Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein, akihutubia wakati wa Uzinduzi wa Tamasha la Urithi wa Utamaduni wa Mwangapwani, kulia Rais Mstaaf wa Tanzania Mhe. Ali Hassan Mwinyi na kushoto Mratibu wa Tamasha hilo Mwinyi Jamali.
Rais Mstafuu wa Tanzania Mhe. Ali Hassan Mwinyi mlezi wa Tamasha hilo akihutubia katika uzinduzi wa tamasha hilo, katika viwanja vya Mwangapwani.
Rais wa Zaanzibar Dk Ali Mohd Shein katikati akiangalia mchezo wa Bao la kete baada ya kuwasili katika Ufunguzi wa Tamasha la Urithi wa kiutamaduni wa watu wa Mangapwani Mkoa wa Kaskazini Wilaya ya Kaskazini "B"Unguja.kulia yake ni Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ali Hassan Mwinyi na kushoto yake ni Mwenyekiti wa Tamasha hilo Mwinyi Jamal Ramadhan.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein, akiangalia ngoma ya Utamaduni inayocheza na Watoto katika sherehe hiyo ya uzinduzi wa Tamasha hilo katika Kijiji cha Mwangapwani Unguja.
Rais wa Zanzibar Dk Ali Mohd Shein wa kwanza kulia akikaribishwa kwa ngoma ya Ndege mara alipowasili katika Ufunguzi wa Tamasha la Urithi la kiutamaduni wa watu wa Mangapwani Mkoa wa Kaskazini Wilaya ya Kaskazini "B"Unguja.
Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ali Hassan Mwinyi akiangalia Sabuni iliotengenezwa kwa Mwani katika Ufunguzi wa Tamasha la Urithi wa kiutamaduni wa watu wa Mangapwani Mkoa wa Kaskazini Wilaya ya Kaskazini "B"Unguja.
Asante kwa hizi picha. Mambo kama haya ya kitamaduni ambayo ni mazuri tutaweza kuyaenzi na kuyatunza zaidi kama tutajitegemea kama nchi na kutoruhusu wageni kuja kutuchafulia mila na silka zetu.
ReplyDeleteBwana Othman shukra zaidi zikushukie juu yako kwa kutuelewesha matokeo yanayotokea lakini pia ningependa kuweka lugha sawa kidogo kama sitokuwa mie ndie mkoseaji hapo ulipoandika Ngoma ya Ndege nafikiri kwa kumbukumbu zangu mie nikiwa mtoto mdogo katika miaka ya mwanzoni mwa 70 Bibi yangu (BiKiyate) Mungu amrahamu alikuwa ni mmoja kati ya wachezaji ya hiyo Ngoma na kwa jina kamili Huitwa MwanaNdege na sio Ngoma ya ndege inawezekana ikawa kumbukumbu zangu ndio mie niliyekoseya na kama ndiyo hivyo nitaomba msamaha (Tunahitaji kuwa na jitihada za kuwazuwiya ndugu zetu wasije kuingia katika mkumbo wa (kuongea swahili)badala ya kuzungumza kiswahili
ReplyDeleteAnonymous 2.
ReplyDeleteNisawa kabisa ulivosema hiyo sio ngoma ya Ndege bali ni Ngoma ya Mwanandege.. Na utamaduni kama huu unataka uendelezwe na uenziwe kaisa kwani ndio utakao wafhamisha Wazanzibari wa Leo (Vijana) nini maana yakua Mzanzibari na sio Mtanzania Visiwani.
Aslimia kubwa ya wazanzibari ni waislamu,tukiachilia utamaduni,mila,dasturi na kadhalika kipi cha kufatwa dini au hivyo vyengine.Sioni sababu ya kudumisha utamaduni wa ngoma ilhali si katika mafundisho ya dini yetu ikiwa hapana budi bask akina mama wafanye sherehe zao peke yao wafurahi na utamaduni wao kisheria lakini sio mijibaba imekaa ikikodolea macho.Tukumbuke hao ni mama zetu au dada zetu be kadhalika tunakubali kuwavua nguo huku tukifurahia INNA LILLAHI WA INNA ILYHI RAAJIUUN
ReplyDelete