Habari za Punde

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Alhajj Hemed Suleiman Andulla Ajumuika na Waumini katika Sala ya Ijumaa Masjid Shaafiy

MAKAMU wa Pili wa Rais wa Zanzibar Alhajj Hemed Suleiman Abdulla  amewataka waumini wa dini ya kiislamu  kwa kila mwenye uwezo kwenda  kutekeleza ibada tukufu ya Hijja Nchini Makka Saudia Rabia.

Ameyasema hayo wakati akisalimiana na waumini wa Masjid Shaafiy uliopo Mbuyu Mnene Wilaya ya magharib B Unguja mara baada ya kumaliza Ibada ya Swala Ijumaa .

Alhajj Hemed amesema ni vyema waumini wa dini ya kiislam wakatambua umuhimu wa kufanya ibada ya hijja wakiwa na nguvu na kuachana na tabia ya kusubiri kufanya ibada hio ikiwa umri umeashakuwa mkubwa  wakitambua kuwa hakuna anaejua kesho yake na uhai ndhamana ya Allah.

Aidha, Mhe. Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar amewataka wazazi na walezi kuendelea kuwalea watoto wao kwenye malezi bora yanayofuata maadili na miongozo ya dini sambamba na kufuatilia myenendo yao kila siku.

Amewasisistiza vijana kutumia fursa ya kusoma na kujiendeleza kielimu na kuancha kujiingiza kwenye makundi ya uhalifu yanayo vunja sheria.

Alhajj Hemed  amewataka wananchi kuendelea kuitunza Amani iliyopo nchini hasa katika kipindi hiki cha kuelekea Uchaguzi Mkuu unatarajiwa kufanyika October 2025 na kutokukubali  kushawishiwa na kutumika katika vitendo vya uvunjifu wa Amani na badala yake wawe mstari wa mbele katika  kuilinda na kuitunza Amani na Utulivu uliopo nchini.

Akitoa Khutba ya swala ya Ijumaa Katibu Mtendaji Ofisi ya Mufti Mkuu Zanzibar Sheikh Khalid Ali Mfaume amewaomba wazazi na walezi kuwalea watoto wao katika malezi yenye kumtambua Allah  (S.w) yatakayopelelekea kuijua dini yao na kufanya matendo mema.

Sheikh Khalid  amesema watoto waliopata malezi bora huweza kujitambua mapema na kujiepusha na makundi maovu yanayochangia uvunjifu wa maadili kupelekea Taifa kukosa nguvu kazi Imara.

Imetolewa na Kitengo cha Habari (OMPR)
Tarehe 23.05.2025

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.