Habari za Punde

Hotuba ya Waziri ya Bajeti ya Wizara ya Fedha Zanzibar.

                                HOTUBA YA WAZIRI WA NCHI, OFISI YA

                                  RAIS – FEDHA, UCHUMI NA MIPANGO YA MAENDELEO

                                               MHESHIMIWA OMAR YUSSUF MZEE

KUHUSU MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI KWA MWAKA WA FEDHA 2013/14

                                               KATIKA BARAZA LA WAWAKILISHI


I: UTANGULIZI

1. Mheshimiwa Spika, naomba kutoa hoja kwamba Baraza lako Tukufu sasa likae kama Kamati ili kupokea, kujadili na hatimae kupitisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi ya Rais Fedha, Uchumi na Mipango ya Maendeleo kwa mwaka wa fedha wa 2013/2014.2. Mheshimiwa Spika, Kwa unyenyekevu mkubwa nianze kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema kwa kutujaalia kukutana kwa mara nyengine katika kikao hiki kinachoendelea cha Baraza lako Tukufu kwa ajili ya kuwasilisha mapendekezo ya Bajeti ya Ofisi ya Rais Fedha, Uchumi na Mipango ya Maendeleo, tukiwa wazima na wenye afya njema. Itakumbukwa kuwa mwanzoni mwa kikao hiki niliwasilisha mapendekezo ya Bajeti ya Serikali ya mwaka 2013/2014, ambayo yaliidhinishwa na Baraza hili Tukufu. Nawashukuru nyote Waheshimiwa Wawakilishi.3. Mheshimiwa Spika, Kwa mara nyengine tena namshukuru sana Mheshimiwa Dkt Ali Mohamed Shein, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi kwa uongozi wake uliojaa hekima na imara kwa nchi yetu na imani yake kwangu binafsi. Nawashukuru pia, wasaidizi wake wakuu, Mheshimiwa Maalim Seif Sharif Hamad. Makamo wa Kwanza wa Rais na Mheshimiwa Balozi Seif Ali Iddi, Makamo wa Pili wa Rais kwa msaada na miongozo yao kwangu binafsi na kwa Ofisi yangu. Kwa ujumla shukurani zangu kwako wewe Mheshimiwa Spika kwa kutuongoza hapa Barazani hadi leo hii tunakaribia kuhitimisha kikao hiki muhimu cha Baraza kilichopitia, kushauri na kuidhinisha Mapendekezo ya bajeti za Wizara mbali mbali za Serikali yetu ya Mapinduzi. Kupitia kwako naishukuru pia Kamati ya Kudumu ya Fedha, Biashara na Kilimo inayoongozwa na Mheshimiwa Salmin Awadh Salmin kwa kupitia Mapendekezo haya, kuyatolea maelekezo na hatimae kuridhia yawasilishwe mbele ya Baraza lako Tukufu.4. Mheshimiwa Spika, Aidha, napenda kutoa shukrani zangu za dhati kwa uongozi wote wa Ofisi ya Raisi Fedha, Uchumi na Mipango ya Maendeleo, unaoongozwa na Ndugu Khamis Mussa Omar, Katibu Mkuu, Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango Ndugu. Amina Kh. Shaaban, Naibu Katibu Mkuu Ndugu Juma A. Hafidh, Wakuu wa Idara na Taasisi pamoja na Wafanyakazi wote wa Ofisi ya Rais Fedha, Uchumi na Mipango ya Maendeleo kwa michango na ushirikiano wao wanaonipa katika kutekeleza majukumu ya Ofisi hii.5. Mheshimiwa Spika, Baada ya maelezo haya ya utangulizi na shukurani, naomba nianze kwa kuwakumbusha wajumbe wa Baraza lako Tukufu majukumu ya Ofisi ya Raisi Fedha, Uchumi na Mipango na Maendeleo. Kimsingi majukumu ya Ofisi hii yamejikita katika maeneo mawili makuu:i) Mipango ya kitaifa (ikiwemo usimamizi wa Mipango ya Maendeleo ya Uchumi); na

ii) Fedha (masuala ya kitaifa na kisekta).Utendaji wa Ofisi hii kwa ujumla unasimamiwa na Katibu Mkuu na masuala ya Uchumi na Mipango ya Kitaifa yanasimamiwa na Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango.II: MAPITIO YA UTEKELEZAJI WA MPANGO NA BAJETI KWA MWAKA 2012/13 NA MALENGO YA MWAKA 2013/14

6. Mheshimiwa Spika, Utekelezaji wa majukumu ya Ofisi hii unaongozwa na Katiba ya nchi, Sheria za Kodi, Sheria za Fedha, Sheria ya Manunuzi, Sheria ya Ukuzaji Vitega Uchumi, Sheria ya Tume ya Mipango na Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi ya mwaka 2010, DIRA ya Maendeleo ya 2020, MKUZA II pamoja na maelekezo mbali mbali ya Tume ya Mipango, Baraza la Mapinduzi na miongozo ya Baraza la Wawakilishi.III: MAPATO NA MATUMIZI

7. Mheshimiwa Spika, Pamoja na kusimamia mapato ya nchi kwa ujumla, ambayo maelezo yake nimeshayatoa kwenye Hotuba ya Bajeti ya Serikali, Ofisi hii pia inawajibu wa kukusanya mapato ndani ya Idara zake na baadae kuingizwa kwenye Mfuko Mkuu wa Serikali. Katika kipindi cha mwaka 2012/13, Ofisi ya Rais Fedha, Uchumi na Mipango ya Maendeleo, ilikadiria kukusanya jumla ya TZS 4,049.42 milioni kutoka vyanzo mbali mbali vya ndani. Mpaka kufikia Juni 30, 2013, Ofisi iliweza kukusanya jumla ya TZS 3,921.90 milioni, sawa na asilimia 96.9 ya makadirio ya mwaka. (Kiambatisho Nam. I)8. Mheshimiwa Spika, Kwa mwaka 2012/13, Ofisi ya Rais Fedha, Uchumi na Mipango ya Maendeleo ilipangiwa kutumia jumla ya TZS 131,500.0 milioni, ambapo TZS 37,249.00 milioni kwa kazi za kawaida, TZS 38,352.0 milioni kwa kazi za maendeleo. Kati ya fedha za maendeleo TZS 8,325.0 milioni kama ni mchango wa Serikali na TZS 30,027.0 milioni ikiwa ni misaada na mikopo kutoka nje. Mfuko Mkuu wa Serikali ulikadiriwa kutumia TZS 54,900.00 milioni. Bajeti hii imeongezeka baada ya kufanya uhaulishaji kwa ajili ya ununuzi wa meli ya Serikali. Katika utekelezaji wa majukumu yake, Ofisi imeweza kutumia jumla ya TZS 37,249.00 milioni sawa na asilimia 100 kwa kazi za kawaida (Kiambatisho II) na TZS 8,897.84 milioni kwa kazi za maendeleo (Kiambatisho III).9. Mheshimiwa Spika, Katika kuelezea utekelezaji wa fedha kwa mwaka uliopita. Kiambatisho Nam. IV kinaonesha mchango wa Serikali katika matumizi ya Programu na miradi ya maendeleo Ki-Idara ambapo jumla ya TZS 4,202.13 milioni sawa na asilimia 50 zilitumika. Kiambatisho Nam. V kinaonesha fedha zilizopatikana kama mchango wa Serikali kimradi. Matumizi ya TZS 54,900.00 milioni yalifanyika kutoka Mfuko Mkuu wa Serikali sawa na asilimia 100 ya makadirio ya mwaka 2012/13. Viambatisho Nam. VI na VII vinaonyesha mgawanyo wa rasilimali kwa kazi za kawaida na maendeleo kwa mwaka 2013/14.10. Mheshimiwa Spika, Baada ya kueleza muhtasari wa mapato na matumizi sasa naomba nieleze mapitio ya utekelezaji wa mipango na bajeti ki–Idara na taasisi na kuelezea malengo ya mwaka 2013/14.IV: UTEKELEZAJI 2012/2013 NA MAKADIRIO 2013/2014 KI-IDARA NA TAASISI

A: TUME YA MIPANGO

11. Mheshimiwa Spika, Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 imeanzisha Tume ya Mipango kuwa ndio chombo cha juu kabisa kwa ajili ya kupanga Maendeleo yetu ya Kiuchumi na kijamii. Tume hii imeundwa upya kufuatia kutungwa kwa Sheria mpya Namba 3 ya mwaka 2012. Sekretarieti ya Tume hii ya Mipango inaundwa na Idara tatu na Taasisi moja inayojitegemea katika kusimamia masuala ya Uchumi na Mipango ya Maendeleo. Idara na taasisi hizo ni, Idara ya Mipango ya Kitaifa, Maendeleo ya Kisekta na Kupunguza Umaskini, Idara ya Ukuzaji Uchumi, Idara ya Mipango na Maendeleo ya Watendakazi na Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali.12. Mheshimiwa Spika, Utekelezaji wa Idara zinazounda Sekretarieti ya Tume ya Mipango ni kama ifuatavyo:A.1 IDARA YA MIPANGO YA KITAIFA, MAENDELEO YA KISEKTA NA KUPUNGUZA UMASKINI

13. Mheshimiwa Spika, Jukumu kubwa la Idara hii ni kuangalia Mipango ya Kitaifa kwa ujumla na jinsi Sekta mbali mbali zinavyotekeleza masuala mbali mbali ambayo yanasaidia katika kupunguza umasikini. Kwa mwaka 2012/2013, Idara iliidhinishiwa jumla ya TZS 225.90 milioni kwa kazi za kawaida na TZS 2,318.2 milioni kwa kazi za maendeleo. Hadi kufikia mwezi Juni 2013, Idara ilishapatiwa jumla ya TZS 225.90 milioni kwa kazi kawaida sawa na asilimia 100 na TZS 1,382.6 milioni kwa kazi za maendeleo sawa na asilimia 59.6 ya makadirio. Fedha hizi zilitumika katika kutekeleza yafuatayo:

i) Kuchapisha nakala 300 za vitabu vya Mapitio ya Hali ya Uchumi na Mpango wa Maendeleo 2012/2013 na vitabu 500 vya Mwelekeo wa Hali ya Uchumi na Mpango wa Maendeleo wa mwaka 2013/2014;

ii) Kufuatilia utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo wa mwaka 2012/2013 wenye programu 22 na Miradi 81 ya maendeleo Unguja na Pemba, ambapo changamoto mbali mbali zilijitokeza zikiwemo, fedha za Miradi kuhaulishwa na kutumika kinyume na shughuli zilizokusudiwa. Changamoto hizi zinaendelea kutafutiwa ufumbuzi unaostahiki ili kuleta ufanisi wa utekelezaji;

iii) Kufanya mapitio ya Sekta ya Fedha katika maeneo ya huduma za kibenki, huduma ndogo ndogo za kifedha, shughuli za Bima, Soko la mitaji, shughuli za mifuko ya Hifadhi ya Jamii. Kazi ya mapitio inatarajiwa kukamilika katika robo ya kwanza ya mwaka 2013/14;

iv) Kutayarisha ripoti ya mwaka ya utekelezaji wa MKUZA II, 2012/13 inayotarajiwa kukamilika robo ya kwanza ya 2013/14;

v) Utayarishaji wa kuandaa kanuni za Sheria ya Tume ya Mipango;

vi) Kuandaa Vikao viwili vya Tume ya Mipango.14. Mheshimiwa Spika, Kwa mwaka 2013/2014, Idara inaombewa jumla ya TZS 688.20 milioni kwa kazi za kawaida na TZS 4,419.80 milioni kwa kazi za maendeleo. Kazi zilizopangwa kutekelezwa katika mwaka wa fedha 2013/2014 ni:

