi 65 ya mahoteli imekaguliwa, miradi 15 ya uwekezaji imefanyiwa Tathmini ya Athari ya Kimazingira (EIA) na kutolewa vyeti vya Mazingira na miradi 5 imefanyiwa uchunguzi wa awali wa kimazingira (scoping) ili kutoa hadidu rejea za kufanya Tathmini za Athari za Kimazingira (angalia kiambatanisho nam. 3). Kiwanda cha Makonyo cha Wawi, Pemba kimefanyiwa ukaguzi wa kimazingira na ripoti ya ukaguzi huo imewasilishwa Wizara ya Biashara, Viwanda na Masoko kwa kuchukuliwa hatua za utekelezaji wa mapendekezo yaliyotolewa.
60. Mheshimiwa Spika, katika kusimamia utekelezaji wa mabadiliko ya tabianchi ngazi ya shehia, kamati kumi za majaribio za usimamizi wa ukanda wa pwani (Intergrated Coastal Zone Managemant – ICZM) zimesaidiwa kuandaa mipango ya utekelezaji wa usimamizi wa mazingira katika maeneo yao; Unguja na Pemba. Kamati hizi zimetayarisha mipango ya utekelezaji ya usimamizi wa mazingira katika maeneo yao. Katika kuziongezea uwezo kamati hizo, mipango ya ICZM ya Shehia za Nungwi na Chwaka imesaidiwa utekelezaji kwa kununuliwa vifaa vya usafi. Aidha, mipango ya ICZM ya Shehia za Mtende na Nyamanzi imesaidiwa kwa kupatiwa miti ya aina mbali mbali ikiwemo ya matunda na misitu.
Hotuba ya bajeti ya Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais 2013/14
24
61. Mheshimiwa Spika, Kamati hizi huwezesha Idara ya Mazingira kuwa na mawasiliano na jamii katika kusimamia masuala ya mabadiliko ya tabianchi na kuimarisha muundo wa usimamizi wa masuala ya mabadiliko ya tabianchi katika ngazi ya shehia. Warsha ya siku moja ya mabadiliko ya tabianchi na Mpango wa Kupunguza Hewa Ukaa kutokana na Uharibifu wa Misitu na Ukataji Ovyo wa Miti kwa Makatibu Wakuu, Manaibu Makatibu Wakuu na Wakurugenzi wa Mipango, Sera na Utafiti wa Wizara zote za Serikali imefanyika.
62. Mheshimiwa Spika, katika kuimarisha usimamizi endelevu wa maliasili, Kanuni za usimamizi endelevu wa maliasili zisizorejesheka zimeandaliwa na kuchapishwa katika Gazeti Rasmi la Serikali la tarehe 15 Febuari 2013. Warsha moja ya wadau juu ya Kanuni hiyo imefanyika. Usimamizi wa Kanuni hiyo kwa ajili ya kupunguza vitendo vya uchukuaji usiofuata taratibu wa maliasili zisizorejesheka utafanyika mwaka wa fedha wa 2013/2014. Aidha, Ekari 15 za eneo la Uwandani Pemba lililochimbwa matofali ya mawe zimefukiwa. Jumla ya miti 2,525 imepandwa katika maeneo yaliyofukiwa, kati ya miti hiyo, 500 ni ya matunda ikiwemo michungwa, miembe na mifenesi; na miti 2,025 ni ya misitu ikiwemo mikungu, mitondoo na mivinje.
63. Mheshimiwa Spika, katika suala la kuongeza uelewa wa elimu ya mazingira kwa jamii na wadau wengine, jumla ya vipindi 15 vya redio na vipindi 3 vya TV vinavyohusu usimamizi wa mazingira vimerushwa hewani, jumuiya na Kamati za Mazingira 8 zimepatiwa elimu ya Mazingira (angalia kiambatanisho 4).
Hotuba ya bajeti ya Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais 2013/14
25
64. Mheshimiwa Spika, katika kuhakikisha kwamba Sera, Sheria na Kanuni za mazingira zinatekelezwa, jumla ya operesheni 117 zimefanyika Unguja na Pemba na watu 33 wamekamatwa na kuhukumiwa kwa faini ya TZS 3,280,000 kwa jumla. Aidha, kilo 670 za mifuko ya plastiki zimeteketezwa katika eneo la Maruhubi. Aidha, Sera mpya ya Mazingira imeandaliwa na kuidhinishwa na Serikali na Mpango wa Utekelezaji wa Usimamizi wa Mazingira umeandaliwa kwa mujibu wa Sera Mpya ya Mazingia.
65. Mheshimiwa Spika, wafanyakazi 7 wamelipiwa sehemu ya gharama za mafunzo ya ngazi za Cheti na Stashahada katika fani za Utumishi wa Umma (3), Ukutubi (1), Kingereza (1), na Ukatibu Muhtasi (2), Wafanyakazi 5 wamelipiwa mafunzo mafupi ya usimamizi wa Mazingira katika vyuo vya Tanzania Bara. (rejea kiambatanisho namba 1).
66. Mheshimiwa Spika, Idara ya Mazingira kwa mwaka wa fedha 2012/2013 ilikadiriwa kutumia TZS 369,369,000 kwa kazi za kawaida kati ya hizo TZS 112,373,000 kwa ajili ya kuendeshea kazi na TZS 257,296,000 kwa ajili ya mishahara. Hadi kufikia Mei 2013 ilikwisha kuingiziwa jumla ya TZS 68,600,000 sawa na asilimia 61 kwa kuendeshea kazi. Aidha Idara ya Mazingira ilipangiwa kukusanya jumla yaTZS 10,800,000 kutokana na huduma ya tathmini za athari za kimazingira. Hadi kufikia mwezi Mei 2013, Idara imefanikiwa kukusanya jumla ya shilingi 6,830,000 sawa na asilimia 63.
