Kutoka
kwa Ummul Muuminiyna ‘Aaishah, Allaah amuwie radhi amesema:
( كَانَ
يَعْتَكِفُ الْعَشْرَ الأَوَاخِرَ مِنْ رَمَضَانَ حَتَّى تَوَفَّاهُ اللَّهُ ،
ثُمَّ اعْتَكَفَ أَزْوَاجُهُ مِنْ بَعْدِهِ )
ومسلم رواه البخاري
Mtume Swalla Allaahu ‘alayhi
wasallam alikuwa akifanya i’itikaaf katika kumi la mwisho la Ramadhaan hadi
mauti yalipomfika. Kisha wake zake waliendelea kufanya i’itikaaf baada yake
Imepokewa
na Bukhaari na Muslim
I’itikaaf
ni mojawapo ya ibada muhimu ambapo muislamu hujitenga na dunia na kujifunga na
msikiti kwa ajili ya kumuabudu Allaah Subhaanahu Wata’ala pekee.
Hukumu
yake ni Sunna ila Sunna hii ni mojawapo katika Sunna ambazo zipo hatarini
kutoweka endapo waislamu ambao ni mimi na wewe hatutakuwa tayari kuihuisha
ibada hii muhimu ambayo Mtume wetu na ruwaza yetu alikuwa akiitekeleza kila
Ramadhaan na wala hakuiacha mpaka wakati wake wa kuondoka duniani ulipowadia.
Kuna
hadithi nyingi zinazozungumzia fadhila za I’itikaaf lakini Maulamaa wa hadithi
wanasema nyingi ni dhaifu hivyo kabla ya kuitumia hadithi yoyote yenye fadhila
za I’itikaaf hakikisha hukumu ya hadithi yenyewe kwanza.
No comments:
Post a Comment