i) Kukusanya na kuandaa taarifa za Mpango wa Maendeleo kwa mwaka 2013/2014 na kuandaa Mwelekeo wa Hali ya Uchumi na Mpango wa Maendeleo kwa mwaka 2014/2015;

ii) Kufuatilia utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo wa mwaka 2013/2014 wenye programu 35 na miradi 75 ya maendeleo Unguja na Pemba;

iii) Kuandaa kikao na Taasisi za Serikali na zisizo za Kiserikali kwa ajili ya matayarisho ya bajeti ya maendeleo ya mwaka 2014/15;

iv) Kuandaa vikao vinne vya Tume ya Mipango na sita vya kamati Tendaji ya Tume;

v) Kuandaa Mafunzo kwa Maafisa Mipango 40 wa wizara 16 za Serikali kuu, Serikali za mitaa na Taasisi juu ya uchambuzi wa Sera (Policy Analysis);

vi) Kuandaa maonesho ya maadhimisho ya wiki ya Umasikini;

vii) Kufanya Uchambuzi wa Hali ya Umasikini kwa vijiji vitano (5) na kuandaa taswira ya Umasikini (Poverty Profile) kwa kuzingatia Ripoti ya Utafiti wa Mapato na Matumizi ya Kaya;

viii) Kutoa mafunzo kwa watendaji 35 juu ya Uandaaji wa Mipango;

ix) Kutoa mafunzo ya ufuatiliaji na tathmini yenye kuleta matokeo kwa watendaji wa vitengo vya Ufuatiliaji na Tathmini vya wizara za Serikali;

x) Kutayarisha mfumo wa ufuatiliaji ICT wa Upatikanaji na uwekaji wa Taarifa;

xi) Kuandaa taarifa za maendeleo ya watu Zanzibar (ZHDR) na utekelezaji wa Malengo ya Milenia (MDGs);

xii) Kufanya tathmini ya mahitaji ya vifaa, mafunzo na muundo wa Taasisi ndani ya Tume ya Mipango na Idara za Mipango, Sera na Utafiti pamoja na kuandaa mpango kazi ili kuimarisha utendaji wa taasisi hizi;

xiii) Kuratibu vikao vya Kamati ya Uongozi na Kamati ya Wataalamu ya Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (MKURABITA).A2. IDARA YA UKUZAJI UCHUMI

15. Mheshimiwa Spika, Jukumu kuu la Idara hii ni kuangalia mwenendo mzima wa ukuaji Uchumi wa Zanzibar. Kwa mwaka wa fedha wa 2012/13, idara ilipangiwa kutumia TZS 288.018 milioni kwa kazi za kawaida, na TZS 150.00 milioni kwa kazi za Maendeleo. Hadi kufikia Juni 2013, Idara iliweza kutumia jumla ya TZS 288.018 milioni kwa kazi za kawaida sawa na asilimia 100 ya makadirio ya mwaka. Aidha, TZS 22.8 milioni zilitumika kwa kazi za Maendeleo sawa na asilimia 15 ya makadirio. Katika kutumia fedha hio, Idara imeweza kutekeleza mambo yafuatayo:

i) Kufuatilia Mwenendo wa Uchumi kwa kutoa taarifa ya Pato la Taifa kwa kila robo mwaka kwa kushirikiana na Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali (OCGS) na Benki Kuu ya Tanzania Tawi la Zanzibar;

ii) Kutathmini na kushauri juu ya mwenendo wa Mfumko wa bei kila mwezi;

iii) Utunzaji wa Taarifa za Takwimu za Kifedha za Serikali (GFS) kwa kuwekewa “Database” litakaloendelea kufanyiwa mapitio kila Takwimu mpya zinapotolewa;

iv) Kufanya mapitio ya mfumo wa utabiri (Modeli) wa Uchumi na wa mapato kwa kila takwimu mpya zinapotolewa kwa ajili ya kutabiri mwenendo wa viashiria vya Uchumi na Mapato;

v) Kupendekeza marekebisho ya sheria za kodi kupitia kitengo cha sera za kodi kwa kushirikiana na wadau mbali mbali wakiwemo Sekta binafsi;

vi) Kuanzisha Kitengo kinachoshughulikia Miradi itakayoekezwa kwa mashirikiano ya Serikali na Sekta binafsi (Public Private Partnership);

vii) Kufanya mafunzo ya awali ya modeli ya programu ya kifedha (financial programming) kwa wafanyakazi;

viii) Kujenga uwezo wa Idara kwa kuwapatia wafanyakazi sita (6) mafunzo ya muda mrefu katika ngazi ya shahada ya pili na wafanyakazi sita (6) mafunzo ya muda mfupi katika nyanja mbalimbali za kiuchumi ndani na nje ya nchi;

ix) Kuandaa na kuutumia mfumo mpya wa taarifa unaohusiana na idadi za bidhaa (New CPI basket) katika kufanya uchambuzi na kutoa taarifa sahihi za mwenendo wa bei za bidhaa nchini;

x) Kuiwakilisha Serikali katika vikao vya kitaalamu vya Kikanda ikiwa ni pamoja na vikao vya Jumuiya ya Afrika Mashariki, Mashirikiano na nchi za Jumuiya ya Umoja wa Ulaya na Mashirikiano ya Jumuia ya Utatu, (EAC- COMESA na SADC).16. Mheshimiwa Spika, Kwa mwaka wa fedha 2013/2014, Idara inaombewa jumla ya TZS 426.69 milioni kwa kazi za kawaida na TZS 150.00 milioni kwa kazi za maendeleo kwa kutekeleza mambo yafutayo:

i) Kutoa taarifa ya Pato la Taifa kwa kila robo mwaka kwa kushirikiana na Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali (OCGS) ili kujua mchango na ukuaji wa kila sekta katika Pato laTaifa;

ii) Kupitia na kuchambua taarifa za hali ya mfumko wa bei na kufuatilia mwenendo wake kwa kila mwezi ili kutoa mapendekezo ya hatua za muda mfupi na mrefu za kudhibiti mfumko wa bei nchini;

iii) Kuimarisha kitengo cha kutunza Taarifa zaTakwimu za kifedha za serikali (GFS) kwa kuendelea kuliongezea Database Moduli mpya kila zinapopatikana taarifa;

iv) Kuandaa tafiti mbili za kiuchumi katika maeneo ya mchango wa wajasiriamali wadogo na wa kati katika Uchumi na utafiti juu ya Maendeleo ya viwanda Zanzibar;

v) Kuimarisha kitengo cha Mashirikiano baina ya Sekta ya Umma na sekta Binafsi (Public Private Partnership) kwa kuwajengea uwezo wafanyakazi, kukamilisha Sera, mapitio ya sheria na muongozo juu ya Mashirikiano hayo;

vi) Kufanya mapitio na kuendeleza mfumo wa utabiri (Modeli) wa uchumi na wa mapato kila takwimu mpya zinapotolewa ili kurahisisha kufanya makadirio ya viashiria vya uchumi;

vii) Kuratibu mapendekezo ya marekebisho ya kodi kupitia kitengo cha sera ya kodi na kutoa ushauri juu ya mwenendo wa kodi;

viii) Kuanza kutumia programu ya kifedha (financial programming) kwa kufanya utabiri wa uchumi wa kila robo mwaka;

ix) Kuendelea kuiwakilisha Serikali katika mikutano, majadiliano na kufuatilia masuala yanayohusu ushirikiano wa kikanda.A3. IDARA YA MIPANGO NA MAENDELEO YA WATENDAKAZI

17. Mheshimiwa Spika, Kwa ujumla idara hii ina jukumu la kuangalia maendeleo ya Watendakazi na hali ya Ukuaji wa Idadi ya Watu. Kwa mwaka 2012/2013, Idara ilipangiwa kutumia TZS 188.47 milioni kwa kazi za kawaida na TZS 190.00 milioni kwa kazi za maendeleo kama mchango wa Serikali. Mpaka kufikia mwishoni mwa mwaka, Idara ilifanikiwa kupata jumla ya TZS 188.47 milioni kwa kazi za kawaida sawa na asilimia 100 ya makadirio na TZS 176.11 milioni ni mchango wa Serikali kwa kazi za Maendeleo sawa na asilimia 92.7 ya makadirio. Matumizi ya fedha hizi yalielekezwa katika maeneo yafuatayo:

i) Kuandaa utafiti mdogo juu ya umakini wa mafunzo ya amali katika ajira;

ii) Kuendelea na zoezi la ukusanyaji wa taarifa za utafiti wa Hali ya Utumishi Unguja na Pemba;

iii) Kuandaa mikutano miwili (2) ya wadau wa masuala ya idadi ya watu Zanzibar kwa robo tatu za mwaka 2012/2013;

iv) Kutayarisha na kuiwasilisha kwa wadau taarifa ya mwaka 2012 juu ya masuala ya Idadi ya Watu na Maendeleo Zanzibar yenye ujumbe wa “Vijana na Ajira”;

v) Kutoa mafunzo kwa Wakurugenzi Mipango, Sera na Utafiti na maafisa Mipango wapatao 35 juu ya kuoanisha viashiria vya idadi ya watu katika mipango ya maendeleo na bajeti;

vi) Kwa usaidizi wa mtaalamu wa ndani, Idara imefanya tathmini, mapitio na majaribio ya daftari la shehia na matokeo yake yameshajadiliwa katika mikutano miwili ya wadau;

vii) Kufanya tathmini juu ya utekelezaji wa program ya Uhai, Hifadhi, Maendeleo ya Mama na Mtoto (YCSPD) katika ngazi ya Shehia na wilaya Unguja na Pemba.18. Mheshimiwa Spika, Kwa mwaka 2013/2014, Idara inaombewa jumla ya TZS 149.104 milioni kwa kazi za kawaida na TZS 342.00 milioni kwa kazi za maendeleo ili kutekeleza yafuatayo:

i) Kufanya uratibu juu ya masuala ya idadi ya watu, watendakazi na ustawi wa mama na mtoto katika ngazi mbalimbali;

ii) Kukamilisha utafiti wa umakini wa mafunzo ya amali katika ajira na taarifa zake kuziwasilisha kwa wadau Unguja na Pemba;

iii) Kuendelea na hatua za utafiti wa Hali ya Utumishi Nchini kwa kukamilisha ukusanyaji wa taarifa, uchambuzi na uandikaji ripoti;

iv) Kutafsiri kwa lugha ya Kiswahili ripoti juu ya Hali na Ustawi wa wastaafu Zanzibar 2012/2013;

v) Kufanya mapitio ya vipaumbele juu ya mahitaji ya wataalamu nchini kutokana na Matokeo ya Utafiti wa Hali ya Utumishi;

vi) Kuchapisha daftari la shehia lililofanyiwa mapitio na kutoa mafunzo kwa masheha na wasaidizi wao juu ya matumizi yake;

vii) Kutayarisha ripoti ya mwaka 2013/14 juu ya masuala ya idadi ya watu Zanzibar, pamoja na kuandaa mikutano ya kila robo mwaka juu ya masuala ya idadi ya watu;

viii) Kushiriki katika maandalizi na kilele cha maadhimisho ya siku ya idadi ya watu duniani ya mwaka 2014;

ix) Kutayarisha ripoti (thematic paper) juu ya masuala ya idadi ya watu na athari zake kijamii na kiuchumi kwa madhumuni ya kuwasilishwa kwenye kikao cha Tume ya Mipango;

x) Kutafsiri na kuchapisha Ripoti ya tathmini juu ya takwimu za kijamii;

xi) Kuandaa mikutano miwili ya Kamati ya Wataalamu juu ya programu ya Uhai, Hifadhi na Maendeleo ya Mama na Mtoto;

xii) Kutathmini utekelezaji wa program ya hifadhi ya mama na mtoto katika ngazi ya sekta, wilaya na shehia;

xiii) Kufanya tathmini juu ya sababu zinazopelekea kuongezeka kwa matukio ya vifo vinavyotokana na uzazi pamoja na mapungufu katika masuala ya lishe na usafi wa mazingira kwenye ngazi za Shehia.A4. OFISI YA MTAKWIMU MKUU WA SERIKALI

