Habari za Punde

HARUSI TRADE FAIR SASA YAFIKISHA MIAKA MINNE


                                   HARUSI TRADE FAIR SASA YAFIKISHA MIAKA MINNE


                                                              Biashara Na Maonesho ya Harusi

                                                Watu wengi zaidi wahamasishwa kushiriki na kutembelea

Maandalizi ya Harusi Fashion Show 2013 yapamba moto, Maonesho hayo ya mavazi na wafanyabiashara wa bidhaa na huduma za harusi yanatarajiwa kufanyika tarehe 6 mwezi wa saba katika hoteli ya Hyatt Kilimanjaro, Dar es salaam. Muanzilishi na muandaaji wa Harusi Fashion Show Mustafa Hassanali amesema ikiwa ni mwaka wake wanne maonesho haya yamekuwa na kuongezeka ubora ukilinganisha na miaka iliyopita halikadhalika tunatarajia kuona mabadiliko kwenye tasnia ya Harusi na washikadau wake.

Mwaka huu Harusi Fashion Show tayari imeshawavuta washiriki wengi, wengi wao ni washiriki ambao wapo toka kuanzishwa kwa maonesho haya mwaka 2010.

Maonesho haya yanatarajiwa kufanyika kuanzia saa moja kamili joini na kuendelea.
“Harusi ni muunganiko wa familia na jamii na nikumbukumbu muhimu ya itakayodumu maisha yote, hivyo basi tumeamua kuwapa bibi na bwana harusi watarajiwa mahitaji yao yote ya siku hiyo muhimu kwenye hitoria ya maisha yao.” Amesema ndugu Esi Mgimba Afisa Habari na Mahusiano wa 361 degrees ambao ndio waandaaji wa onesho hilo.

Harusi Fashion Show inawaleta pamoja wadau wa biashara za harusi ili waweze kukutana kufahamiana na kuangalia fursa za kibiashara baina yao ili waweze kuzitumia kuboresha biashara zao na uhusiano wa kibiashara ambao utachangia kukuwa kwa tasnia hii.

Miongoni mwa washiriki amabao watakuwepo mwaka huu ni pamoja na keki, maua na wapambaji, wapiga picha, wabunifu wa mavazi ya harusi na wengineo wengi.

Na wafuatao ni washiriki wa Maonesho ya Harusi Mwaka huu,

The Wedding Kingdom, Sintah Bridal Lounge, E-cakes, Twaiba Classic, Manjou, An Nisaa Abayas, Mustafa Hassanali Bridals, Queen Jeweler, Mbezi Beach Hotel, Malaika Media, Harusi Nzuri, Julius Importers and Exporters Ltd, Rupam Stores, AVP, Shyland Photogenic, Gogo Shop, Liquid Lab, Brand House, The Cake Shop, Van Roy Production, Eve Collection na East West Photography.

“Kwakuwa idadi kubwa ya washiriki imethibitisha ushiriki wao, viingilio kwenye maonesho ya harusi ni 50,000 kwa viti maalumu na 20,000 kwa viti vya kawaida, na kutazama vipambio vya harusi ni bure, tunawaomba na kuwashauri watanzania wajitokeze kwa wingi kuja kuona na kuthamini ubunifu wa bidhaa za Kitanzania “ alimalizia ndugu Mgimba.

Maonyesho hayo ya biashara za Harusi yameletwa kwenu kwa hisani ya 361 degrees, Clouds Fm and Clouds Tv, Eventlites, Prime advitising, Century Cinemax na Baileys Cream with Spirit.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.