Habari za Punde

UNESCO Yakabidhi Vifaa Wizara ya Habari Vitendea Kazi.

Na Miza Othman –Maelezo Zanzibar Shirika la Kimataifa la Elimu Sayansi na Utamaduni UNESCO limeikabidhi vifaa Wizara ya Habari Utamaduni Utalii na Michezo Zanzibar vyenye thamani ya Shilingi Milioni 46 ili kuijengea uwezo Wizara hio.
 
Vifaa hivyo ni pamoja na Kamera mbili, Lenzi mbili, Digital Recorder 7, Vipaza sauti viwili, TV moja, pamoja na Mashine 2 za kutayarishia vipindi.

Akikabidhi vifaa hivyo Mkurugenzi wa UNESCO Tanzania Bi Vebeke Jense amesema lengo la kuletwa vifaa hivyo ni kuijengea uwezo Wizara hiyo ili kuleta mabadiliko hasa katika upande wa tasnia ya habari.

Baada ya Makabidhiano hayo Waziri wa Habari Utamaduni Utalii na Michezo Said Ali Mbarouk amelishukuru Shirika hilo kwa kuwa karibu na Wizara yake na kuahidi Vifaa hivyo vitatumika ipasavyo ili kutimiza lengo lililokusudiwa.

Waziri Mbarouk amesema iwapo Wafanyakazi watavituza Vifaa hivyo na kuvifanyia kazi ipasavyo hapana shaka mabadikliko katika wizara hiyo yataonekana hasa ikizingatiwa kuwa ni vifaa vya kisasa.

Amesema kwa muda Mrefu Idara ya Habari Maelezo imekuwa na upungufu wa Vifaa katika kukabiliana na majuku yake ya kila siku na kwamba upatikanaji wa Vifaa hivyo itakuwa ni suluhu ya tatizo hilo.

Kwa upende wake Mkurugenzi wa Tume ya Utangazaji Omar Chande amesema itakuwa ni jambo jema iwapo Vifaa hivyo pia vitatumika katika kuandaa habari za vijijini badala ya mijini pekee.

Aidha amefahamisha kuwa baadhi ya vifaa vinatarajiwa kufika siku za karibuni ili kuiwezesha Idara ya Habari Maelezo kuwa ya kisasa na kutimiza maelengo yake.

Msaada huo wa Vifaa vyenye thamani ya Milioni 46 umekuja kufuatia ahadi iliyotolewa na Shirika la UNESCO kwa Idara ya Habari kuiwezesha kupata Vifaa ambavyo vitasaidia katika kuendeleza majukumu yake ya kila siku.

IMETOLEWA NA HABARI MAELEZO ZANZIBAR 04/07/2013

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.