Habari za Punde

Hadithi ya leo (14)


Mtume Muhammad Swalla Allaahu ‘alayhi wasallam amesema:

رحم الله رجلاً قام من الليل فصلي ،ثم أيقظ امرأته فصلت،فإن أبت نضح في وجهها الماء،ورحم الله امرأة قامت من الليل فصلت ثم أيقظت زوجها فصلي ،فإن أبي نضحت في وجهه الماء " (رواه النسائي)

Allaah humrehemu mwanamme anayeamka usiku na kusali  (Tahajjud) kisha akamuamsha mkewe naye akasali, na kama akikataa humrushia (humnyunyizia)  maji kwenye uso wake ( ili aamke). Na Allaah humrehemu mwanamke anayeamka usiku na kusali (Tahajjud) na kisha akamuamsha mumewe naye akasali na kama akikataa humrushia (humnyunyizia)  maji kwenye uso wake (ili aamke)

Imepokewa na Annasaaiy

Hadithi nyengine inayotuhimiza kujenga ushirikiano mkubwa kati ya mume na mke katika kufanya ibada hasa za usiku mkubwa.

Mume na mke wanapaswa kusaidiana katika kumtii Allaah Subhaanahu Wata’ala.
Ni fursa nzuri kulitumia hili kumi la mwisho ambapo tuoeneshe njia na mfano wa kuamshana na kuzitekeleza hizi ibada za usiku kwa ajili ya kupata radhi zake Allaah Subhaanahu Wata’ala na kwa kuweza kulipwa malipo yasiyokuwa na hesabu ndani ya mwezi mtukufu wa Ramadhaan, ndani ya siku kumi bora za mwisho wa mfungo wa Ramadhaan.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.