Hotuba ya bajeti ya Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais 2013/14
26
MALENGO KWA MWAKA 2013/2014
67. Mheshimiwa Spika, Idara ya Mazingira kwa mwaka wa fedha 2013/14 imejipangia kutekeleza malengo yafuatayo:-
1. Kuimarisha usimamizi wa udhibiti wa uchafuzi wa mazingira.
2. Kuimarisha usimamizi endelevu wa maliasili.
3. Kukuza uelewa wa elimu ya mazingira kwa jamii na wadau wengine wa Mazingira
4. Kuimarisha mazingira ya utendaji kazi na kuwajengea uwezo wafanyakazi
5. Kuimarisha na kusimamia utekelezaji wa Mikakati, Sera, Sheria na Kanuni.
68. Mheshimiwa Spika, ili Idara ya Mazingira iweze kutekeleza malengo iliyojipangia kwa mwaka wa fedha 2013/2014, naliomba Baraza lako Tukufu liidhinishe jumla ya TZS 127,884,000 kwa ajili ya kuendeshea ya kazi.
69. Mheshimiwa Spika, Idara ya Mazingira kwa mwaka wa fedha 2013/2014, imepangiwa kukusanya jumla ya TZS 10,500,000 kutokana na ada ya hifadhi ya mazingira ikwa ni pamoja na Vyeti vya Mazingira.
Hotuba ya bajeti ya Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais 2013/14
27
IDARA YA WATU WENYE ULEMAVU
70. Mheshimiwa Spika, Idara hii ina majukumu ya kuratibu masuala mbali mbali ya watu wenye ulemavu kwa mujibu wa Sheria No. 9 ya mwaka 2006.
71. Mheshimiwa Spika, kwa mwaka wa fedha 2012/2013 Idara ya Watu Wenye Ulemavu ilijipangia kutekeleza malengo yafuatayo:-
1. Kuratibu Shughuli za Baraza la Taifa la Watu wenye Ulemavu.
2. Kuwapatia visaidizi na kuimarisha juhudi za taasisi katika kushughulikia masuala ya Watu wenye Ulemavu.
3. Kuandaa na kusimamia utekelezaji wa Sera, Sheria na kanuni za Watu wenye Ulemavu.
4. Kuimarisha mazingira mazuri ya kazi na kujenga uwezo wa wafanyakazi katika kuleta ufanisi.
72. Mheshimiwa Spika, hadi kufikia Mei 2013, Idara ya Watu Wenye Ulemavu imeweza kutekeleza yafuatayo katika malengo iliyojipangia:-
73. Mheshimiwa Spika, vikao vinne vya Baraza la Taifa la Watu wenye Ulemavu vimefanyika na kujadili mambo mbali mbali yanayowahusu Watu wenye Ulemavu. Miongoni mwa mambo yaliyojadiliwa ni matayarisho ya maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Watu wenye Ulemavu ambayo hufanyika kila ifikapo tarehe 3
Hotuba ya bajeti ya Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais 2013/14
28
Disemba. Kwa mwaka huu wa fedha maadhimisho hayo yalifanyika kisiwani Pemba ambayo yametoa muamko kwa jamii juu ya haki na fursa sawa kwa watu wenye ulemavu. Ujumbe wa maadhimisho ya mwaka huu ni "ONDOA VIKWAZO ILI KUJENGA JAMII JUMUISHI KWA WOTE".
74. Mheshimiwa Spika, Jumuiya 10 za Watu wenye Ulemavu zimepatiwa ruzuku ya TZs 1,700,000 kwa kila moja kwa ajili ya kuendesha shughuli zao za kawaida. Jumuiya hizo ni CHAVIZA, ZANAB, UWZ, JMZ, SAD’Z, JUWAUZA, ZADA, ZACDID, ZAPDD na SOZ. Utoaji wa ruzuku hizo ni miongoni mwa juhudi za Serikali katika kuhakikisha jumuiya za watu wenye ulemavu zinatekeleza vyema shughuli za kuwahudumia wadau wao.
75. Mheshimiwa Spika, Shughuli ya chakula cha usiku kwa ajili ya kuchangia kutunisha Mfuko wa Maendeleo ya Watu Wenye Ulemavu ambao ulianzishwa kwa mujibu ya Sheria namba 9 ya mwaka 2006 ilifanyika. Mfuko huo kwa hivi sasa una jumla ya TZS 158,157,319. Idara inaendelea kuzifuatilia ahadi za michango ambayo bado haijawasiliswa. Aidha, Idara ilipokea misaada ya visaidizi vya Watu Wenye Ulemavu kutoka kwa Umoja wa Wazanzibari wanaoishi Canada (ZANCANA), Kampuni ya Bobar pamoja na watu wengine mmoja mmoja. Misaada hiyo iligaiwa kwa wahusika.
76. Mheshimiwa Spika, katika kuhakikisha mazingira mazuri ya utendaji na kuleta ufanisi kazini, jumla ya wafanyakazi watatu wamechangiwa gharama za masomo, katika mafunzo ya Shahada ya pili ya Sheria,
Hotuba ya bajeti ya Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais 2013/14
29
Shahada ya kwanza ya IT, na Stashahda ya uhasibu. (rejea kiambatanisho namba 1)
77. Mheshimiwa Spika, jumla ya Shehia 19 za Mkoa wa Mjini Magharibi na 3 za Mkoa wa Kusini Unguja zimefanyiwa uhamasishaji, wazee wa watoto wenye ulemavu na wazee wa watoto wasio na ulemavu walishiriki katika zoezi hilo. Uhamasishaji huo ulikuwa juu ya kuinua uwelewa katika masuala ya haki za watu wenye ulemavu, Mkataba wa Kimataifa wa haki za watu wenye ulemavu na Sera ya Maendeleo kwa Watu wenye Ulemavu. (angalia kiambatanisho nam 5). Vikao vinne vya maafisa waratibu wa masuala ya Watu wenye Ulemavu vimefanyika ili kufuatilia utekelezaji wa Sheria ya Haki na Fursa sawa kwa Watu wenye Ulemavu hapa Zanzibar.
