Rais wa Serekali ya Mapinduzi Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi, Spika wa Baraza la Wawakilishi Pandu Ameir Kificho, ni miongoni mwa Viongozi waliofika kumpokea Rais wa Marekani Barack Obama, alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere Tanzania.
Ndege iliomchukuwa Rais Obama ikiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere
Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete na Balozi wa Marekani Nchini Tanzania Balozi Alfonso, wakiende kumpokea Mgeni wao Rais wa Marekani Barack Obama akiwasili katika Uwanja wa Mwalim Nyerere kwa ziara ya Siku mbili kutembelea Tanzania akitokea Nchini Afrika ya Kusini.
Rais wa Marekani akiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalim Nyerere kwa ziara ya siku mbili, akiongozana na Mkewe na Watoto wake wakishuka katika ndege yake.
Rais Obama akiteta na Mwenyeji wake Rais Kikwete alipowasili Tanzania akiwa katika ziara ya siku mbili Tanzania.
Rais Obama akiwa na Mwenyeji wake Rais wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete wakielekea katika jukwaa maalum aliloandaliwa kwa ajili ya kupingwa wimbo wa Mataifa haya mawili
Rais wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete akifurahia jambo na Rais wa Marekani Barack Obama. wakiwa katika uwanja wa ndege.
Rais Obama akiwapungia mkono wananchi waliofika uwanja wa ndege kumlaki alipowasili kwa ajili ya ziara ya siku mbili Tanzania.
Rais Obama akikaguwa Bwaride lililoandaliwa kwa ajili yake wakati wa mapokezi yake Tanzania.
Waandishi wa Habari wa Vyombo mbalimbali Duniani wakiwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalim Nyerere wakiwa katika harakati zakupata picha kwa ajili ya Vyombo vyao kuhabarisha Wananchi kujionea mambo ya ziara ya Rais Obama Tanzania.
Rais wa Marekani Barack Obama akiendele kukagua Bwaride rasmin aliloandaliwa wakati wa mapokezi yake Tanzania.
Rais wa Marekani Barack Obama akiongozani na Mkuu wa Majeshi Tanzania Davis Mamunyange, baada ya kukagua bwaride aliloandaliwa kwa ajili yake katika mapokezi hayo mjini Dar-es- Salaam, akiwa katika ziara ya siku mbili Tanzania.
Wananchi wakiwa katika harakati za kupata picha ya kumbukumbu ya Rais Obama wakiwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wakati wa mapokezi ya Rais Obama
Rais Kikwete akiwa na Mgeni wake Rais wa Marekani Barack Obama wakiangalia ngoma ya Utamaduni zilioandaliwa kwa ajili yake katika mapokezi hayo.
Rais Obama akiangalia moja ya Ngoma za Utamaduni alipowasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalim Nyerere Tanzania kwa ziara ya siku mbili Tanzania
Watanzania wakipunga Bendere za Tanzania na Marekani ikiwa ni shamrashamra za kumpokea Rais Obama alipowasili uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mawalim Nyerere Tanzania.
Wananchi wakiwa katika maeneo ya Vingunguti ikiwa ni mapokezi ya Rais wa Marekani Barack Obama.
Wananchi wa Tanzania Wakiwa katika makutano ya Barabara ya Mandela na Nyerere maeneo ya Buguruni wakisubiri kumpokea Rais Obama.
Vijana wakiwa na bango kama wakiwa katika mitaa ya Buguruni wakimpokea Rais wa Marekani Barack Obama alipowasili Mjini Dar kwa ziara ya siku mbili.
No comments:
Post a Comment