Na Hafsa Golo
PAMOJA na Serikali kuwataka wafanyabiashara wasipandishe bei za bidhaa hasa katika mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani,lakini hali imekuwa tafauti siku moja tu Waislamu kuanza kutekeleza ibada hiyo.Uchunguzi uliofanywa na mwandishi wa habari hizi katika masoko ya Mwanakwerekwe, Darajani na Mombasa umebaini bidhaa za futari zimepanda ghafla.
Kipolo kimoja cha majimbi kimeuzwa kwa shilingi 90,000 wakati kabla ya mfungo wa Ramadhan kipolo kama hicho kiliuzwa shilingi 35,000-40,000 huku pakacha ya viazi vikuu imepanda kutoka shilingi 15,000 kabla ya Ramadhan hadi shilingi 35,000 sasa.
Aidha mkungu wa ndizi mbivu ya mkono wa tembo imeuzwa kwa shilingi 50,000 -60,000 huku mbichi ikiuzwa kwa shilingi 20,000-25,000 ambapo awali iliuzwa shilingi 17,000 -15,000.
Aidha viazi mbatata bado vimesalia katika bei ya awali, lakini inatarajiwa kupanda kadiri siku zinaposonga mbele.
Kwa bei ya reja reja ndizi mbivu ya mkono tembo dole moja liliuzwa shilingi 3000 hadi 2500, mzuzu dole moja limeuzwa kwa shilingi 700 huku chana moja ya mtwike ikiuzwa kwa shilingi 3000 hadi 2500.
Kwa upande wa nazi, imeuzwa kuanzisha shilingi 300 hadi 650 badala ya shilingi 200 na 150 kabla ya Ramadhan.
Wananchi waliofika katika masoko hayo kununua futari, walielezea kusikitishwa na kupanda ghafla bei za bidhaa na kuomba serikali iingilie kati haraka.
Mmoja ya wananchi hao aliejitambulisha kwa jina la Mwatima Ramadhan aliwataka wafanyabiashara kuzingatia utukufu wa mwezi huu kwa kuwaonea huruma wafungaji badala ya kufikia faida tu.
Mfanyabiashara wa soko la Mwanakwerekwe, Said Suleiman alisema bei ya bidhaa inatarajiwa kupanda zaidi.
Nae Mkuu wa soko la Mombasa, Mohammed Saidi Arafa alisema kama hali itaendelea kuwa hivyo, inaweza kuwaumiza wafungaji na familia zao.
Hizibiashara hapa unguja zina fanya na wagenihawana uchungu waladini, waofitina kwanda mbele na kufugande na kuhamanishana kufanya fujo;miskitini, mbona pemba vitu havipandi bei kama unguja wachuuzi kutoka pemba wana wakomoawenyeji wao, hawajali ukarim wa watu wa unguja
ReplyDelete