78. Mheshimiwa spika, katika kuendeleza usajili wa watu wenye ulemavu jumla ya wilaya 9 zimefanyiwa usajili ikiwa wilaya tano za unguja na wilaya nne za Pemba kwa ajili ya kuweza kupata takwimu sahihi na kurahisisha upangaji wa Sera na Mipango ya Maendeleo kwa Watu wenye ulemavu(angalia kiambatanisho nam 6).
79. Mheshimiwa Spika, Idara ya Watu Wenye Ulemavu kwa mwaka wa fedha 2012/2013 ilikadiriwa kutumia TZS 532,562,000 kwa kazi za kawaida kati ya hizoTZS 435,570,000 kwa kuendeshea kazi na TZS 99,992,000 kwa ajili ya mishahara. Hadi kufikia Mei 2013 ilikwisha kuingiziwaTZS 391,000,000 sawa na asilimia 92.8 kwa kuendeshea kazi.
Hotuba ya bajeti ya Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais 2013/14
30
MALENGO KWA MWAKA WA FEDHA 2013/2014
80. Mheshimiwa Spika, Idara ya Watu Wenye Ulemavu kwa mwaka wa fedha 2013/14 imejipangia kutekeleza malengo yafuatayo:-
1. Kuimarisha Mazingira ya Utendaji kazi..
2. Kutengeneza mfumo wa takwimu (data base) za Watu wenye Ulemavu
3. Kusimamia haki, fursa sawa na ujumuishwaji wa Watu wenye Ulemavu.
81. Mheshimiwa Spika, ili Idara ya Watu Wenye Ulemavu iweze kutekeleza majukumu iliyojipangia kwa mwaka fedha 2013/2014, naliomba Baraza lako Tukufu liidhinishe jumla ya TZS 396,782,000 kwa ajili ya kuendeshea kazi.
OFISI YA MAKAMO WA KWANZA WA RAIS PEMBA
82. Mheshimiwa Spika, Ofisi hii ina jukumu la kuratibu, kusimamia na kufuatilia utekelezaji wa shughuli zote za Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais kwa upande wa Pemba.
83. Mheshimiwa Spika, Ofisi Kuu Pemba kwa mwaka wa fedha 2012/2013 ilijipangia malengo yafuatayo:-
1. Kusimamia na Kuratibu utekelezaji wa shughuli zote za Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Pemba
2. Kuimarisha mazingira ya kazi na kuwajengea uwezo wafanyakazi.
Hotuba ya bajeti ya Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais 2013/14
31
3. Kukuza na kuimarisha mawasiliano ya habari.
4. Kusimamia na kuratibu udhibiti wa matumizi ya fedha.
84. Mheshimiwa Spika, hadi kufikia Mei 2013 Ofisi Kuu Pemba imeweza kutekeleza yafuatayo katika malengo iliyojipangia:-
85. Mheshimiwa Spika, katika kusimamia na kuratibu utekelezaji wa shughuli za Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Pemba, Elimu juu ya athari za dawa za kulevya ilitolewa katika skuli za sekondari 17 ambapo jumla ya wanafunzi 1,117 (wanaume 540, wanawake 577) na walimu 49 (wanaume 40, wanawake 9) walifikiwa. (angalia kiambatanisho nam 7). Aidha, tathimini ilifanywa kwa Mateja walioingia sober house iliyojumuisha vijana 181. Tathmini hiyo iliangalia uhakiki wa njia za matumizi ya dawa na kutoa matokeo ambayo yalionesha wanaotumia dawa kwa njia ya kujidunga sindano (IDUs) – 108 na wanaotumia dawa kwa uvutaji unga (SUs )- 73
86. Mheshimiwa Spika, ziara ya kupitia kila Wilaya ili kuyatambua mahitaji ya watu wenye ulemavu kwa ajili ya kupatiwa visaidizi ilifanyika, kufuatia ziara hiyo watu wenye ulemavu kutoka Shehia mbali mbali walipatiwa visaidizi ili kuwarahisishia kupata mahitaji yao. Ziara nyengine iliyofanyika ni kutembelea vikundi vya ushirika na ujasiriamali vya watu wenye ulemavu kwa mkoa wa kaskazini Pemba. Vikundi hivyo ni pamoja na kikundi cha wasioona (ZANAB) Wete, Kikundi cha Tuimarishe cha Kianga Ole, Vikundi vya Hirimu Mfasi
Hotuba ya bajeti ya Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais 2013/14
32
na Tupendane vya Micheweni pamoja na Mwanzomgumu cha Shumba mjini.
87. Mheshimiwa Spika, katika kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi OMKR inaendelea kufanya ufuatiliaji wa maeneo yalioathirika kutokana na uharibifu unaojitokeza, jumla ya maeneo 18 yametembelewa ili kujionea uharibifu wa mazingira unaosababishwa na uingiaji wa maji chumvi na ukataji ovyo wa mikoko. (Aidha, maeneo yaliyoathirika na uharibifu wa mazingira kutokana na uchimbaji wa mchanga Kangani na ukataji matofali Mwambe yalitembelewa ili kuona ni hatua gani zinaweza kuchukuliwa kunusuru hali iliyopo. Mikutano ya kushauriana juu matokeo ya athari za uharibifu wa mazingira na migogoro iliyopo miongoni mwa wananchi imefanyika na maagizo yametolewa kwa wananchi wa maeneo husika kukubali kufanya yale yaliyo katika uwezo wao kwa hatua za awali.
88. Mheshimiwa Spika, katika kuimarisha mazingira bora ya kazi shughuli mbali mbali za kiutawala na uendeshaji zimefanyika ikiwemo kulipa gharama mbali mbali za huduma, matengenezo ya gari, bima ya gari, ulipaji wa kodi ya jengo la ofisi pamoja na ununuzi wa vifaa mbali mbali kwa matumizi ya ofisi. Aidha katika kuimarisha mawasiliano ya habari, kamera 1 (Digital) imenunuliwa kwa ajili ya usambazaji na ufuatiliaji wa taarifa mbali mbali za utekelezaji.
