Na Miza Othman, Maelezo
Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imesema kwamba Jumla ya wanafunzi 161 wamewalipiwa ada ya Masomo na Posho mbali mbali kwa wale wanaoendelea na Masomo katika vyuo mbalimbali vya Nje kutokana na usumbufu wanaoupata chuoni.
Hayo yamesemwa huko Baraza la wakilishi Mbweni nje kidogo ya Mji wa Zanzibar na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Aamali Ali Juma Shamuhuna wakati alipokuwa akiwasilisha Bajeti ya Wizara yake Barazani hapo kuhusu makadirio ya Mapato na Matumizi ya Fedha kwa mwaka 2013/2014 mwaka ujao.
Amesema wanafunzi hao wamelipiwa fedha hizo ikiwa ni sehemu ya serikali kuwapatia msaada huo ili waweze kujisomea vizuri.
Amesema ni vyema kwa wanafunzi wanaofaulu kiwango cha juu kuwapatiya Mikopo hiyo ya elimu ya juu kutokana na chombo hicho kupewa jukumu la dhamana la kuwapatia mikopo ya gharama za elimu kwa wanafunzi na wafanya kazi wanaojiunga na vyuo vya elimu ya juu nchini ilikupata wataalamu baadae.
“Bodi ya mikopo ya Elimu ya juu imeendelea kutowa Mikopo pamoja na kukusanya Marejesho kutoka kwa Wahitimu wa taasisi za elimu ya juu waliopatiwa mikopo hiyo”, alisema Shamuhuna.
Aidha ameeleza kuwa mafanikio yaliopatikana katika mwaka 2012/2013 kutokana na kupatiwa mikopo ya Elimu ya juu ni misada kutoka Falme ya Oman ambayo aliitoa kuwasaida wanafunzi hao ambayo ikiwa ni sehemu ya ushirikiano na undugu walio nao muda mrefu.
Amesema idadi ya wanafunzi waliogharamiwa masomo kupitia Bodi ya mikopo hiyo iliongezeka kutoka wanafunzi 1,086 mwaka 2011/2012 hadi wanafunzi 1,897 mwaka 2012/2013
No comments:
Post a Comment