Na Mwajuma Juma
NUSU fainali ya kwanza ya michuano ya Kombe la Mazingira inatarajiwa kuchezwa leo katika uwanja wa Mao Dze Tung mjini hapa.
Mchezo huo utakaoanza saa 10:00 za jioni utazikutanisha timu za Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais na timu ya Idara ya Uvuvi na Maendeleo ya Mazao ya Baharini Zanzibar.
Ili kutinga hatua hiyo, OMPR iliichapa KMKM Veteran mabao 2-1, na Uvuvi ikaifunga Shirika la Umeme Zanzibar (ZECO) mabao 3-2.
Ratiba ya mashindano hayo inaonesha nusu fainali ya pili itachezwa kesho kati ya timu ya Hits Fm na Habari SC.
Wanahabari wa Hits FM waliifunga Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais bao 1-0 na Habari SC ikaiondoa Mamlaka ya Maji Zanzibar (ZAWA) kwa kipigo cha mabao 2-0.
Katika michuano hiyo iliyoshirikisha timu nane, bingwa atazawadiwa shilingi laki tatu, na kikombe, huku mshindi wa pili atapata shilingi laki mbili na mipira miwili.
WAKATI huo huo, ligi ya mpira wa kikapu kanda ya Unguja, iliendlea juzi kwa maafande wa Polisi kuwaendesha puta African Magic kwa kuwafunga vikapu 55-48 kwenye uwanja wa Maisara.
No comments:
Post a Comment