19. Mheshimiwa Spika, Jukumu kubwa la Ofisi hii ni kukusanya na kuzichambua takwimu za kiuchumi na kijamii. Katika mwaka wa fedha 2012/13 Ofisi ya Mtakwimu Mkuu SMZ ilipangiwa jumla ya TZS 1,262 milioni kwa ajili ya utekelezaji wa kazi za kawaida na TZS 2,900 milioni kwa utekelezaji wa kazi za miradi ya Maendeleo.20. Mheshimiwa Spika, Mpaka kufikia mwishoni mwa mwezi Juni 2013, jumla ya TZS 1,262 milioni sawa na asilimia 100 ya makadirio ziliweza kupatikana kwa kutekeleza kazi za kawaida na TZS 1,164 milioni sawa na asilimia 40 ya makadirio zilipatikana kwa ajili ya kazi za maendeleo.21. Mheshimiwa Spika, Katika kutekeleza majukumu yake, Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali iliweza kufanya yafuatayo:

i) Kukusanya Takwimu za Kijamii na Hali ya Uchumi wa Zanzibar kwa mwaka 2012 na kutoa Ripoti yake, iliyobainisha ukuaji wa uchumi wa Zanzibar kwa mwaka 2012;

ii) Kukamilisha matayarisho yote na kusimamia kwa upande wa Zanzibar Sensa ya Watu na Makazi ya Tanzania, iliyofanyika tarehe 26 Agosti, 2012;

iii) Kufanya tafiti katika sekta ya uzalishaji na viwanda, utalii, uwekezaji, na utumiaji wa huduma ya maji Zanzibar ambapo utafiti wa uzalishaji wa viwanda,utalii na uwekezaji ripoti zake bado ambapo utafiti wa utumiaji wa huduma ya maji Zanzibar ripoti yake imekamilika na kuonesha matumizi, mtandao na upatikanaji wa maji nchini;

iv) Kukamilisha na kuwasilisha kwa wadau taarifa za tafiti nne (4) juu ya Viashiria vya UKIMWI, Malaria, Sensa ya Kilimo na ile ya Mifugo za mwaka wa 2011/12;

v) Kuwapatia mafunzo katika ngazi ya Shahada ya uzamili (Masters Degree) jumla ya maafisa Takwimu (7), mmoja (1) katika fani ya TEHAMA na Takwimu, Ofisa mmoja (1) katika Stashahada ya Uzamili (Post Graduate Diploma), mmoja (1) katika fani ya Uchambuzi wa Umasikini, (Poverty Analysis), maafisa sita (6) katika ngazi ya Shahada ya kwanza katika fani ya Takwimu na Uchumi, na maofisa wawili (2) Stashahada katika fani ya takwimu na rasilimali watu;

vi) Kuwapatia jumla ya maofisa kumi na moja (11) mafunzo ya muda mfupi katika fani za Uhasibu, Uongozi wa miradi ya maendeleo, Ukaguzi na Tathmini (Monitoring & Evaluation), Rasilimali watu (HR), na masuala ya Takwimu (Statistical packages).22. Mheshimiwa Spika, Kwa mwaka 2013/2014, Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali inaombewa jumla ya TZS 1,550 milioni ikiwemo ruzuku ya TZS 1,300 milioni kwa ajili ya utekelezaji wa kazi za kawaida na jumla ya TZS 250.0 milioni kwa ajili ya utekelezaji wa mradi mmoja wa Maendeleo. Ofisi inatarajia kupokea jumla ya TZS 3,933.0 milioni kama mkopo kutoka Benki ya Dunia kwa ajili ya utekelezaji wa Mradi wa Uimarishaji Takwimu Tanzania (TSMP) kwa upande wa Zanzibar, na TZS 36.0 milioni zinatarajiwa kutoka Benki Kuu ya Tanzania ikiwa ni mchango wake kwa ajili ya ukusanyaji wa takwimu za Faharisi ya Bei (Consumer Price Index) na takwimu zaPato la Taifa kwa robo mwaka. Mambo yaliyopangwa kutekelezwa ni pamoja na:i) Kufanya Utafiti wa Hali ya Uchumi wa Zanzibar kwa mwaka 2013 na kutoa taarifa yake ikiwa ni pamoja na taarifa ya makadirio ya ukuaji uchumi wa Zanzibar kwa mwaka 2013;

ii) Kutekeleza Mpango wa Sensa na Utafiti kwa kufanya tafiti zikiwemo za Sekta Isiyo Rasmi (Zanzibar Informal Sector Survey), Utafiti wa Hali ya Nguvu Kazi (Zanzibar Integrated Labour Force Survey), Utafiti wa Viashirio vya Kiuchumi na Kijamii (Tanzania Panel Survey), Utafiti wa Sekta ya Biashara, Usafiri na Ujenzi (Integrated Survey on Trade, Transport and Communication);

iii) Kuendelea na Uchambuzi wa takwimu za Sensa ya Watu na Makaazi na kutoa taarifa zake;

iv) Kutekeleza Mradi wa Uimarishaji Takwimu Tanzania (TSMP) ikiwa ni pamoja na kuanza kazi za usanifu na uchoraji wa ramani za jengo la Makao Makuu ya Ofisi ya Mtakwimu Mkuu Zanzibar;

v) Kuendeleza na kukuza taaluma za kitakwimu hapa Zanzibar ikiwa ni pamoja na kuwapatia mafunzo maofisa takwimu, kuendesha semina na mikutano ya watoaji na watumiaji wa takwimu, kuimarisha mifumo ya utoaji na uhifadhi wa takwimu kwa kutumia mitandao ya “Tanzania Socio-Economic Database” (TSED) na “National Data Archives” (NADA), na kutoa miongozo ya ukusanyaji, uchambuzi na uwekaji wa takwimu rasmi miongoni mwa Idara na Taasisi za Serikali.B: MASUALA YA FEDHA

23. Mheshimiwa Spika, Kama nilivyotangulia kusema, Ofisi yangu inasimamia Uchumi na Mipango ya Maendeleo kupitia Tume ya Mipango. Ofisi pia inasimamia masuala ya Fedha Serikalini. Idara zinazosimamia masuala ya fedha ni Idara ya Mhasibu Mkuu wa Serikali, Idara ya Bajeti, Idara ya Uhakiki mali na Mitaji ya Umma, na Idara ya Fedha za Nje.Baada ya kukamilisha maelezo yanayohusu masuala ya Uchumi na Mipango, naomba sasa nieleze masuala ya Fedha.B1. IDARA YA MHASIBU MKUU WA SERIKALI

24. Mheshimiwa Spika, Idara hii ndio inayosimamia masuala ya fedha nchini ikiwemo utunzaji wa mapato, udhibiti wa matumizi pamoja na kuwaendeleza Wahasibu na Wakaguzi. Kwa mwaka wa fedha wa 2012/13, Idara ilipangiwa kutumia jumla ya TZS 2,371.163 milioni kwa kazi za kawaida na TZS 40.0 milioni kwa kazi za maendeleo. Hadi kufikia mwezi Juni 2012/13, Idara ilipatiwa jumla ya TZS 2,371.163 milioni sawa na asilimia 100 ya makadirio kwa kazi za kawaida na jumla ya TZS 38.0 milioni sawa asilimia 95 kwa kazi za Maendeleo. Mambo yaliyotekelezwa kwa mwaka huo ni:

i) Kusimamia mapato na kuendelea kuimarisha udhibiti na usimamizi wa matumizi ya Serikali;

ii) Kukamilisha ufungaji wa hesabu za mwaka 2011/12 na kuziwasilisha kwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali;

iii) Kuratibu vikao kumi na moja (11) vya kila mwezi vya Kamati za Ukomo wa matumizi;

iv) Kulipa kwa wakati TZS 132,660.00 milioni kwa ajili ya mishahara Serikalini, TZS 100,020.00 milioni kwa matumizi mengineyo na TZS 31,270.00 milioni zikiwa ni mchango wa Serikali kwa Miradi ya Maendeleo;

v) Kupokea TZS 21,000.00 milioni sawa na asilimia 98 ya makadirio ya TZS 21,400 milioni kutoka Serikali ya Muungano wa Tanzania ikiwa ni kodi ya wafanyakazi wa Muungano wanaofanya kazi Zanzibar;

vi) Kulipa TZS 8,649.02 milioni mafao ya pencheni na TZS 6,968.74 milioni kiinua mgongo kwa wastaafu 747;

vii) Kutoa mafunzo ya muda mrefu na mfupi kwa Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu za Ndani wapatao 50;

viii) Kuchapisha vitabu 15,900 vya Risiti za Serikali;

ix) Kusimamia na kuendeleza mfumo wa pamoja wa Usimamizi wa fedha (Integrated Financial Management System - IFMS);

x) Kusimamia deni la Taifa na kuhudhuria vikao vya Wataalam wa Kamati ya Madeni huko Tanzania Bara; na

xi) Kufanya mapitio ya sheria ya Fedha Namba 12 ya mwaka 2005 na kutoa Rasimu ya kwanza ya Ripoti hiyo.25. Mheshimiwa Spika, Kwa mwaka 2013/2014 Idara inaombewa jumla ya TZS 3,183.57 milioni kwa kazi za kawaida na TZS 40.00 milioni kwa kazi za maendeleo ikiwa ni mchango wa Serikali katika kugharamia Programu ya Mageuzi ya Usimamizi wa Fedha za Umma. Aidha, Idara kupitia Mfuko Mkuu wa Serikali imetengewa jumla ya TZS 66,056.00 milioni kusimamia matumizi ya Mfuko Mkuu. Mambo yatakayotekelezwa kwa mwaka 2013/2014 ni kama yafuatayo:

i) Kusimamia mapato na kuendelea kuimarisha udhibiti na usimamizi wa matumizi ya Serikali;

ii) Kusimamia matumizi ya Mfuko Mkuu wa Serikali;

iii) Kutoa mafunzo mafupi ya Uhasibu na Ukaguzi kwa wafanyakazi wa kada ya uhasibu na ukaguzi wa fedha wapatao 70;

iv) Kufunga hesabu za Serikali za mwaka 2012/13;

v) Kusimamia na kuimarisha mfumo wa fedha wa IFMS kuendana na mfumo wa PBB na kubadilisha “Server”;

vi) Kuchapisha vitabu 22,000 vya Risiti za Serikali;

vii) Kuziimarisha na Kuzijengea uwezo Kamati za ukaguzi za Wizara za SMZ;

viii) Kusimamia Deni la Taifa;

ix) Kuratibu vikao kumi na moja (11) vya kila mwezi vya Kamati ya Ukomo wa Matumizi;

x) Kusimamia marekebisho ya Sheria ya Fedha za Umma ili iendane na wakati;

xi) Kuhudhuria vikao mbalimbali vya Kamati ya Wataalam wa deni la Taifa na kamati ya Ukomo vinavyofanyika huko Tanzania Bara;

xii) Kusimamia ukusanyaji wa TZS 26,000.00 milioni kutokana na wafanyakazi wa SMT wanaofanya kazi Zanzibar.B2. IDARA YA BAJETI

