Habari za Punde

TDL yatoa msaada kwa wajane na yatima wa ajali ya Mv Spice na Skagit


 
 
 
 
 
Mkurugenzi wa Kampuni ya  Tanzania Distilleries Limited (TDL) David Mgwassa (kushoto), akiwakabidhi msaada wa vyakula na mafuta ya kupikia vyote vikiwa na thamani ya sh.milioni 9, wabunge wa Zanzibar, Ahmed Ngwali (kulia), wa Jimbo la Ziwani na Khalifa Suleiman wa Jimbo la Kagando kwa ajili ya kuwasaidia wajane na yatima waliofiwa na wategemezi wao katika ajali ya meli ya Mv Spice na Skagit zilizotokea visiwani humo. Makabidhiano hayo yalifanyika Dar es Salaam juzi.

 Mgwasa, alisema,”Kampuni yetu inatoa msaada hasa kwa ajili ya Mwezi huu Mtukufu wa Ramadhani ili watoto hawa yatima wakapate futari. Alisema msaada uliotolewa umelenga kuwasaidia yatima walioko Pemba kwanza. Mbunge wa Gando, Khalifa alisema “...Na pia wananchi wasitizame nani ametoa msaada ila ini amesaidia ili tu kuwasaidia hawa wenye uhitaji,” alisema Khalifa.
 
Chanzo - HabariLeo



2 comments:

  1. Huo msaadea vipi mbona kuna matangazo ya bia hapo, thats unacceptable

    ReplyDelete
  2. Jamani tumeambiwa msada nikitu chalazima kwa anaye hitajikusaidiwa haijalishi tangazo labia au lamzinga msadaulotolewa ni wa chakula kwa wajane na mayatima waliofiliwa kwa ajli yameli huko pba, hakuambiwa wanye bia au abebe bia. kinachongaliwa moyo wa kutoa ambao viongozi wingi wa muamsho hawana moyo huwo kaziyao fitina hatuwatoi mpaka watubu zambizao duwa zimewazuru,nawakae mpaka tupate zenji yetu huru tupumue

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.