Joseph Ngilisho, Arusha
WATU wawili wamefariki dunia na wengine kujeruhiwa baada gari walilokuwa wakisafiria kupasuka gurudumu na kupinduka likiwa kwenye mwendo wa kasi.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake, Kamanda wa polisi mkoani hapa, Liberatus Sabas alisema tukio hilo limetokea Juni 9 mwaka huu majira ya sa 11 jioni katika barabara ya Arusha – Dodoma katika eneo la Makuyuni wilayani Monduli mkoani Arusha.
Alisema tukio hilo limelihusisha gari aina ya hiace lenye namba za usajili T 352 PJW Toyota Hiace, lililokuwa na abiria ambapo likiwa kwenye mwendo kasi ghalfa lilipasuka gurudumu la mbele na kupinduka.
Kamanda Sabas aliwataja waliokufa katika ajali hiyo kuwa ni Veronica Martin (30) na mtoto wa aliyetambulika kwa jina la Dorcas Peter (8) wote wakazi wa Manyara.
Alisema chanzo cha ajali hiyo ni kuwa dereva hiyo alikuwa kwenye mwendo kasi hali iliyosababisha ajali hiyo na baada ya ajali hiyo derera wa gari hilo alikimbia na kulitelekeza gari katika eneo la ajali.
Aidha miili ya marehemu hao imehifadhiwa katika hospitali ya mkoa ya Mount Meru huku majeruhi wengine wakiendelea kupatiwa matibabu.
Kamanda Sabas aliwataka madereva kuwa waangalifu pindi wanapokuwa barabarani kwa ajili ya kuokoa roho za watu kwani uendeshaji mbovu umekuwa ukichangia kuwepo kwa ajali za mara kwa mara.
No comments:
Post a Comment