89. Mheshimiwa Spika, Ofisi hii kwa mwaka wa Fedha 2012/2013 ilikadiria kutumia jumla ya TZS 316,659,000 kwa kazi za kawaida. Kati ya hizo TZS
Hotuba ya bajeti ya Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais 2013/14
33
157,774,000 kwa kuendeshea kazi na TZS 158,596,000 kwa ajili ya mishahara. Hadi kufikia Mei 2013 ilikwisha kuingiziwa kiasi cha TZS 77,189,906 sawa na asilimia 49 kwa matumizi ya kuendeshea kazi.
MALENGO KWA MWAKA WA FEDHA 2013/2014
90. Mheshimiwa Spika, Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Pemba kwa mwaka wa fedha 2013/14 imejipangia kutekeleza malengo yafuatayo:-
1. Kuwajengea uwezo wafanyakazi na kuwapatia maslahi.
2. Kuimarisha mazingira ya utendaji kazi.
3. Kuratibu na kusimamia utekelezaji wa shughuli za OMKR Pemba.
4. Kukuza na kuimarisha mawasiliano ya habari
91. Mheshimiwa Spika, ili Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Pemba iweze kutekeleza majukumu iliyojipangia kwa mwaka wa fedha 2013/2014, naliomba Baraza lako Tukufu liidhinishe jumla ya TZS 330,175,000 kwa kazi za kawaida kati ya hizo TZS 167,575,000 kwa kuendeshea kazi na TZS 162,600,000 kwa ajili ya malipo ya mishahara.
TUME YA KURATIBU NA UDHIBITI WA DAWA ZA KULEVYA
92. Mheshimiwa Spika, Tume hii ina jukumu la kuratibu mapambano dhidi ya biashara, matumizi, uingizwaji na usafirishaji wa dawa za kulevya. Tume pia ina jukumu la kutoa taaluma kwa jamii pamoja na kutoa huduma za
Hotuba ya bajeti ya Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais 2013/14
34
tiba na ushauri nasaha kwa watumiaji wa dawa za kulevya.
93. Mheshimiwa Spika, kwa mwaka wa Fedha 2012/2013 Tume ya Kuratibu na Udhibiti wa Dawa za Kulevya ilijipangia malengo yafuatayo:-
1. Kuratibu na kuendeleza mapambano dhidi ya uingizaji na usafirishaji wa dawa za kulevya.
2. Kuimarisha mazingira mazuri ya kazi katika kuleta ufanisi.
3. Kuongeza mwamko wa jamii juu ya athari na udhibiti wa dawa za kulevya.
4. Kuratibu na kuimarisha juhudi za taasisi katika kushughulikia mapambano dhidi ya dawa za kulevya
94. Mheshimiwa Spika, hadi kufikia Mei 2013 Tume ya Kuratibu na Udhibiti wa Dawa za Kulevya imeweza kutekeleza yafuatayo katika malengo iliyojipangia:-
95. Mheshimiwa Spika, ili kuhakikisha Sheria ya Dawa ya Kulevya inatekelezeka "Road Map" ya utekelezaji wa sheria hiyo imeandaliwa na kuekewa makisio ya fedha zinazo hitajika kwa ajili ya utekelezaji kwa kilawadau, Aidha mkutano wa kwanza wa Tume ya Kitaifa ya Dawa za Kulevya umefanyika ambapo uliweza kujadili mambo mbali mbali yenye lengo la kuendeleza mbele vita dhidi ya dawa za Kulevya.
96. Mheshimiwa Spika, juhudi za taasisi zinazohusika na mapambano ya Dawa za Kulevya pamoja na
Hotuba ya bajeti ya Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais 2013/14
35
mashirikiano kutoka kwa raia wema zinaendelea vizuri. Jumla ya watu 22 wamekamatwa kwa makosa ya dawa za Kulevya kati yao (wanaume 21 na wanawake 1) na kesi 21 ziko mahakamani na upelelezi unaendelea. Katika kuona kwamba sheria ya Udhibiti wa dawa za kulevya inatekelezwa ipasavyo Rasimu ya kanuni ya sheria hiyo tayari imeshaandaliwa.
97. Mheshimiwa Spika, katika kuhakikisha jamii inapata mwamko juu ya athari na udhibiti wa dawa za kulevya, vipindi 10 vilivyolenga kuinua mwamko wa jamii juu ya athari ya dawa za kulevya vimerushwa hewani kupitia vyombo mbali mbali vya habari viliopo nchini vinavyomilikiwa na Serikali na taasisi binafsi kama vile: Zenji FM, ZBC, HITS FM na Bomba FM. Aidha filamu fundishi kuhusiana na athari za dawa za kulevya imetayarishwa ambayo itatumika katika programu na vipindi vya kuhamasisha jamii.
98. Mheshimiwa Spika, Tume pia iliandaa ziara katika skuli za Serikali na Binafsi. Jumla ya wanafunzi 6,270 (wanawake 3,677 na wanaume 2,593) kutoka skuli 45 za Unguja wamepatiwa elimu juu ya athari za Dawa za Kulevya na maambukizi ya virusi vya UKIMWI. (rejea kiambatanisho namba 7). Ziara za utoaji wa elimu katika shehia mbali mbali za Unguja, kwa lengo la kuonana na kamati za ulinzi na Polisi jamii za shehia hizo ambapo jumla ya shehia tano za Mkoa wa Mjini/Magharibi ambazo zinaonekana kuathirika zaidi na biashara ya Dawa za Kulevya na matumizi yake yanayochangia maongezeko ya uhalifu katika jamii zilifanyika.
Hotuba ya bajeti ya Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais 2013/14
36
99. Mheshimiwa Spika, kwa kutambua mchango wa taasisi zisizo za kiserikali katika mapambano dhidi ya dawa za kulevya, Tume tayari imeshazipatia ruzuku nyumba tisa za makaazi ya vijana wanaoacha matumizi ya dawa za kulevya (Sober Houses) kwa ajili ya kusaidia mahitaji mbali mbali.(angalia kiambatanisho Nam.8).
