Habari za Punde

Wizara ya Afya Zanzibar Kuimarisha huduma za uzazi wa Mpangilio katika Maeneo mbali mbali ya Afya

Na.Omar Abdallah. 

WIZARA ya Afya Zanzibar imesema itaendelea kuimarisha huduma za uzazi wa Mpangilio katika maeneo mbali mbali ya Afya kwa lengo la kupunguza vifo vitokananvyo na uzazi.

Mkurugenzi Mipango Sera na Utafiti wa Wizara ya Afya Zanzibar Abdullatifu Khatib Haji ameyaeleza hayo wakati alipofungua mkutano wa wadau unaohusiana na uzazi wa mpango uliofanyika Wizara ya afya Vuga.

Amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia Wizara ya Afya inaendelea kufanya jitihada mbali mbali kuona kuwa afya ya mama na mtoto inaimarika kwa kuchukua hatua mbali mbali   ikiwa na pamoja na kuhamasisha matumizi ya uzazi wa mpangilio.

Amefahamisha kuwa imefika wakati kwa sasa masuala ya huduma za afya ya mama na mtoto pamoja uzazi wa mpangilio yaimarishwe zaidi katika maeneo ya utoaji wa huduma hasa katika vituo vya Afya vya Unguja na Pemba.

Amesema katika kuimarisha huduma za uzazi wa mpangilio hapa nchini ni vyema kuwe na mikakati madhubiti itakayofanikisha huduma hii kupanda na kupunguza matatizo mbali mbali yanayotokana na uzazi.

Kwa upande wake Mratibu wa huduma za uzazi wa mpangilio Kitengo cha Afya mama na mtoto Radhia Mataka amesema kwa Zanzibar takwimu zinaonesha kuwa miaka ya 1999 njia za uzazi wa mpango zilikuwa zikiongozeka na hadi mwaka 2022 idadi ya matumizi ya njia za uzazo wa mpango ilipungua kwa mujibu wa utafiti uliofanyika.

Amesema jitihada mbali mbali zinafanyika katika kuhakikisha huduma ya uzazi wa mpangilio inaongezeka katika wilaya zote za Unguja na Pemba kwa kushirikina na wadau, kutoa elimu sambamba na kufanya huduma katika maeneo mbali mbai ikiwa na lengo kuwafikia walengwa.

mwisho

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.