Pia, Mheshimiwa Majaliwa atashiriki katika kongamano la biashara, uwekezaji na utalii ambalo litahusisha wafanyabiashara kutoka Tanzania na Japan.Vilevile Waziri Mkuu atashiriki katika Mikutano ya Uwili yenye lengo la kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na Japan.
Maonesho hayo yalianza tangu Aprili 13, 2025 na yanatarajia kumalizika Oktoba 13, 2025, hii ni mara ya pili kwa Japan (Osaka) kuwa mwenyeji wa maonesho haya ya kimataifa, ambapo mara ya mwisho yalifanyika 1970 (EXPO 1970).
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Mkewe Mary Majaliwa (kulia) wakisalimiana na Balozi wa Tanzania nchini Japan, Mheshimiwa Baraka Luvanda walipowasili kwenye uwanja wa Ndege wa Kansai ulipo Osaka nchini Japan ambako atamwakilisha Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwenye Maonesho ya World Expo 2025 Osaka.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Mkewe Mary Majaliwa (kulia) wakizungumza na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki, Cosato Chumi walipowasili kwenye uwanja wa Ndege wa Kansai ulipo Osaka nchini Japani ambako Waziri Mkuu atamwakilisha Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hssan kwenye Maonesho ya World Expo 2025 Osaka. Kulia ni Mke wa Waziri Mkuu, Mary Majaliwa.
No comments:
Post a Comment