100. Mheshimiwa Spika, katika kuimarisha mazingira mazuri ya kazi na kuleta ufanisi, mfanyakazi mmoja anaendelea kulipiwa masomo kwa ngazi ya Diploma ya Uhasibu katika Chuo Cha Maendeleo ya Utalii kilichopo Maruhubi–Unguja. (rejea kiambatanisho namba1).
101. Mheshimiwa Spika, Tume ya Kuratibu na Udhibiti wa Dawa za Kulevya kwa mwaka wa fedha 2012/2013 ilikadiriwa kutumia TZS 247,091,000 kwa kazi za kawaida. Kati ya hizo TZS 146,607,000 kwa kuendeshea kazi na TZS 100,684,000 kwa ajili ya mishahara. Hadi kufikia Mei 2013 ilikwisha ingiziwa TZS 66,435,000 sawa na asilimia 45 kwa kuendeshea kazi.
MALENGO KWA MWAKA WA FEDHA 2013/2014
102. Mheshimiwa Spika, Tume ya Kuratibu na Udhibiti wa Dawa za Kulevya kwa mwaka wa fedha 2013/14 imejipangia kutekeleza malengo yafuatayo;
1. Kupunguza matumizi ya Dawa za Kulevya.
2. Kupunguza usafirishaji, uzalishaji na usambazaji wa Dawa za Kulevya
Hotuba ya bajeti ya Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais 2013/14
37
3. Kuweka mazingira bora ya kazi na kuleta ufanisi katika mapambano dhidi ya dawa za kulevya
103. Mheshimiwa Spika, ili Tume ya Kuratibu na Udhibiti wa Dawa za Kulevya iweze kutekeleza malengo iliyojipangia kwa mwaka wa fedha 2013/2014, naliomba Baraza lako Tukufu liidhinishe jumla ya TZS 160,117,000 kwa kwaajili ya kuendeshea kazi.
TUME YA UKIMWI
104. Mheshimiwa Spika, majukumu makuu ya Tume ya UKIMWI ni kuhakikisha kwamba sera na mikakati ya taifa ya kupiga vita UKIMWI zinaandaliwa na kutekelezwa, kutafuta rasilimali zitakazotumika katika utekelezaji wa muitiko wa kitaifa wa kupambana na UKIMWI, kuimarisha uwezo wa wadau katika kufanyia kazi programu za UKIMWI na kuratibu shughuli zao, kushajihisha utoaji wa huduma za tiba na matunzo kwa watu walioathirika na kuathiriwa, kufuatilia na kutathmini umakini na ufanisi wa utekelezaji wa mikakati, sera na muitiko wa kitaifa na kutoa taarifa zote zinazohusiana na UKIMWI.
105. Mheshimiwa Spika, Tume ya UKIMWI kwa mwaka wa fedha 2012/2013 ilijipangia malengo yafuatayo:-
Hotuba ya bajeti ya Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais 2013/14
38
1. Kuimarisha mazingira mazuri ya wafanyakazi wa Tume kwa ajili ya kuleta ufanisi katika shughuli za uratibu wa masuala ya UKIMWI.
2. Kuongeza uwezo wa programu za habari, utetezi na mawasiliano ili kuchochea mabadiliko ya tabia katika jamii na makundi maalum.
3. Kuimarisha Uratibu na Utekelezaji wa Sera na Sheria na Mkakati wa Taifa wa Pili wa kupambana na UKIMWI.
4. Kuongeza utumiaji wa taarifa zinazotokana na Ufuatiliaji, Tathmini na utafiti katika programu za UKIMWI.
5. Kusimamia utaratibu wa udhibiti wa matumizi ya fedha.
106. Mheshimiwa Spika, hadi kufikia Mei 2013 Tume ya UKIMWI imeweza kutekeleza yafuatayo katika malengo iliyojipangia:-
107. Mheshimiwa spika, katika kuimarisha mazingira mazuri ya wafanyakazi wa tume kwa ajili ya kuleta ufanisi katika shughuli za uratibu wa masuala ya UKIMWI Stahiki za likizo kwa wafanyakazi 2 na malimbikizo ya mishahara kwa wafanyakazi 3 zimelipwa. Wafanyakazi 3 wanaosoma fani za Uhasibu (1), Uongozi (1) na Manunuzi (1) wamelipiwa gharama za masomo. Malipo ya huduma mbalimbali zikiwemo ununuzi wa mafuta kwa kurahisisha ufuatiliaji wa kazi, matengenezo ya gari na ofisi, malipo ya maji, ulinzi, umeme, mtandao kwa kurahisisha mawasiliano, vifaa vya kuandikia yamefanyika.
Hotuba ya bajeti ya Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais 2013/14
39
108. Mheshimiwa Spika, ili kuhakikisha ufanisi katika kuongeza uwezo wa program za habari, utetezi na mawasiliano kwa kuchochea mabadiliko ya tabia katika masuala ya UKIMWI, nyumba tano za makaazi ya vijana walioacha dawa za kulevya (Sober houses) zimesaidiwa kwa kununuliwa televisheni na radio moja kila nyumba. katika muendelezo wa kuelimisha makundi maalum kwa kuwatumia waelimishaji rika , idadi ya dada poa 307, kaka poa 38, na wanaojidunga sindano 271,wameweza kufikiwa kupitia katika mikusanyiko mbali mbali . Pia, taasisi za dini zimeweza kuhamasisha waumini wao wapatao 380 kupitia katika mikusanyiko ya kidini juu ya mbinu bora za kutumia huduma za kuzuia maambukizo ya UKIMWI, kupanua upatikanaji wa taarifa za afya ya uzazi pamoja na kuwepo kwa usawa wa kijinsia kuhusiana na elimu ya UKIMWI.
109. Mheshimiwa Spika, Elimu ya UKIMWI inayohusu mpango wa kuimarisha uwezo wa jamii kupambana na UKIMWI (Community Capacity Enhancement Programme – CCE) imetolewa kwa shehia mbali mabli za Unguja na Pemba.jumla ya shehia 21 zimeweza kufikiwa Unguja na Pemba.