26. Mheshimiwa Spika, Jukumu la Idara hii ni kusimamia Bajeti na matumizi ya Serikali pamoja na kuratibu mifumo ya Bajeti Serikalini. Kwa mwaka wa fedha wa 2012/2013, Idara ilipangiwa kutumia jumla ya TZS 21,712.77 milioni kwa kazi za kawaida. Kati ya Fedha hizo, TZS 5,010.00 milioni ni kwa ajili ya marekebisho ya Mishahara Serikalini, TZS 426.4 milioni ni matumizi ya Idara na TZS 16,276.0 milioni kwa ajili ya Ruzuku kwa Taasisi zilizo chini ya Ofisi. Hadi kufikia mwisho wa mwezi wa Juni 2013 Idara ilitumia jumla TZS 21,712.77 milioni sawa na asilimia 100 ya Makadirio, ambapo TZS 2,490 milioni zimetumika kwa marekebisho ya Mshahara, TZS 426.4 milioni kwa kazi zake za kawaida za Idara na TZS 2,520 milioni zilihaulishwa kwenda katika kifungu cha safari za Nje za Viongozi Wakuu. Fedha za Idara zilitumika katika kutekeleza majukumu yafuatayo:

i) Kusimamia, kufuatilia na kuandaa taarifa ya utekelezaji wa Bajeti ya mwaka 2012/2013;

ii) Kuratibu shughuli za kibajeti kwa kuhakikisha kwamba Wizara na Taasisi za Serikali zinatekeleza bajeti zao kulingana na mfumo wa MTEF;

iii) Kuratibu utayarishaji na kutoa mafunzo kwa maofisa mipango na wahasibu wa Wizara na Taasisi husika juu ya Bajeti inayozingatia Programu (PBB);

iv) Kuandaa Warsha ya uwasilishaji wa taarifa (feedback) kutoka IMF East AFRITAC juu ya mfumo wa PBB kwa Wakurugenzi Mipango, Sera na Utafiti baada ya mapitio ya Wizara sita za SMZ;

v) Kuwapeleka wafanyakazi wanne (4) kwenye mafunzo ya kivitendo nchini Mauritius na wanne (4) nchini Rwanda yanayohusiana na mchakato wa utayarishaji wa bajeti inayozingatia programu (PBB);

vi) Kusimamia utayarishaji wa maelezo ya bajeti inayozingatia Programu kwa ajili ya kuwasilishwa Baraza la Wawakilishi;

vii) Kufanya uhakiki juu ya mishahara kwa wafanyakazi wanaopelekea mishahara yao benki;

viii) Kuandaa mapendekezo ya Bajeti ya Serikali kwa mwaka 2013/2014.27. Mheshimiwa Spika, Kwa mwaka wa fedha 2013/2014 Idara inaombewa jumla ya TZS 36,834.12 milioni kwa kazi za kawaida, zikiwemo TZS 17,500 milioni kwa ajili ya marekebisho ya mishahara Serikalini, TZS 18,663.00 milioni kwa ajili ya Ruzuku kwa Taasisi zilizo chini ya Ofisi ya Rais Fedha, Uchumi na Mipango ya Maendeleo na TZS 671.1 milioni kwa ajili ya matumizi ya kawaida ya Idara. Mambo yaliyopangwa kutekelezwa na Idara hii ni haya yafuatayo:

i) Kukamilisha Mswaada wa Sheria mpya ya Fedha;

ii) Kutayarisha na kutoa muongozo wa bajeti kwa Wizara na Taasisi husika za Serikali hadi kufikia Disemba 2013;

iii) Kuratibu utayarishaji na kutoa mafunzo kivitendo kwa Wizara zote kumi na sita (16) juu ya Bajeti inayozingatia Programu (PBB);

iv) Kuandaa database ya viashiria vya utekelezaji na matokeo (KPI Database), Muongozo wa Viashiria vya utekelezaji na kutoa mafunzo kwa maofisa OR-FUMM;

v) Kuwapatia Mafunzo Waheshimiwa Wajumbe wa Baraza la Mapinduzi, Baraza la Wawakilishi, Makatibu Wakuu na Wakuu wa Taasisi za Kijamii (CSO) juu ya Muundo na mfumo wa bajeti inayozingatia Programu (PBB);

vi) Kwa kushirikiana na Mhasibu Mkuu wa Serikali, kuandaa mafunzo na kufanya marekebisho ya kitaalamu katika mfumo wa hesabu (Charts of Account) pamoja na kuoanisha fedha na bajeti;

vii) Kwa kushirikiana na Idara ya Mipango ya Maendeleo ya Kitaifa, Idara ya Mhasibu Mkuu wa Serikali, Idara ya Ukuzaji Uchumi na Idara Fedha za Nje, kutoa taarifa za bajeti kwa wananchi kwa lengo la kuwaelewesha mafungamano (Intergration) ya uchumi wa nchi na bajeti;

viii) Kuimarisha uwezo wa watendaji wa Idara kwa kuwapatia mafunzo katika maeneo ya uandaaji na uchambuzi wa taarifa pamoja na kuwapatia vitendea kazi;

ix) Kuimarisha mfumo wa usimamizi na database ya Mishahara na Taarifa za Watendakazi.B3. IDARA YA FEDHA ZA NJE

28. Mheshimiwa Spika, Jukumu la Idara ya Fedha za Nje ki ujumla ni kuimarisha uhusiano wetu na wafadhili kutoka nje pamoja na upatikanaji wa fedha kwa ajili ya maendeleo yetu. Kwa mwaka wa fedha 2012/2013 idara Ilitarajiwa kuratibu na kusimamia upatikanaji wa jumla ya TZS 331,300 milioni ikiwa ni ruzuku na mikopo). Fedha hizo zinajumuisha TZS 105,400 milioni kama ruzuku, TZS 187,800 milioni kama mkopo na TZS 39,900 milioni ni misaada ya kibajeti.29. Mheshimiwa Spika, Hadi Kufikia Juni 2013 Idara imeweza kuratibu upatikanaji wa jumla ya TZS 223,400 milioni sawa na asilimia 67.45 ya makadirio kutoka kwa Washirika wa Maendeleo na Mashirika ya kimataifa. Kati ya fedha hizo, TZS 22,110 millioni ni misaada ya kibajeti sawa na asilimia 55 ya makadirio ya TZS 39,900 milioni. Kwa upande wa Programu na miradi ya Maendeleo, Idara imeratibu upatikanaji wa TZS 201,300 milioni. Kati ya hizo TZS 131,800 milioni ni ruzuku sawa na asilimia 125.05 ya makadirio ya TZS 105,400 milioni. Ongezeko hili limetokana na kuwa hakukuwa na makadirio ya matumizi ya mradi wa usambazaji wa umeme Unguja kupitia Shirika la Maendeleo la Japan (JICA) na makadirio madogo kwa mradi wa utandazaji wa waya wa umeme chini ya bahari kutoka Rasi Kiromoni hadi Fumba kupitia Changamoto ya Milenia ya Marekani (MCC-A).30. Mheshimiwa Spika, Kwa mwaka wa 2012/2013 Idara iliidhinishiwa matumizi ya TZS 120. 45 milioni kwa kazi za kawaida na TZS 1,382.0 milioni kwa kazi za Maendeleo. Hadi kufikia June 2013 Idara ilitumia jumla ya TZS 120. 45 milioni sawa na asilimia 100 za makadirio kwa kazi za kawaida na TZS 399.8 milioni sawa na asilimia 28.9 kwa kazi za Maendeleo na kuweza kutekeleza yafuatayo:

i) Kushiriki mikutano mitano (5) ya kimataifa na mikutano na washirika mbali mbali iliyofanyika nje ya Nchi kwa lengo la kuendeleza mashirikiano na Washirika wa Maendeleo;

ii) Kushiriki mikutano11 ya Taasisi za Serikali na minne (4) ya sekta binafsi ambayo imefanyika kufuatilia taarifa za misaada na utekelezaji wake;

iii) Kuwapatia mafunzo wafanyakazi wanane (8) wa Idara katika fani ya ukusanyaji na uchambuzi wa taarifa za misaada.31. Mheshimiwa Spika, Katika mwaka wa fedha 2013/2014 Idara inaombewa jumla ya TZS 94.5 milioni kwa kazi za kawaida na TZS 995.03 milioni kwa kutekeleza Mradi wa Kuimarisha Utawala Bora Awamu ya Pili na TZS 494.45 milioni kwa Mradi wa Kuimarisha Usimamizi wa Misaada Zanzibar. Shughuli nyengine zitakazofanyika ni pamoja na:

i) Kuimarisha upatikanaji wa rasilimali itakayofikia TZS 235,411 milioni kutoka kwa Washirika wa Maendeleo, kupitia programu na miradi mbali mbali ya maendeleo. Kati ya fedha hizo TZS 148,614.0 milioni zinatarajiwa kupatikana kupitia mikopo na TZS 86,797.0 milioni ni ruzuku. Misaada ya kibajeti (GBS) inatarajiwa kufikia TZS 40,000.00 milioni kwa mwaka 2013/2014. Kati ya fedha hizo, TZS 26,500.0 milioni zitatokana na ruzuku na TZS 13,500.0 milioni zitatokana na mikopo ya kibajeti. Aidha, Serikali inatarajiwa kupata TZS 2,510.00 milioni kupitia Fedha za Msamaha wa Madeni (MDRI);

ii) Kufuatilia na kufanya uchambuzi wa taarifa za misaada;

iii) Kuimarisha ushirikiano na uratibu wa misaada baina ya Washirika wa Maendeleo pamoja na Mashirika na Taasisi za Serikali.B.4 IDARA YA UHAKIKIMALI NA MITAJI YA UMMA

