Habari za Punde

Benki ya Watu wa Zanzibar Yatimiza Miaka 47

.
     Benki ya Watu wa Zanzibar Limited Inasherehekea Miaka 47 tokea kuanzishwa kwake  Zanzibar
   tarehe 30-6-1966.

Bodi ya Wakurugenzi ,Uongozi na Wafanyakazi wake wote wanapenda kuchukua fursa hii kuwapongeza wateja wake wote na Wananchi kwa Ujumla waliochangia maendeleo ya PBZ kwa njia moja ama nyengine hadi leo hii kutimiza miaka 47.

           Endelea kutumia Benki ya Watu wa Zanzibar Limited kwa huduma zake imara na bora.

                                 Benki ya Watu, Chaguo la Watu

                 Miaka 47 ya PBZ Oyeeeeeeeee!!!!!!! 

1 comment:

  1. Miaka 47 ya kuanzishwa kwake, hailingani kabisa na mafanikio yaliyopatiakana!

    Ndani ya 47, ukiangalia makao makuu ya PBZ pale darajani huwezi kuamini.. ni bora hata makao makuu ya kampuni ya BOMBAY BAZAAR pale mlandege.

    PBZ ilianzishwa ktk zama ambazo hazikua na ushindani wowote wa Kibiashara na walikua huru kuendesha biashara popote ndani ya Tza.

    Ndani ya miaka 47, ni miaka 3 iliyopita ndio wamefanikiwa kuanzisha matawi yake mawili, pale Kariakoo Dsm.

    PBZ haina tofauti kubwa na mashirika mengine ya z'bar kama vile ZIC, TVZ.

    Mashirika haya kama yangesimamiwa na kutumia fursa vizuri, naamini leo hii wangekua ni Watanganyika wanaolalamikia mfumo wa muungano na sio sisi!

    Shirika linaloshindwa kuwekeza vizuri ndani ya nchi yake hivi kweli litaweza kuwekeza nje?

    Mabenki kama vile CRDB yaliyoanzisha miaka michache tu iliyopita leo hii wana matawi KENYA KONGO na RWANDA!

    Naamini tusipojipanga tutaishia kulalamika tu, na EAC..nayo hiyooo.. inakuja kutuononea!

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.