110. Mheshimiwa Spika, jarida la JIHADHARI toleo nambari 16 limechapishwa na kusambazwa kwa wadau kwa lengo la kutoa habari kwa jamii. Maadhimisho ya siku ya UKIMWI Duniani yamefanyika tarehe 1/12/2012 ambapo kilele chake kilifanyika Mangapwani, Wilaya ya Kaskazini B Unguja. Lengo kuu la maadhimisho hayo lilikuwa ni kuihamasisha jamii juu ya kujikinga na UKIMWI. Any new son the new data.
Hotuba ya bajeti ya Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais 2013/14
40
111. Mheshimiwa Spika, Katika kuimarisha uratibu wa shughuli za UKIMWI nchini, Tume imefanya mikutano ya uratibu kwa wadau mbalimbali ikiwemo taasisi za Serikali , taasisi zisizo za kiserikali, kamati za UKIMWI za Wilaya na Shehia, jumuia ya wafanyabiashara, na taasisi za viongozi wa dini. Mikutano 12 (6 Unguja na 6 Pemba) imeweza kufanyika na kuhusisha watu 253. Mikutano hiyo imetusaidia kujua maendeleo ya utekelezaji wa shughuli za UKIMWI zinazotekelezwa na taasisi hizo pamoja na changamoto zilizomo katika maeneo yao. Kwa kutambua umuhimu wa kupata taarifa kwa watu wenye mahitaji maalumu, mkakati wa mawasiliano na utetezi umechapishwa kwa lugha ya wasioona.
112. Mheshimiwa Spika, katika kuendelea na utekelezaji wa Mkakati wa Pili wa Taifa wa kupambana na UKIMWI, Mapitio ya Sheria ya Tume ya UKIMWI Nam. 3 ya mwaka 2002 yamefanyika na rasimu ya mswada wa marekebisho yake yanatarajiwa kuwasilishwa kwenye kikao kinachofuata cha Baraza la Wawakilishi. Aidha, mapitio ya Sera yamefanyika, na rasimu ya Sera ya UKIMWI inaendelea kuandikwa kwa lugha nyepesi (popular version) ili kuifanya jamii na wadau wengine kuielewa na kuitekeleza kwa urahisi.Warsha ya siku mbili kwa Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi ilifanyika kwa lengo la kuwaongezea uelewa pamoja na kupata michango yao juu ya rasimu za sheria, sera na mkakati wa utetezi na mawasiliano. Pia, Tume imeandaa mkakati wa kutafuta rasilimali na tayari umewasilishwa kwa kamati ya wataalamu na kupatiwa maoni. Vile vile, warsha ya kuzijengea uwezo taasisi za Serikali na zisizokuwa za serikali juu ya namna ya kuingiza masuala
Hotuba ya bajeti ya Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais 2013/14
41
ya UKIMWI katika mipango na kazi zao za kila siku ilifanyika, jumla ya watu 42 walishiriki katika mafunzo hayo kutoka Unguja na Pemba.
113. Mheshimiwa Spika:Katika kuimarisha mwitiko wa jamii kupambana na UKIMWI, Tume imeweza kuzisaidia Shehia 22 kuibua mipango kazi ya UKIMWI na udhalilishaji wa jinsia kwa ajili ya utekelezaji. Aidha, Tume imeendesha mafunzo ya wiki mbili kwa wakufunzi 15 juu ya program ya kuzijengea uwezo Shehia kupambana na UKIMWI. Washiriki hao wametoka katika taasisi za Serikali na zisizo za kiserikali na ndani ya jamii kwa ujumla. Tayari wameshaanza kazi za kuwafundisha wajumbe wa kamati za UKIMWI za shehia, Vile vile, Tume imefanya mafunzo kwa kamati za shehia 10 ( 6 Unguja, 4 Pemba) zinazosimamia programu za kuimarisha uwezo wa jamii kupambana na UKIMWI na udhalilishaji wa kijinsia, utetezi na haki za binadamu.
114. Mheshimiwa Spika, katika kukabiliana na mabadiliko ya tabia kwa vijana ikiwemo utumiaji wa dawa za kulevya, zinaa, wizi nk, Tume imetayarisha nakala rahisi ya kiongozi cha mafunzo ya mawasiliano kati ya mzazi na mtoto (parent child comunication guide) kwa ajili ya kuwawezesha wazazi kuwa na mawasiliano na watoto wao juu ya afya ya uzazi na UKIMWI.
115. Mheshimiwa Spika, utafiti wa mwisho uliofanywa wa HIV na Malaria umeonesha wanawake na wanaume wenye umri wa miaka 15-49 walifanyiwa uchunguzi wa damu kwa kupimwa maambukizi ya VVU na UKIMWI.
Hotuba ya bajeti ya Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais 2013/14
42
Utafit huo umeonyesha kwamba kiwango cha maambukizi ya VVU Tanzania kwa mwaka 2011/2012 kimepungua kutoka 5.7(Takwimu 2007) hadi 5.1, hii ni afadhali kidogo kwa Tanzania kwa ujumla. Lakini Kwa upande wa Zanzibar, kiwango cha maambukizi hayo kimepanda kutoka asilimia 0.6 (takwimu 2007) hadi asilimia 1, ongezeko hili kwa upande wetu ni kubwa. Hali hii inahitaji nguvu za pamoja kwa Serikali na wananchi wote kuhakikisha kwamba maambukizi zaidi yana dhibitiwa Taarifa kamili kwa mikoa yote mitano angalia kiambatanisho nam 9.
116. Mheshimiwa Spika, jumuia ya Watu Wanaoishi na Virusi vya UKIMWI (ZAPHA+) ni moja kati ya taasisi za kiraia muhimu sana inayotoa mchango mkubwa katika mapambano dhidi ya UKIMWI. ZAPHA+ imejengewa uwezo juu ya mbinu za utafutaji wa rasilimali fedha kwa ajili ya kuendeleza mbele mapambano dhidi ya UKIMWI. Kupitia Tume ya UKIMWI, ZAPHA+ wamepatiwa jumla ya TZS 551,471,765 na wahisani kwa kufanya shughuli zao za uratibu.