32. Mheshimiwa Spika, Jukumu kubwa la Idara hii ni kusimamia Mali za Serikali hasa katika manunuzi na uuzaji pamoja na Mitaji ya Umma. Kwa mwaka 2012/2013 Idara ilitengewa jumla ya TZS 287.2 milioni kwa kazi za kawaida, ambapo mpaka kufikia mwishoni mwa mwezi Juni 2013 jumla ya TZS 287.2 milloni ziliweza kupatikana sawa na asilimia 100 ya makadirio. Aidha, kwa kazi za maendeleo jumla ya TZS 6,000.00 millioni zilitengwa kwa kazi za ujenzi wa Ofisi za Serikali na uhakiki wa mali za Serikali, ambapo jumla ya TZS 3,300.00 milioni sawa na asilimia 55 ziliweza kupatikana. Fedha zote hizi zilitumika katika kutekeleza yafuatayo:

i) Kusimamia ukamilishaji wa Daftari la Mali za Serikali kwa Wizara tano (5); za Miundombinu na Mawasiliano, (OR) Fedha, Uchumi na Mipango ya Maendeleo, Ardhi, Makaazi, Maji na Nishati, Afya na Elimu na Mafunzo ya Amali;

ii) Kufanya ukaguzi wa manunuzi katika Wizara 14 na taasisi zake kwa mwaka 2012/13 sambamba na kuhakiki Mali za serikali;

iii) Kusimamia Mitaji ya Serikali ambapo jumla ya TZS 401.50 millioni zilikusanywa kutoka vyanzo vya mapato vifuatavyo: Mashamba ya Mipira, Kodi katika nyumba ya Afrika House na ukodishwaji wa matangi ya mafuta;

iv) Kutoa mafunzo ya Manunuzi na Uondoshaji wa Mali za Serikali kwa Wizara ya Katiba na Sheria, Mashirika ya Bima, Utalii na Meli ili taasisi hizo ziweze kufanya manunuzi ya vifaa vyao kama Sheria za manunuzi zinavyoelekeza;

v) Kutoa mafunzo ya siku tatu (3) kwa Wahakikimali wa Wizara za Serikali ili kuweza kupata taaluma na njia sahihi za ukaguzi wa manunuzi na Mali za Serikali;

vi) Kufanya tathmini ya utendaji, masoko, muundo na mitaji kwa Mashirika manne (4) ya Serikali likiwemo Shirika la Meli, Utalii, Bima na Magari. Kwa ujumla Shirika la Magari na Utalii yameonekana kutofanya vizuri katika biashara zao;

vii) Kufanya uchanganuzi wa hesabu za mwaka 2010/11 kwa Shirika la Bima, Bandari, ZSTC na PBZ yameonesha kutengeneza faida katika biashara zao, kwa ujumla yameweza kulipia Serikalini gawio la faida la jumla ya TZS 400.00 millioni;

viii) Kuratibu na kusimamia ujenzi wa Ofisi za Serikali katika Wizara ya Katiba na Sheria na kwa sasa ujenzi umeshafikia ghorofa ya tano (5) kati ya ghorofa nane.33. Mheshimiwa Spika, Kwa mwaka 2013/2014, Idara inaombewa jumla ya TZS 502.70 millioni kwa kazi za kawaida na TZS 7,500.00 milioni kwa kutekeleza miradi miwili ya maendeleo. Malengo yaliyopangwa kutekelezwa ni pamoja na yafuatayo:

i) Kuendelea kusimamia na kutathmini Mashirika, Mitaji kwa viwanda vya ZAPOCO, Kiwanda cha Sukari na Manukato - Mahonda, Cocacola na Hisa za Serikali zikiwemo ZANTEL na Benki ya Posta;

ii) Kufatilia taratibu za manunuzi pamoja na uhakiki wa Mali za Serikali kwa Wizara 16 na Taasisi zake kwa mwaka 2012/2013;

iii) Kuendeleza tathmini ya Mali za Serikali kwa wizara tatu (3) Wizara ya Kazi, Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi na Ushirika, Katiba na Sheria, Ustawi wa Jamii, Maendeleo ya Vijana, Wanawake na Watoto;

iv) Kuendelea kuifanyia mapitio Sheria namba 9 ya Manunuzi ya mwaka 2005;

v) Kuwajengea uwezo watendaji watano (5) wa Idara katika masuala ya usimamizi wa Mitaji na Mali za Serikali;

vi) Kuandaa miongozo ya manunuzi (Procurement Guidelines) pamoja na kuwapatia mafunzo watendaji wote wa Idara juu ya taaluma hiyo.C. IDARA ZA URATIBU NA UTAWALA

34. Mheshimiwa Spika, Ofisi ya Rais Fedha Uchumi na Mipango ya Maendeleo inasimamia pia shughuli za Uratibu na Utawala kupitia Idara zake nne (4) ambazo ni Idara ya Uendeshaji na Utumishi, Idara ya Mipango, Sera na Utafiti, Ofisi Kuu ya Pemba na Idara ya Uratibu wa shughuli za SMZ Dar es Salaam.C.1 IDARA YA UENDESHAJI NA UTUMISHI

35. Mheshimiwa Spika, Jukumu kubwa la Idara hii ni kusimamia masuala yote ya utendaji na Utumishi ndani ya Ofisi ya Raisi fedha, Uchumi na Mipango ya Maendeleo. Idara hii kwa mwaka 2012/13, iliidhinishiwa jumla ya TZS 16,127.49 milioni kwa ajili ya kazi za kawaida, ambapo mpaka kufikia mwezi Juni 2013 ilishatumia jumla ya TZS 16,127.49 milioni sawa na asilimia 100 ya makadiro. Matumizi haya yalifanyika katika kutekeleza mambo yafuatayo:

i) Kuimarisha uwezo wa wafanyakazi wa Wizara kwa kuwapatia watendaji 65 mafunzo ya muda mrefu katika vyuo mbali mbali vya Tanzania katika fani za uhasibu, ununuzi na ugavi, teknolijia ya Habari, fedha, uchumi na rasilimali watu;

ii) Kuwapatia watendaji 90 mafunzo ya muda mfupi ndani na nje ya nchi;

iii) Kusimamia na kugharamia vikao 15 vya Bodi ya Zabuni na vikao vyengine mbali mbali vya uongozi wa Ofisi;

iv) Kusimamia ukarabati na ujenzi wa Ofisi Pemba ambapo tayari Ofisi imekamilisha michoro kwa ajili ya ujenzi wa jengo litakalotumiwa na Ofisi ya Rais Fedha, Uchumi na Mipango ya Maendeleo; Kazi, Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi na Ushirika pamoja na Wizara ya Ustawi wa Jamii, Maendeleo ya Vijana, Wanawake na Watoto;

v) Kuwapatia wafanyakazi 150 likizo zao pale walipostahiki;

vi) Kuwahudumia viongozi wakuu wa Serikali katika safari zao za ndani na nje ya nchi;

vii) Kuendelea na udhamini wa wanafunzi 1,377 katika vyuo mbalimbali nchini Tanzania katika fani za Uchumi, Fedha, Uhasibu, Manunuzi na Ugavi pamoja na Teknolojia ya Habari.36. Mheshimiwa Spika, Kwa mwaka wa fedha 2013/2014, Idara inaombewa jumla ya TZS 3,962.35 milioni ili kutekeleza majukumu yafuatayo:

i) Kuwajengea uwezo wa kiutendaji wafanyakazi 85 wa Ofisi ya Rais Fedha, Uchumi na Mipango ya Maendeleo kwa kuwapatia mafunzo ya muda mrefu na mfupi katika fani zinazohusiana na majukumu ya Ofisi;

ii) Kuwapatia likizo za mwaka watendaji 200;

iii) Kwa kushirikiana na Wizara husika, kusimamia kuanza rasmi ujenzi wa jengo la Ofisi huko Pemba kwa ajili ya Ofisi za Wizara tatu;

iv) Kuwapatia udhamini wanafunzi 1,000 katika vyuo mbali mbali kwa fani zinazohitajika na Wizara ambapo Wanafunzi 634 wanaendelea na masomo na Wanafunzi 366 wataanza mwaka wa masomo 2013/2014;

v) Kuandaa mafunzo ya ndani kwa wafanyakazi 50 kwa lengo la kuielewa vizuri Sheria mpya Namba 2 ya Utumishi wa Umma;

vi) Kuratibu shughuli za ukaguzi wa hesabu na utendaji wa Wizara;

vii) Kuendeleza mazingira bora ya kazi na huduma za kiutawala kwa kuwapatia watendaji vitendea kazi na maeneo bora ya kazi.C.2 IDARA YA MIPANGO, SERA NA UTAFITI

37. Mheshimiwa Spika, Kwa mwaka 2012/13, Idara ilikadiriwa kutumia TZS 134.19 milioni kwa ajili ya kazi za kawaida na TZS 20,504.69 milioni kwa ajili ya kazi za Maendeleo. Hadi kufikia Juni 30 mwaka 2013 Idara ilitumia TZS 134.19 milioni sawa na asilimia 100ya makadirio kwa kazi za kawaida na TZS 2,465.0 milioni sawa na asilimia 12 kwa kazi za maendeleo.38. Mheshimiwa Spika, Kwa mwaka 2012/13 Idara imeweza kutekeleza kazi zifuatazo:

i) Kuratibu utekelezaji wa majukumu ya Ofisi na kuandaa Ripoti mbali mbali za utekelezaji;

ii) Kusimamia maandalizi ya bajeti ya Wizara mwaka 2013/2014;

iii) Kuandaa warsha mbili za kuhamasisha wafanyakazi kuhusiana na masuala ya mtambuka;

iv) Kuratibu maandalizi ya Sera na Mkakati wa Sekta ndogondogo za Fedha pamoja na kukamilisha marekebisho ya sheria ya ZSSF na ZIPA;

v) Kufuatilia na kutathmini utekelezaji wa miradi inayosimamiwa na Ofisi;

vi) Kushiriki katika mikutano minne (4) huko Tanzania Bara iliyojadili mageuzi ya sekta ya fedha na uimarishaji wa Sekta ndogo ndogo za fedha nchini;

vii) Kutayarisha hadidu rejea za kumpata Mshauri elekezi kwa ajili ya kuandaa Mpango mkakati na Muongozo wa Utekelezaji wa Programu ya Mageuzi katika Usimamizi wa Fedha za Umma;

viii) Kukamilisha ununuzi magari 17, piki piki 32, vifaa vya kukusanyia taka 1000 pamoja na kukamilisha Ripoti tatu (3) za ushauri kwa mradi wa Uimarishaji Huduma za Kijamii Mijini (ZUSP).39. Mheshimiwa Spika, Kwa mwaka 2013/14, Idara inaombewa jumla ya TZS 285.30 milioni kwa kazi za kawaida na TZS 1,250.00 milioni kwa kazi za Maendeleo. Aidha Idara itaratibu matumizi ya TZS 17,000.00 milioni kwa ununuzi wa meli ya Serikali. Kazi zilizopangwa kutekelezwa ni pamoja na hizi zifuatazo:

i) Kuiimarisha na kuipanua sekta ya fedha ili iweze kuchangia zaidi uchumi wa Zanzibar kwa kuandaa Sera, Mkakati na Mpango kazi wa utekelezaji;

ii) Kukamilisha Sera ya Taasisi ndogondogo za kifedha;iii) Kuratibu mapitio ya Mipango, Sera na Sheria za ZSSF, ZIPA, Sheria za Fedha za Umma na Sheria ya Manunuzi ndani ya Wizara na Taasisi zake;

iv) Kuratibu utayarishaji wa ripoti za robo, nusu na mwaka pamoja na Bajeti ya Wizara;

v) Kuhamasisha na kushajihisha masuala Mtambuka katika Wizara na taasisi zake;

vi) Kuratibu na kusimamia utendaji wa Bodi na Baraza la Rufaa ya Kodi kwa ajili ya kutatua migogoro ya walipa kodi;

vii) Kuwajengea uwezo na kuandaa mazingira bora kwa wafanyakazi wa Idara ikiwemo mafunzo maalum juu ya Uchambuzi wa Sera, uandaaji wa tafiti na tathmini ya sekta ya fedha nchini;

viii) Kuratibu ununuzi wa meli mpya ya abiria na mizigo ya Serikali;

ix) Kuratibu miradi ya Wizara ikijumuisha utayarishaji wa Mpango Mkuu wa Maeneo Huru Fumba, mradi wa kuimarisha Huduma za Miji Unguja na Pemba, mradi wa Ujenzi wa Maabara ya komputa (ZIFA), Programu ya Usimamizi wa Mageuzi ya Fedha za Umma (PFMRP) na mradi wa Kuimarisha Utawala Bora Awamu ya Pili.C.3 OFISI KUU - PEMBA

