Na Kija Elias, Rombo
MWANAFUNZI wa kidato pili katika shule ya sekondari Kilamvua wilayani Rombo mkoani Kilimanjaro (jina limehifadhiwa) anashikiliwa na polisi mkoani hapa kwa kosa la kufanya mapenzi na ng’ombe wao.
Mwanafunzi huyo alikutwa na baba yake mzazi akiwa uchi akifanya mapenzi na ng’ombe na alipomuona alijaribu kukimbia.
Lakini alimfukuza na alipomkamata alimfikisha kituo cha polisi wilayani Rombo kuchukuliwa hatua.
Watu wanaomfahamu mtoto huyo walisema mbali ya kumnajisi mnyama huyo pia aliwahi kukamatwa akimnajisi kuku ambae baadae alifariki.
Alipoulizwa kijana huyo alikiri kufanya mapenzi na ng’ombe, na kusema kuwa alijifunza mchezo huo kutoka kwa wenzake, ambao walikuwa wakifanya mapenzi na ng’ombe wakati wakiwa machungani.
Alisema amejikuta akizoea kufanya mapenzi na ng’ombe kutokana na kukataliwa na wasichana pindi anapowafuata kwa sababu wamekuwa wakitaka fedha nyingi na yeye hana.
No comments:
Post a Comment