117. Mheshimiwa Spika, ziara za ukaguzi wa ndani wa hesabu zimefanyika kuwatembelea wadau mbali mbali Unguja na Pemba kufuatilia na kufanya uhakiki wa mahesabu kwa wadau wanaopata fedha kupitia Tume ya UKIMWI Zanzibar.
118. Mheshimiwa Spika, Tume ya UKIMWI kwa mwaka wa fedha 2012/2013 ilikadiriwa kutumia TZS milioni 739,000,000 kwa kazi za kawaida. Kati ya hizo TZS 500,838,000 kwa ajili ya kuendeshea kazi na TZS 238,162,000 kwa ajili ya kulipia mishahara. Hadi
Hotuba ya bajeti ya Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais 2013/14
43
kufikia Mei 2013 Tume ilikwisha kuingiziwa TZS 280,035,552 sawa na asilimia 56 kwa ajili ya kuendeshea kazi. Aidha, Tume iliidhinishiwa TZS 50,000,000 kwa kazi za maendeleo kutokana na mchango wa Serikali. Hadi kufikia Mei 2013, ilikwisha ingiziwa TZS 15,000,000 sawa na asilimia 30. Kwa upande wa fedha za wahisani Tume ilikadiriwa kupatiwaTZS 893,760,000. Hata hivyo kutokana na kupata fedha zaidi kutoka kwa wahisani baada ya bajeti ilitarajia kupata 1,604,700,000. Hadi kufikia Mei 2013, jumla ya TZS 1,187,016,000 sawa na asilimia 74 zilikwisha kupatikana (angalia kiambatanisho namba 10).
MALENGO KWA MWAKA WA FEDHA 2013/2014
119. Mheshimiwa Spika, Tume ya UKIMWI kwa mwaka wa fedha 2013/14 imejipangia kutekeleza malengo yafuatayo:-
1. Kuongoza, kuratibu na kusimamia utekelezaji wa Sera, Sheria na Mkakati wa Pili wa Kitaifa wa UKIMWI kwa wadau wote.
2. Kuimarisha ubora wa taarifa zinazokusanywa pamoja na kufuatilia matumizi ya taarifa zinazotokana na ufuatiliaji, tathmini na utafiti wa programu za UKIMWI.
3. Kutoa miongozo na kuratibu masuala ya habari, utetezi na mawasiliano kuhusu UKIMWI ili kuchochea mabadiliko ya tabia katika jamii na makundi maalum.
4. Kuongoza pamoja na kuimarisha mazingira mazuri ya kazi na wafanyakazi wa Tume kwa
Hotuba ya bajeti ya Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais 2013/14
44
ajili ya kuleta ufanisi katika shughuli za uratibu wa masuala ya UKIMWI.
120. Mheshimiwa Spika, ili Tume ya UKIMWI iweze kutekeleza malengo iliyojipangia kwa mwaka wa fedha 2013/2014, naliomba Baraza lako Tukufu liidhinishe jumla ya TZS 768,000,000 kwa kazi za kawaida, kati ya hizo TZS 510,714,700 kwa ajili ya kuendeshea kazi na TZS 257,285,300 kwa ajili ya mishahara. Aidha, naliomba Baraza lako Tukufu liidhinishe jumla ya TZS 50,000,000 kwa kazi za maendeleo kutokana na mchango wa Serikali na TZS 1,719,000,000 kutoka kwa wahisani (rejea kiambatanisho namba 10).
SHUKURANI
121. Mheshimiwa Spika, naomba niwashukuru kwa dhati kabisa Waheshimiwa Wajumbe wa Baraza lako tukufu kwa kuwa wasikivu na wastahamilivu wakati wote nilipokuwa nikiwasilisha hotuba yangu. Ni matumaini yangu kwamba Waheshimiwa Wajumbe wataendelea kushirikiana na ofisi yetu katika kutoa michango mbali mbali ambayo itaiwezesha kutatua matatizo yanayoikabili jamii. Ofisi yetu itaipokea na kuifanyia kazi michango yote itakayotolewa na Wajumbe wa Baraza hili kwa maslahi ya Jamii na Taifa kwa ujumla.
122. Mheshimiwa Spika, napenda kutoa shukrani zangu za kwa nchi marafiki, mashirika ya Kimataifa na watu binafsi kwa kuendelea kutusaidia kuendeleza shughuli za Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais. Nchi hizo ni pamoja na Marekani, Finland, Norway, Uingereza, Uholanzi, China, India, Qatar, Oman na Falme za nchi za
Hotuba ya bajeti ya Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais 2013/14
45
Kiarabu. Pia mashirika ya kimataifa yakiwemo UNDP, UNICEF, UNFPA, UNAIDS, UNEP, UNODC, UNFCCC, WHO, World Bank, Taasisi ya Maendeleo ya Kimataifa ya Serikali ya Uingereza (DFID), AIHA, CDC, ICAP, Save the Children na nchi na mashirika mengine ambayo sikuyataja, lakini kwa njia moja au nyengine yanatuunga mkono katika shughuli zetu za maendeleo. Michango yao tunaijali na kuithamini.
123. Mheshimiwa Spika, natoa shukurani za dhati kwa Taasisi mbali mbali za Serikali zikiwemo vyombo vya ulinzi na usalama na taasisi zisizo za kiserikali zinazojishughulisha na masuala ya UKIMWI, mapambano dhidi ya dawa za kulevya, utunzaji na uhifadhi wa mazingira na kutetea haki na fursa za watu wenye ulemavu. Nawaomba waendelee kutupa mashirikiano kwa lengo la kuwatumikia wananchi wa Zanzibar na kufikia lengo kuu la kukuza uchumi na kupunguza umasikini. Aidha, napenda kuvishukuru sana vyombo vyote vya habari kwa kushirikiana nasi katika kuielimisha jamii juu ya athari za uharibifu wa mazingira, matumizi ya dawa za kulevya, namna ya kujikinga na VVU na UKIMWI na umuhimu wa kuwahudumia watu wenye ulemavu.