40. Mheshimiwa Spika, Ofisi Kuu Pemba ambayo inatekeleza shughuli za Ofisi kwa upande wa Pemba. kwa mwaka wa fedha wa 2012/2013 iliidhinishiwa jumla ya TZS 663.48 milioni kwa kazi za kawaida, ambapo mpaka kufikia mwezi Juni 2013, Ofisi ilishapatiwa jumla ya TZS 663.48 milioni sawa na asilimia 100 ya makadirio. Shughuli zilizofanywa katika utekelezaji wa majukumu hayo ni kama zifuatazo:

i) Kuweka mazingira mazuri ya kazi na kuongeza ufanisi bora;

ii) Kulipia gharama mbali mbali za uendeshaji wa Ofisi na huduma;

iii) Kuimarisha huduma za mtandao wa IFMS;

iv) Kuratibu upatikanaji wa mafunzo kwa wafanyakazi katika fani mbali mbali, ambapo jumla ya wafanyakazi 21 wakiwemo wanawake 6 na wanaume 15 walipatiwa mafunzo ikiwemo shahada ya uzamili ya usimamizi wa fedha (7); shahada ya uzamili ya uhasibu (6 ); shahada ya kwanza ya uhasibu (5 ) shahada ya kwanza ya Ununuzi na Ugavi (2); na shahada ya kwanza ya masoko ( 1);

v) Kuratibu shughuli za manunuzi ya vifaa na huduma katika Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali, Wizara ya Afya, Wizara ya Biashara Viwanda na Masoko na Baraza la Mji la Chake Chake;

vi) Kufanya ukaguzi na uhakiki wa mali za Serikali katika Wizara ya Afya, Ofisi ya Rais na MBLM, Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Ofisi za Wakuu wa Mikoa, Ofisi za wakuu wa Wilaya ikiwemo wilaya ndogo ya Kojani;

vii) Kutoa mafunzo kwa maofisa Mipango 24 wa Wizara zote juu ya utayarishaji na uimarishaji wa Daftari la Mali za Kudumu za Serikali (Fixed Assets Register);

viii) Kutoa mafunzo kwa Wahasibu na Wakaguzi wa ndani wa hesabu za Serikali 22 juu ya Sheria ya Fedha Nam. 5 ya 2005, pamoja na kuwajengea uwezo wa kazi zao juu ya matumizi ya mtandao wa IFMS kwa lengo la kuimarisha shughuli za uhasibu Serikalini;

ix) Kufanya ukaguzi wa shughuli za kiuhasibu pamoja na ukusanyaji wa mapato katika Wizara na Taasisi zote za Serikali;

x) Kuratibu utoaji wa mafunzo kwa maofisa Mipango 24 wa Wizara zote, Mikoa na Wilaya zote kwa upande wa Pemba juu ya upangaji wa mipango na bajeti inayozingatia malengo ya MKUZA II;

xi) Kuratibu mafunzo kwa Kamati za Shehia 62 katika Mkoa wa Kusini Pemba kwa ajili ya uwekaji kumbukumbu za Shehia;

xii) Kuwapatia mafunzo wafanyakazi wote wa Ofisi kuu Pemba masuala ya Shughuli Mtambuka;

xiii) Kuratibu utekelezaji wa miradi ya Maendeleo kwa upande wa Pemba.41. Mheshimiwa Spika, Kwa mwaka wa fedha wa 2013/2014 Ofisi ya Pemba inaombewa jumla ya TZS 825.075 milioni ili kutekeleza majukumu yafuatayo:

i) Kuandaa mazingira bora ya kazi na kuleta ufanisi na huduma bora katika kazi;

ii) Kufanya uhakiki wa mali za Serikali na kufanya ukaguzi wa manunuzi katika Wizara na Taasisi zote za Serikali zilizopo Pemba;iii) Kusimamia na kuimarisha shughuli za uhasibu Serikalini kwa upande wa Pemba;

iv) Kuratibu utekelezaji wa miradi ya kitaifa Pemba na kusimamia utekelezaji wa mipango na bajeti za Wizara na Taasisi zake;

v) Kuratibu shughuli za rasilimali watu pamoja na kuimarisha mfumo wa uwekaji wa kumbukumbu na kuendeleza shughuli Mtambuka (Cross Cutting Issues);

vi) Kuendelea kuratibu upatikanaji wa nafasi zaidi za masomo kwa wafanyakazi wake katika ngazi na fani mbali mbali;

vii) Kushirikiana na Idara ya Uendeshaji na Utumishi kuanza rasmi ujenzi wa Ofisi mpya Pemba;

viii) Kusimamia, kuendeleza na kudhibiti fedha za umma ikiwemo ukusanyaji wa mapato na matumizi ya fedha na mali za serikali na taasisi zake pamoja na kutoa huduma za uhasibu na ukaguzi;ix) Kuwapatia mafunzo na kuwaweka tayari watumiaji wapya wa mtandao wa IFMs kwa Wizara na Taasisi za Serikali, Ufuatiliaji na upatikanaji wa hati za Serikali (Counterfoils);

x) Kufuatilia uwekaji wa kumbukumbu katika madaftari ya Shehia kwa Wilaya zote. Kufanya mjadala na wadau juu ya umuhimu wa “ Vital registration“ na ukusanyaji wa takwimu zinazozingatia masuala ya idadi ya watu;

xi) Kuratibu mafunzo ya kushajihisha uingizaji wa masuala ya idadi ya watu katika mipango ya asasi za Serikali.C.4 IDARA YA URATIBU WA SHUGHULI ZA SMZ DAR ES SALAAM

42. Mheshimiwa Spika, Kwa mwaka wa fedha 2012/13 Idara iliidhinishiwa kutumia TZS 212.58 milioni kwa kazi za kawaida ambapo shughuli kubwa za Idara ni kutekeleza shughuli za Uratibu kati ya Zanzibar na Tanzania Bara na nje ya Tanzania. Mpaka mwisho wa mwezi Juni 2013 Idara ilishatumia jumla yaTZS 212.58 milioni, sawa na asilimia 100 ya makadirio. Katika kufanikisha malengo yake, Idara ilitekeleza yafuatayo:

i) Kuratibu na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa Korea Institute for Development Strategy (KIDS) kuhusiana na mpango mpya wa mafunzo ambao umeandaliwa na Taasisi hiyo kwa nchi tatu za Afrika ikiwemo Tanzania;

ii) Kushiriki katika ziara ya Mhe. Rais Jakaya M. Kikwete nchini Oman ambapo mikataba mbalimbali ilisainiwa ukiwemo mkataba wa Elimu ya juu uliosainiwa na Mhe.Waziri wa Elimu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar;

iii) Kushiriki katika mkutano wa Tume ya Ushirikiano baina ya Tanzania na Kenya ambapo masuala ya kiuchumi, Utawala, Ulinzi na Jamii yalizungumziwa;iv) Kuratibu mazungumzo baina ya Waziri wa Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo na Balozi za Rwanda na Wawakilishi wa Jumuiya ya Wafanyabiashara wa China pamoja na Jumuiya ya wafanyabiashara wa Zanzibar, lengo likiwa ni kuzungumzia mashirikiano ya kukuza utalii baina ya nchi zetu;

v) Kushiriki katika warsha ilioyoandaliwa na Jumuiya ya Ulaya (EU) kuhusiana na upembuzi yakinifu na mapendekezo mengine kwa ajili ya kutekeleza mkakati wa ufadhili wa Umoja wa Ulaya wa kuwepo kwa Ofisi ya Ofisa Mamlaka ya Taifa (National Authorizing Officer - NAO) ambaye ni kiunganishi kikuu baina ya Miradi na Washirika wa Maendeleo;

vi) Kushiriki kwenye kikao cha matayarisho ya mkutano wa Biashara ya huduma kwa nchi za SADC, ambapo kwa upande wa Zanzibar mkazo ni kuimarisha Sekta ya Utalii;vii) Kushiriki vikao vya maandalizi ya mkutano wa watendaji wakuu, kuhusiana na Umoja wa Fedha wa Jumuiya ya Afrika Mashariki;

viii) Kuratibu upatikanaji wa nafasi za mafunzo na kushiriki katika vikao vya uteuzi ambapo wafanyakazi kumi na tano (15) kutoka Zanzibar walichaguliwa kujiunga na masomo katika fani na viwango mbali mbali kwa mwaka wa masomo 2013/2014 katika nchi za Algeria, Uingereza na China.43. Mheshimiwa Spika, Kwa mwaka wa fedha 2013/2014, Idara inaombewa jumla ya TZS 326.97 milioni ili kutekeleza majukumu yafuatayo:

i) Kuratibu na kukuza ushirikiano baina ya Taasisi za Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na zile za Serikali ya Jamhuri ya Muungano;

ii) Kuratibu ushirikiano wa kiuchumi na kimaendeleo baina ya SMZ na Ofisi za Balozi za nje na mashirika ya Maendeleo yaliyo na Ofisi zake Dar es Salaam;iii) Kushiriki katika mikutano mbali mbali ya kiuchumi na kijamii inayoandaliwa na SMT kwa faida ya Serikali;

iv) Kuratibu upatikanaji wa nafasi za mafunzo kutoka nchi rafiki na Mashirika ya Kimataifa.D. TAASISI ZA FEDHA ZINAZOJITEGEMEA

44. Mheshimiwa Spika, Ofisi ya Rais Fedha, Uchumi na Mipango ya Maendeleo inasimamia taasisi tisa (9) zinazojitegemea ambazo zinajumuisha Bodi ya Mapato Zanzibar, Mamlaka ya Mapato Tanzania - Zanzibar, Mfuko wa Barabara, Mamlaka ya Ukuzaji wa Vitega Uchumi, Chuo cha Uongozi wa Fedha Chwaka, Shirika la Bima Zanzibar, Mfuko wa Hifadhi ya Jamii, Benki ya Watu wa Zanzibar na Ofisi ya Mtakwimu MKuu wa serikali ambayo iko chini ya Tume ya Mipango.D1. BODI YA MAPATO ZANZIBAR (ZRB)

45. Mheshimiwa Spika, Bodi ya Mapato Zanzibar ni miongoni mwa Taasisi iliyopewa jukumu la kukusanya mapato ya ndani kwa ajili ya matumizi ya Serikali. Kwa mwaka 2012/2013, Bodi ya Mapato ya Zanzibar (ZRB) ilipangiwa kukusanya jumla ya TZS 162,000.0 milioni, ambapo mpaka kufikia mwishoni mwa mwezi Juni 2013, makusanyo halisi yalifika jumla ya TZS 141,708.0 milioni sawa na asilimia 87 ya makadirio. Pamoja na kutofikia lengo, mapato kutoka ZRB yamekuwa kwa asilimia 17.6 ikilinganishwa na kiasi cha TZS 120,500 milioni zilizokusanywa 2011/2012. Kwa mwaka 2012/1013 Bodi imeweza kufanya yafuatayo:

i) Kusajili walipa kodi 687 wakiwemo 575 kwa ajili ya ushuru wa stempu, 34 kwa ajili ya kodi ya ongezeko la thamani, 32 watembezaji wageni na 46 kwa ajili ya mikahawa na kodi za Hoteli;

ii) Kutoa elimu kwa walipa kodi kwa kuendesha semina nane (8), vipindi vya Redio na mikutano saba (7) juu ya umuhimu wa kutoa Stakabadhi wanapofanya mauzo;

iii) Kufanya mapitio ya idadi ya Hoteli na viwango vinavyotumika kutoza kodi kwa Hoteli mbali mbali ziliyopo Zanzibar na kufanya marekebisho katika Sheria ya Kodi ya Ongezeko la Thamani na Sheria ya Ushuru wa Hoteli;

iv) Kuchukua hatua za kukabiliana na magendo ya mafuta kwa kutoa elimu kwa Jamii, kufanya mikutano ya wauzaji wa jumla na rejereja na kufanya zoezi maalum la kukamata mafuta ya magendo kwa kushirikiana na vyombo vya Ulinzi na Usalama ambapo lita 32,732 za diseli zilikamatwa.46. Mheshimiwa Spika, Kwa mwaka wa fedha wa 2013/2014, Bodi ya Mapato imekadiria kukusanya jumla ya TZS 171,700.0 milioni sawa na ongezeko la asilimia 21 ikilinganishwa na makusanyo halisi ya mwaka 2012/2013. Ili kufikia lengo hili, ZRB imepanga kuchukua hatua zifuatazo:

i) Kutekeleza hatua mbali mbali na kuimarisha mapato kama zilivyotangazwa na Serikali;

ii) Kufanya ukaguzi kwa walipa kodi;

iii) Kuwaongezea uwezo wa kiutendaji wafanyakazi 65 kwa kuwapatia mafunzo maalum katika utozaji kodi kwenye sekta za Utalii, simu, mawasiliano na mafuta;

iv) Kupitia mfumo wa mapato ya Mawizara;

v) Kuvipitia viwango mbalimbali vya kulipia kodi.

