Habari za Punde

Mwenyekiti wa Tume ya Katiba Jaji Warioba kuzungumza na Waandishi wa Habari Dar.

Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba, atakutana na Wanahabari kesho, Ijumaa, Julai 5, 2013, kuanzia saa 4:00 asubuhi, katika Ukumbi wa Mikutano wa Tume uliopo katika Ofisi za Tume, Mtaa wa Ohio, jijini Dar es Salaam.

Katika mkutano huo, pamoja na mambo mengine, Jaji Warioba atazungumzia mikutano ya Mabaraza ya Katiba ya kujadili Rasimu ya Katiba itakayofanyika katika kila halmashauri ya wilaya. Mikutano hiyo itaanza hivi karibuni.

Nyote mnakaribishwa.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.