Amesema Mtume Swalla
Allaahu ‘Alayhi wasallam
: الصِّيَامُ وَالْقُرْآنُ يَشْفَعَانِ لِلْعَبْدِ
يَوْمَ الْقِيَامَةِ، يَقُولُ الصِّيَامُ: أَيْ رَبِّ مَنَعْتُهُ الطَّعَامَ
وَالشَّهَوَاتِ بِالنَّهَارِ، فَشَفِّعْنِي فِيهِ. وَيَقُولُ الْقُرْآنُ:
مَنَعْتُهُ النَّوْمَ بِاللَّيْلِ فَشَفِّعْنِي فِيهِ. قَالَ: فَيُشَفَّعَانِ».
Funga
na Qur’aan zitamwombea mja siku ya kiama. Funga itasema (siku hiyo), Ewe mola nilimzuia kula na matamanio muda
wote wa mchana ( wa funga) hivyo Ninamuombea shufaa yako. Na Qur’aan (siku
hiyo) itasema; nilimkosesha usingizi wakati wa usiku (kwa sababu ya kunisoma wakati
wa ibada) hivyo ninamuombea shufaa yako. Na maombi ya shufaa yatatakabaliwa .
Imepokewa
na Ahmad
Ewe
Mola tujaalie kuifunga funga uliyoitambulisha kwetu kwamba ni yako ili iwe ndio mkombozi wetu wa kutuokoa na
adhabu zako siku ya kiama.
Ewe
Mola tujaalie kuisoma Qur’aan tutakayojaaliwa kuisoma katika mwezi huu adhimu
iwe ndio mkombozi wetu wa kutuokoa na adhabu zako siku ya kiama.
Aamiyn
Aamiyn
naam ni kweli lakini sio kwa wale wanaofuturu kwa riziki zilizopatikana kwa fedha za haramu , na
ReplyDeletewengi ni namna hio , huchukua pesa za rushwa , au wakipanga bajeti za kununua vitu vya serikali au mashirika , basi hutia kamisheni zao humo , hizo zote ni pesa za haramu ,hazifai kununua chakula na kufuturia kwenye funga