47. Mheshimiwa Spika, Bodi ya Mapato inaombewa ruzuku ya TZS 8,410.00 milioni kwa matumizi ya kazi za kawaida kwa mwaka wa fedha 2013/2014 ili kutekeleza majukumu yake. Hii ni sawa na ongezeko la asilimia 15 kutoka ruzuku ya TZS 7,296 milioni waliyopatiwa mwaka 2012 /2013.D2. MAMLAKA YA MAPATO TANZANIA (TRA)

48. Mheshimiwa Spika, Katika mwaka wa fedha wa 2012/2013 Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Ofisi ya Zanzibar ambayo jukumu lake kubwa ni kukusanya mapato ya Muungano kwa upende wa Zanzibar, ilipangiwa kukusanya jumla ya TZS 106,730.4 milioni. Katika kufikia lengo hilo, Idara ya Forodha na Ushuru wa bidhaa ilipangiwa kukusanya jumla ya TZS 67,077milioni sawa na asilimia 63 ya lengo la mwaka na Idara ya Kodi za Ndani ilipangiwa kukusanya kiwango kilichobaki cha TZS 39,653.4 milioni sawa na asilimia 37 ya lengo la mwaka.49. Mheshimiwa Spika, TRA Zanzibar ilimudu kukusanya TZS 103,865.69 milioni sawa na asilimia 97 ya lengo. Utekelezaji huu unamaanisha ukuaji wa mapato kwa asilimia 13 kutoka TZS 91,666.4 milioni zilizokusanywa mwaka 2011/2012. Kati ya Fedha zilizokusanywa, Idara ya Forodha iliweza kukusanya TZS 63,822.00 milioni sawa na asilimia 95 ya lengo au asilimia 61 ya mapato yote yaliyokusanywa na TRA Ofisi ya Zanzibar. Idara ya Kodi za ndani imemudu kukusanya TZS 40,043.69 milioni zaidi ya asilimia 100 ya lengo lake au asilimia 39 ya mapato yote yaliyokusanywa.50. Mheshimiwa Spika, Kwa mwaka wa fedha wa 2013/2014, Mamlaka ya Mapato (TRA) – Ofisi ya Zanzibar imepangiwa kukusanya TZS 147,900.00 milioni sawa na ongezeko la asilimia 42.4 ya mapato halisi yaliyokusanywa kwa mwaka 2012/2013. Kati ya lengo hilo, Idara ya Forodha na Ushuru inatarajiwa kukusanya jumla ya TZS 98,792 milioni sawa na asilimia 67 ya makadirio na Idara ya kodi za ndani inatarajiwa kukusanya TZS 49,107 milioni sawa na asilimia 33 ya makadirio.D3. MFUKO WA BARABARA

51. Mheshimiwa Spika, Jukumu kubwa la Mfuko wa Barabara ni kusimamia matengenezo ya barabara zetu. Kwa mwaka wa fedha wa 2012/13 Mfuko wa Barabara ulilenga kupokea Ruzuku ya jumla ya TZS 5,868 milioni kwa kazi za barabara na Uendeshaji wa Mfuko. Hadi kufikia tarehe 30 Juni 2013, jumla ya TZS 5,868.0 millioni walishapokea, Ruzuku ambayo ni sawa na asilimia 100 ya makadirio ya mwaka.52. Mheshimiwa Spika, Katika mwaka 2012/13 Mfuko ulipanga kutumia jumla ya TZS 6,320.0 milioni kwa kazi ya matengenezo ya barabara na Uendeshaji wa Mfuko, ambapo mpaka kufikia Juni 30, 2013 jumla ya TZS 4,222.00 milioni zilitumika sawa na asilimia 67 ya makadirio ya mwaka. Kati ya matumizi hayo jumla ya TZS 3,520.00 milioni zililipwa kwa kazi za barabara zikiwa ni asilimia 63 ya makadirio ya TZS 5,551 milioni. Vile vile, jumla ya TZS 702.00 milioni zilitumika kwa kazi za Uendeshaji wa Mfuko zikiwa ni asilimia 91 ya makadirio ya TZS 769 milioni. Aidha, kazi zenye thamani ya TZS 1,800.00 millioni bado zinaendelea kutekelezwa na malipo yake yatafanyika mara kazi hizo zitakapokamilika.53. Mheshimiwa Spika, Katika mwaka wa fedha wa 2012/13 Mfuko uliweza kukamilisha majukumu mbali mbali uliojipangia yakiwemo:

i) Ufungaji wa hesabu za mwaka 2011/12 na kukamilisha ukaguzi wa Fedha na Ufundi kwa mwaka 2011/12 kwa wakati uliopangwa;

ii) Kuandaa Ripoti ya mwaka 2011/12;

iii) Ununuzi wa gari ya ofisi kwa ajili ya ukaguzi wa kazi na majukumu mengine;

iv) Ununuzi wa generata la ofisi kwa matumizi ya dharura;

v) Kumpatia mafunzo ya shahada ya juu mfanyakazi mmoja pamoja na mafunzo ya cheti kwa mfanyakazi mwengine;

vi) Kuendesha semina tatu kwa wadau mbali mbali kuhusu kazi za Mfuko wa Barabara na majukumu ya Taasisi nyengine katika utunzaji wa barabara;

vii) Kutoa mafunzo ya usimamizi na utekelezaji wa kazi za matengenezo ya barabara.54. Mheshimiwa Spika, Kwa mwaka wa fedha wa 2013/14 Mfuko wa Barabara utaendelea na jukumu lake la kuweka utaratibu madhubuti wa utunzaji wa fedha zinazokusanywa kwa ajili ya kuzifanyia matengenezo ya barabara pamoja na kuhakikisha kuwa fedha hizo zinatumika kwa ufanisi na kwa lengo lililokusudiwa. Kwa mwaka 2013/2014, Mfuko wa Barabara unaombewa Ruzuku ya jumla ya TZS 6,903 milioni. Kati ya fedha hizo, TZS 6,046 milion ni kwa ajili ya matengenezo ya barabara na TZS 857.0 milioni kwa ajili ya uendeshaji wa Ofisi.D.4 MAMLAKA YA UKUZAJI VITEGA UCHUMI ZANZIBAR (ZIPA)

55. Mheshimiwa Spika, Jukumu kubwa la Mamlaka hii ni kushajihisha wawekezaji wa nje na ndani kuekeza nchini pamoja na kuwasaidia wawekezaji kufikia malengo yao ya uwekezaji. Kwa mwaka wa fedha wa 2012/2013, ZIPA ilipangiwa kuwavutia wawekezaji miradi wapatao 38 katika sekta mbalimbali za kiuchumi, kijamii na viwanda. Aidha ZIPA ilipanga kukusanya kutoka vyanzo vyake vya mapato jumla ya TZS 1,754.16 milioni na kupatiwa ruzuku kutoka Serikalini ya TZS 300.00 milioni na kufanya jumla ya matumizi yao kufikia TZS 2,054.16 milioni. Hadi kufikia Juni 2013, ZIPA imeweza kukusanya jumla ya TZS 1,058.97 milioni sawa na asilimia 60.4 ya makadirio kutoka katika vyanzo vyake na kupatiwa asilimia 100 ya ruzuku yote iliyopangiwa na Serikali.56. Mheshimiwa Spika, Katika kutekeleza majukumu yake, Mamlaka iliweza kukamilisha kazi zifuatazo:

i) Miradi 30 iliidhinishwa yenye mtaji wa USD 335,428,485.67;

ii) Mamlaka imetangaza fursa za uwekezaji kwa kushiriki katika Mkutano wa Maonyesho ya Biashara nchini Korea na Mkutano wa EPA nchini Ubelgiji;

iii) ZIPA imeshiriki mikutano miwili ya Kanda nchini Msumbiji na Ethiopia. Mikutano mengine iliyoshiriki ni pamoja na nchi za Geneva, Oman, Kigali, Afrika ya Kusini na Dubai pamoja na mikutano ya ndani ya Dar Es Salaam na Arusha. ZIPA pia imeweza kujitangaza nchini China kupitia ziara ya Mhe.Rais wa Zanzibar;

iv) Kukamilisha ujenzi wa barabara kiwango cha lami kwa sehemu ya nje na sehemu ya ndani kiwango cha kifusi na kuweka taa za usalama kwenye eneo la Maruhubi;

v) Kuanza matayarisho ya Utayarishaji wa “Master Plan” ya eneo la Fumba;

vi) Kukamilisha michoro ya Ujenzi wa Ofisi ya ZIPA Pemba;

vii) Kuratibu shughuli zote za uwekezaji kwa upande wa Pemba ikiwepo ukaguzi wa miradi mipya na ya zamani iliyoekezwa Pemba;

viii) Wafanyakazi wanane (8) wameshiriki mafunzo ya muda mfupi, sita (6) wanaendelea na mafunzo ya muda mrefu kati yao watatu (3) wanaendelea na mafunzo ya Shahada ya kwanza, wawili (2) shahada ya pili na mmoja (1) Stashahada.57. Mheshimiwa Spika, Kwa mwaka 2013/2014, ZIPA inakusudia kukusanya jumla ya TZS 1,622.79 milioni kutoka katika vyanzo vyake vya ndani na kupatiwa ruzuku ya TZS 300.00 milioni. Aidha ZIPA imekadiria kupata jumla ya TZS 2,295.39 milioni kutoka kwa wawekezaji mbali kwa njia ya misaada ili kutimiza mahitaji ya TZS 3,918.18 milioni kwa kufanikisha utekelezaji wa shughuli za Kawaida na Maendeleo. Katika hilo, Serikali imepanga kuipatia ZIPA jumla ya TZS 450.00 milioni kwa ajili ya uendelezaji wa Maeneo Huru. Katika kukamilisha malengo yake, ZIPA imepanga kutekeleza kazi zifuatazo:

i) Kufanya utafiti ili kutambua fursa mpya za uwekezaji na zilizopo, ifikapo mwisho wa mwaka 2013/2014;

ii) Kutoa huduma za upembuzi, uchambuzi na kuidhinisha miradi mipya;

iii) Kuimarisha Tovuti ya ZIPA kwa kuingizwa habari zilizopo na za kisasa za uwekezaji;

iv) Kuvutia wawekezaji wa ndani na nje ya nchi kwa njia mbali mbali zikiwemo kusambazwa vipeperushi;

v) Kufanya semina na midahalo ya mara kwa mara ya kuvutia wawekezaji wa ndani na nje ya nchi;

vi) Kushiriki katika maonyesho ya biashara ya kikanda na kimikoa;

vii) Kukamilisha Mpango wa maendeleo ya Rasilimali watu pamoja na kuandaliwa mfumo wa kuvutia wafanyakazi kimaslahi ifikapo mwaka 2014;

viii) Kukamilisha marekebisho ya Sheria ya ZIPA kwa kushirikiana na Idara ya Mipango, Sera na Utafiti.D5. CHUO CHA UONGOZI WA FEDHA, CHWAKA ZANZIBAR

