Habari za Punde

Mfanyakazi wa ndani achinjwa, mwili wake watupwa



Mwili wa Pepetua baada ya kutolewa shimoni.
 
Na Fatuma Kitima,DSM

MFANYAKAZI wa ndani raia wa Kenya aliyetambulika kwa jina la Perpetua Maina (30) amekutwa amekufa katika eneo la Mikocheni B jijini Dar es Salaam.

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Kamishna wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam , Suleiman Kova alisema tukio hilo lilitokea Juni 9 mwaka huu karibu na dampo la kutupia taka katika eneo la Mikocheni B, karibu na eneo linalomilikiwa na wakala wa majengo Tanzania (TBA).

Kamanda Kova alisema marehemu alikutwa amekufa akiwa amechinjwa sehemu ya shingo,jeraha sehemu ya mkono wa kushoto,jereha sehemu ya usoni huku mwili wake ukiwa umetapakaa damu sehemu za kichwani.

Jeshi la Polisi linamshikilia Philemon Laiza (27) mtunza bustani katika nyumba ya Jaji Kileo ambae anatuhumiwa kuhusika katika tukio hilo.

Alisema mtuhumiwa huyo aliekuwa akifanya kazi pamoja na marehemu alikiri kuwa marehemu siku ya Ijumaa saa usiku 2:00 alitoweka nyumbani na kuonekana akiwa amekufa.

Mtuhumiwa bado anahojiwa na upelelezi ukikamilika atafishwa mahamani.

Katika tukio lingine watuhumiwa wawili wanaosadikiwa kuwa ni majambazi hatari wanaojihusisha na uporoji wa mali za raia wa kigeni ufukweni mwa bahari mjini humo wamekamatwa.

Aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni Isaya Mafuru (31),Jusuph Juma (33) ambao ni mafundi ujenzi wakazi wa Msasani na baada ya upelezi waliwezesha kukamata watuhumiwa wengine sita.

Alisema watuhumiwa aho walikiri kuhusika na matukio mbalimbali ya uhalifu katika maeneo hayo ikiwemo kumpora raia wa kigeni.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.