124. Mheshimiwa Spika, napenda kutoa shukurani za pekee kwa watendaji wote wa Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais kwa ushirikiano na ushauri uliowezesha kutekelezwa kwa majukumu ya Ofisi kwa mwaka 2012/2013 kama yalivyobainishwa katika hotuba hii. Napenda kumshukuru Makamu wa Kwanza wa Rais Mheshimiwa Maalim Seif Sharif Hamad, akiwa ndio kiongozi wa ofisi yetu, kwa maelekezo yake kwangu na
Hotuba ya bajeti ya Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais 2013/14
46
kwa watendaji na kuifanya ofisi yetu iweze kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi mkubwa. Pia napenda kuwashukuru sana Katibu Mkuu, Dk. Omar Dadi Shajak, Naibu Katibu Mkuu, Dk. Islam Seif Salum, Afisa Mdhamini, Fatma Mohammed Omar, Wakurugenzi Watendaji na Wakurugenzi wa Idara na Taasisi zilizo chini ya Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais pamoja na Watendaji wote kwa ushirikiano na kazi kubwa walioifanya katika kuandaa mpango na bajeti hii kwa wakati.
125. Mheshimiwa Spika, Mwisho napenda kuwashukuru wananchi wote kwa kufanikisha kazi za maendeleo ya nchi yetu. Napenda kutoa wito kwa wananchi wote na waheshimiwa Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi kuhakikisha kuwa azma ya Serikali ya kulinda mazingira na kujikinga na athari za mabadiliko ya tabianchi, kutetea na kulinda haki za watu wenye ulemavu, kudhibiti matumizi ya dawa za kulevya na kujikinga na maambukizi mapya ya UKIMWI inazingatiwa na inaendelea kupewa kipaumbele kwa manufaa ya Taifa letu na kizazi kijacho.
HITIMISHO
126. Mheshimiwa Spika, kwa heshima nachukuwa nafasi hii kuwaomba Wajumbe wa Baraza lako Tukufu waipokee, waijadili, watushauri, watuelekeze na hatimae kuidhinisha matumizi ya Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais ya jumla ya shilingi Bilioni tatu na milioni ishirini (TZS 3,020,000,000) kwa mwaka wa fedha 2013/2014. Kati ya fedha hizo, TZS Bilioni moja milioni mianane ishirini na moja (TZS 1,821,000,000) kwa
Hotuba ya bajeti ya Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais 2013/14
47
ajili kuendeshea kazi na shilingi Bilioni moja milioni miamoja tisini na tisa (TZS 1,199,000,000) kwa ajili ya mishahara. Aidha naliomba Baraza lako Tukufu kuidhinisha jumla ya TZS Milioni miamoja na hamsini (TZS 150,000,000) kwa kazi za maendeleo ikiwa ni mchango wa Serikali na TZS Milioni mianane (TZS 800,000,000) ikiwa ni mchango wa wahisani (angalia kiambatanisho namba 11).
127. Mheshimiwa Spika, aidha, naliomba Baraza lako tukufu liidhinishie Tume ya UKIMWI matumizi ya jumla ya TZS Milioni miasaba sitini na nane (TZS 768,000,000) kwa kazi za kawaida, ambapo shilingi Milioni miatano na kumi lakisaba na kumi na nne na miasaba (TZS 510,714,700) kwa ajili ya kuendeshea kazi na TZSMilioni miambili hamsini na saba lakimbili na thamanini na tano na miatatu (TZS 257,285,300) kwa ajili ya mishahara. Aidha, naliomba Baraza lako tukufu kuidhinisha jumla ya shilingi Milioni hamsini (TZS 50,000,000) kwa kazi za maendeleo ikiwa ni mchango wa Serikali na TZS Bilioni moja milioni miasaba kumi na tisa (TZS 1,719,000,000) ikiwa ni mchango wa wahisani (rejea kiambatanisho Namba 11).
Aidha naliomba Baraza lako Tukufu likubali mchango wa jumla ya TZS 10,800,000 ikiwa ni mapato yaliokadiriwa kukusanya kwa mwaka wa fedha 2013/2014 na Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais.
Mheshimiwa Spika, naomba kutoa hoja. Hotuba ya bajeti ya Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais 2013/14
48
KIAMBATANISHO NAM. 1
TAARIFA YA WATUMISHI WALIOKO MASOMONI NO | JINA | CHUO ANACHOSOMA | MAFUNZO ANAYOCHUKUWA | DARAJA | |||
Ofisi ya Faragha | |||||||
1 | Mwanakharusi Kh Andrew | Chuo cha utumishi wa Umma | Katibu Muhtasi | Stashahada | |||
Idara ya Mipango, Sera na Utafiti | |||||||
2 | Nassor A Rashid | Chuo cha Juba-Sudani | Economics Science | Shahada ya pili | |||
Idara ya Uwendeshaji na Utumishi | |||||||
3 | Zena Mussa Mwinyi | Utumishi wa Umma | Kutunza kumbukumbu | Stashahada | |||
4 | Rukia Hemed Abdalla | Chuo cha Utumishi wa Umma | Katibu Muhtasi | Stashahada | |||
5 | Jokha Nassor Mvinja | Chuo cha Chanika | Ununuzi na Ugavi | Shahada ya kwanza | |||
6 | Khadija Juma Khamis | IFM | Uhasibu | Shahada ya Pili | |||
Idara ya Mazingira | |||||||
7 | Msichoke Khairalla Tawakal | Chuo cha Utumishi wa Umma | Rasilimali watu | Cheti | |||
8 | Dawa Mussa Ame | Chuo cha Utumishi wa Umma | Ukutubi | Cheti | |||
9 | Tatu Suraka Juma | Chuo cha Utumishi wa Umma | Rasilima Watu | Cheti | |||
10 | Shari Ali Ahmed | Chuo cha Kuendeleza na Mafunzo maalumu. | Katibu Muhtasi | Stashahada | |||
1 | Rehema | Chuo cha Utumishi | Rasilimali |
No comments:
Post a Comment