Na Jumbe Ismailly, Iramba
MAHAKAMA ya Wilaya ya Iramba mkoani Singida imemhukumu mwanamke mmoja,Sayuni Ramadhani (42) mkazi wa kijiji cha Kisana wilayani hapa kifungo cha miaka mitatu jela baada ya kukiri kumng’ata mumewe sehemu za siri na kumbakisha ngozi nyemba.
Kabla ya kutolewa kwa hukumu hiyo,Mwendesha Mashitaka,Mkaguzi wa polisi, Vicent Ndasa aliomba mahakama hiyo itoe adhabu kali kwa mshitakiwa huyo ili iwe fundisho kwake na kwa wanawake wengine wanaotarajia kufanya kosa kama lililofanywa na mshitakiwa huyo.
Naye mshitakiwa kwa upande wake aliiomba mahakama hiyo imwonee huruma kwa kumpa adhabu nafuu kwa vile hilo ni kosa lake la kwanza na pia anakabiliwa na jukumu la kubwa la kulea watoto wake.
Akitoa hukumu hiyo,Hakimu Mfawidhi wa mahakama hiyo, Mrisho Mrisho alisema baada ya kuzingatia maombi ya pande zote mbili, mahakama imemtia hatiani mshitakiwa na kumhukumu kwenda je;a miaka mitatu.
Awali Mwendesha mashitakaalidai kwamba Juni 4mwaka huu saa 12 jioni katika kijiji cha Kisana,wilayani hapa mshitakiwa kwa makusudi alimng’ata mumewe Onesmo Nathania(42) uume wake na kuubakisha ngozi nyembamba.
Aalidai kitendo hicho kilimsababishia maumivu makali mlalamikaji na hivyo kupelekea kukimbizwa hospitali kwa matibabu.
Alidai siku ya tukio wanandoa hao wakitokea kwenye kilabu cha pombe za kienyeji katika kijiji cha Kisana, walipofika nyumbani kwao walianza kugombana na kupigana na ndipo mshitakiwa alipochukua uamuzi wa kumng’ata uume mu
No comments:
Post a Comment