Habari za Punde

Zanzibar yakubali masharti ya maziwa makuu kuhusu ubakaji

Na Ali  Issa Maelezo  Zanzibar

 
Baraza  la Mapnduzi Zanzibar limetoa Maamuzi  juu ya suala zima la Ubakaji kisini Zanzibar kwa kuyakubali Masharti  yaliotolewa na Nchi za Maziwa Makuu katika mkutano wake ulio fanyika nchini Kongo mwaka jana  .
 
Maazimio hayo yalio pitishwa na nchi hizo,  Baraza la Mapinduzi limeyakubali masharti hayo ambayo ni pamoja na kuazishwa Mahakama maalum ya Kesi za Udhalilishaji , kuzifanya kesi hizo kuwa ni kesi maalum, kuipa madaraka Mahakama ya kufika katika tukio la uzalilishaji,na   Maamuzi ya kesi hizo zisizidi miezi sita pamoja na  kila nchi ichukue nafasi ya kulaani jambo hilo kwa kutoa matangazo mbali mbali kupitia vyombo vya habari na mawasiliano .
 
Hayo yamesemwa leo huko Baraza la Wakilishi Bweni nje kidogo ya mji wa Zanzibar na Waziri wa Katiba na  Sheria Abubakari Khamis Bakari wakati alipo kuwa akitoa jumla ya Majumisho katika ufafanuzi  wa Wizara ya katiba  kupitia Wizara ya Ustawi wa Jamii Maendeleo ya Wanawake na Watoto Barazani hapo 




Amesema  kutokana na suala hilo la uzalilishaji kuwa kubwa wizara yake imeshapewa jukumu na  Baraza la Mapinduzi la Zanzibar mara baadaya kukutana Mawaziri na kulijadili kwapamoja suala la ubakaji
Amesema baraza hilo lilipitisha maamuzi na kutakiwa wizara ya katiba na sheria iandae sheria kuishulikia jambo hilo la ubakaji na uzalilishaji .
Amesema kinacho fuata baada ya mamuzi hayo ,wizara yake hivisasa wamo  katika mchakato kuazisha sheria hiyo na itafanya kazi mara baada ya kupitishwa na kutiwa saini .
Amesema  katika sheria hyo mbali na hayo yatayo kuwemo  pia ni pamoja na kumuweka kiziwizini mtuhumiwa mpaka kesi hiyo imalizike, ili kuhofia kupoteza ushahidi
Jengine kufungwa miaka mingi mhusika wa ubakaji ili iwefundisho na kukomesha suala hilo .   
Mengine Waziri aliyataja kuwemo katika sheria hiyo kuorodhesha majina ya vyuo vyote vya Qraan  na kuvipa usajili, kwani inadaiwa baadhi ya walimu wa vyuo vya Quraan nao ni sehemu ya ubakaji watoto wadogo
Mengine ni kumuwekea kizuwizi mtoto wakati atapokuwa akitoa ushahidi ili aminike kwavile atakuwa hana wasiwasi ya kile anacho kizungumza akiwa hamuoni  mtuumiwa .
Aidha alisema pia suala jengine ni kuwashajihisha masheha na wanajamii,wazazi pia litakuwa sehemu ya ushahidi pamoja na kukitumia kifaa cha DNA kitakapokuwepo badae .   
Nae waziri wa wizara hiyo ya ustawi wa Jamii maendeleo ya wanawake, vijana na watoto Zainab Omar Mohamed akitoa majumuisho ya wizara hiyo alisema alisikitishwa sana juu ya maamuzi ya kesi hizo na kusema kwavile Wizara ya sheria tayari inaandaa utratibu mzuri kuna siku tatizo la udhalilishaji litakwisha.
Akizungumzia suala la maadili na malezi ya watoto   Wizara yake na kwa kushirikina na wizara ya elimu na mafunzo ya amali inandaa Sera ya kumlinda Mtoto ikiwemo malezi na mengineo.
Aidha alisema suala la pecheni ya wazee limo kwenye mchakato kuwapa pencheni kila mzee waumri utao tajwa wakati ukifika, pamoja na kusema baraza la vijana, na  watoto  litajadiliwa Oktoba mwaka huu kwangazi ya  shehia na  wilaya.

1 comment:

  1. kaka ni UZALILISHAJI AU UDHALILISHAJI ? AU mambo ya swaumu tu hayo !!
    ramadhani njema....

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.