58. Mheshimiwa Spika, Chuo cha Uongozi wa Fedha (ZIFA) kina jukumu la kutoa mafunzo ya fani ya Fedha na zinazolingana, kuandaa semina za kiutawala na kutoa mafunzo ya muda mfupi katika fani maalumu. Kwa mwaka wa fedha 2012/2013, Chuo kiliweza kukusanya Mapato ya TZS 2,614.12 milioni na kuweza kutumia Mapato hayo pamoja na Ruzuku ya TZS 1,641.0 millioni iliyopatiwa na Serikali na hatimae kutekeleza shughuli zifuatazo:i) Kukusanya jumla ya TZS 2,614.12 milioni kutokana na ada za masomo, ruzuku na huduma nyengine na kutumia TZS 1,705.40 milioni kwa kazi za Kawaida na TZS 908.74 milioni kwa Kazi za Maendeleo;

ii) Kuwapatia mafunzo ya muda mfupi walimu 24;

iii) Kuendelea kujenga mahusiano ya kiutendaji baina ya Chuo na “Governing Bodies” (NACTE), NBAA, TCU na AUA zinazohusiana na masuala ya elimu;

iv) Kuratibu mitihani yote ya wanafunzi katika mihula miwili ya mwaka wa masomo 2012/2013 ambapo jumla ya wanafunzi 1,214 walitahiniwa;

v) Kufanya manunuzi ya vifaa vya kufundishia na ofisini vikiwemo viti, meza, mbao za kuandikia na vitabu vya fani mbali mbali;

vi) Kuwapatia fursa za masomo walimu sita katika Shahada ya Uzamivu (PhD) kati yao wanne wanaendelea na wawili wanatarajiwa kurudi masomoni mwaka huu wa fedha;

vii) Kumuwezesha mwalimu mmoja kwenda katika masomo ya Shahada ya Uzamili (Masters) na wafanyakazi watatu wa kada ya utawala kwenda masomo ya muda mrefu , mwalimu mmoja kufanya mitihani ya bodi ya CPA (T) na wafanyakazi watano (5) wasiokuwa walimu kushiriki katika mafuzo mafupi katika fani za udereva na mafunzo ya masjala;

viii) Kusajili na kusomesha wanafunzi 1,256 katika fani na ngazi mbali mbali;

ix) Kutoa ushauri elekezi kwa Taasisi za Serikali katika kuandaa Mpango Mkakati, Kanuni za Utumishi na Kanuni za Fedha, kufunga mahesabu n.k;

x) Kuanzisha na kuimarisha Kituo cha Ujasiriamali (Incubation Centre) kwa kuandaa Mpango Mkakati wa kituo hicho pamoja na kuimarisha shughuli za utafiti na kituo cha utafiti na uchapishaji;

xi) Kujenga ukuta wa dakhalia mpya pomoja na kutengeneza viwanja vya michezo.

59. Mheshimiwa Spika, Kwa mwaka wa fedha 2013/2014. Chuo kimekadiria kukusanya jumla ya TZS 2,675.87 milioni kutokana na ada na huduma inazozitoa na mkopo kutoka ZSSF wa TZS 800.00 milioni. Aidha Chuo kinaombewa ruzuku ya TZS 1,800.00 milioni kwa kazi za kawaida na TZS 200.00 milioni kwa Kazi za Maendeleo. Mambo yaliyopangwa kutekelezwa na Chuo ni haya yafuatayo:

i) Kufanya mapitio ya mitaala katika fani za Stashahada ya Uongozi wa Fedha-Uhasibu, Stashahada ya Ununuzi na Ugavi na Stashahada ya TEHAMA;

ii) Kuongeza idadi ya programu, ambapo mwaka huu stashahada ya uzamili ya usimamizi wa Fedha itaanzishwa;

iii) Kufanya mapitio ya programu (Self -Review Study) ili kuwa na ithibati endelevu;

iv) Kufanya manunuzi ya vifaa vya kisasa vya kufundishia, manunuzi ya vitabu vya kiada na ziada (500) na Basi la Wafanyakazi;

v) Kuwapeleka wafanyakazi kumi na mbili (12) mafunzo mafupi na ya kitaalamu pamoja na walimu thalathini na nne (34) kwenye mafunzo mafupi na ya kitaalamu ikiwemo mafunzo ya njia na mbinu bora za kufundishia, TEHAMA na utafiti;

vi) Kusajili wanafunzi wapya 830, ngazi ya Cheti, Diploma, Shahada ya kwanza na Stashahada ya Uzamili na hatimae kufundisha na kuwatahini wanafunzi 1,400 katika fani mbali mbali;

vii) Kuandaa na kufanya mahafali ya kumi (10) ya chuo ambayo wanafunzi 550 wanatarajia kuhitimu;

viii) Kuendeleza wafanyakazi wanne wa kada ya utawala kwenye mafunzo ya muda mrefu (watatu wanaendelea na mmoja mpya);

ix) Kuwawezesha walimu sita katika mafunzo ya Shahada ya Uzamivu (PhD) wanne (4) wanaendelea na wawili (2) wapya pamoja na mwalimu mmoja katika mafunzo ya muda mrefu ya Shahada ya Uzamili;

x) Kuchangia shughuli za Maendeleo kwa wanajamii ikiwemo kununua vitabu vya kusaidia shughuli za kitaaluma Skuli za Chwaka na kuendesha mafunzo ya ujasiriamali kwa wadau wa Chwaka na maeneo ya karibu;

xi) Kuendesha mafunzo sita (6) ya kuongeza uwezo wa utendaji na mihadhara miwili (2) ya kitaalamu;

xii) Kufanya tafiti mbili (2) za kitaifa juu ya bajeti na fedha (Finance and Budgeting) pamoja na mabadiliko ya zao la mwani kibiashara (commercialization of seaweed);

xiii) Kuimarisha kituo cha kuwalea wajasiriamali (Incubation Centre) pamoja na kutoa Ushauri wa Kitaalamu katika Taasisi mbali mbali za Serikali na binafsi;

xiv) Kufanya mapitio ya Mpango Mkakati wa Chuo, Kanuni za Fedha na Sheria ya Chuo;

xv) Kujenga jengo jipya la ghorofa tano kwa ajili ya Maabara ya Kompyuta, madarasa na ofisi ambapo kwa mwaka huu wa fedha ghorofa mbili zinatarajiwa kumalizika;xvi) Kuwawezesha wafanyakazi wawili kushiriki kwenye mafunzo mafupi na ya kitaalamu katika fani za Katibu muhtasi na usimanizi wa ofisi;

xvii) Kufanya matengenezo ya zahanati ya chuo na ununuzi wa vifaa vyake.D6. SHIRIKA LA BIMA LA ZANZIBAR

60. Mheshimiwa Spika, Shirika hili lina jukumu la kutoa huduma za Bima kwa ujumla. Katika mwaka wa fedha wa 2012/2013, Shirika lilikadiria kukusanya mapato kutokana na ada za Bima ya TZS 11,747.00 milioni ambapo mpaka kufikia mwezi Disemba 2012, Shirika limeweza kukusanya jumla ya TZS 10,516.00 milioni sawa na asilimia 90 ya makadirio. Kwa upande wa matumizi, Shirika lilipanga kutumia jumla ya TZS 3,391.00 milioni kwa kazi za kawaida na TZS. 1,000.0 milioni kwa kazi za Maendeleo. Hadi kufikia mwezi Disemba 2012 Shirika liliweza kutumia jumla ya TZS 3,291 milioni kwa kazi za kawaida, sawa na asilimia 97 na TZS 636.00 milioni kwa shughuli za Maendeleo, sawa na asilimia 64. Mbali ya fedha za Uendeshaji,Shirika limetumia jumla ya TZS 4,075 milioni kuwalipa wateja wa Bima waliopata ajali.61. Mheshimiwa Spika, Shirika la Bima la Zanzibar kwa kipindi kijacho cha mwaka wa fedha 2013 hadi kufikia Disemba linakadiria kukusanya jumla ya TZS. 12,370 milioni kutokana na vianzio vyake mbali mbali vya mapato. Makadirio haya ya mapato ni zaidi ya mapato halisi ya mwaka 2012 uliopita kwa asilimia 18. Aidha, Shirika linatarajiwa kutumia jumla ya TZS 3,854 milioni kwa kazi za kawaida na TZS 692.0 milioni kwa kazi za Maendeleo. Kutokana na hali ya ushindani wa kibiashara kwa mwaka 2013 Shirika limejiwekea kutekeleza yafuatayo:

i) Kutumia asilimia 43 ya fedha za kazi za Maendeleo kwa ajili ya ununuzi wa vitendea kazi (magari) kwa ajili ya Kanda zilizoko Tanzania Bara;

ii) Kutoa huduma bora na za kisasa kwa wateja wake kwa kuwafatilia baada ya kupatiwa huduma na kueleza matatizo yao na kulipa madai kwa wakati;

iii) Kuongeza mapato kwa asilimia 18 kwa mwaka;

iv) Kukuza mtaji wa kutoa gawio kwa Serikali ambayo ndiyo mmiliki pekee;

v) Kuongeza wafanyakazi watano (5) wenye ujuzi na uzoefu wa kufanya kazi;

vi) Kukuza mtaji katika uwekezaji wa dhamana za Serikali na hisa;

vii) Kufanya matumizi kwa kiwango kisichozidi asilimia 20 ya mapato;

viii) Kujihusisha zaidi katika masuala ya kijamii ikiwemo utoaji wa misaada kwa vikundi vidogo vidogo na utoaji wa vyandarua katika Hospitali mbali mbali;

ix) Kuongeza kiwango cha soko kutoka asilimia 4.5 hadi asilimia 5 ifikapo 2015 ambapo kwa mwaka 2013/2014 kilifikia asilimia 4.7.D7. MFUKO WA HIFADHI YA JAMII ZANZIBAR (ZSSF)

62. Mheshimiwa Spika, Jukumu kubwa la Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar ni kukusanya michango ya wafanyakazi na kuwekeza katika miradi yenye tija na hatimae kutoa mafao kwa wanachama pale tu muda unapofikia kama Sheria ya Mfuko inavyoagiza. Kwa mwaka wa fedha 2012/2013 Mfuko umetekeleza kazi zifuatazo:

i) Kusajili waajiri 73 dhidi ya lengo la kusajili waajiri 85 hii ni sawa na asilimia 86. Wanachama waajiriwa waliosajiliwa ni 3,405 sawa na asilimia 85 ya lengo la kusajili waajiriwa 4,000;

ii) Kulipa mafao yenye jumla ya TZS 6,524 milioni sawa na asilimia 112 ya lengo lililoekwa la kulipa jumla ya TZS 5,853 milioni;

iii) Kukusanya michango ya wanachama yenye jumla ya TZS 24,756 milioni dhidi ya lengo la kukusanya TZS 24,858 milioni sawa na asilimia 99.6;iv) Kuanza ujenzi wa kiwanja cha kufurahishia watoto cha Uhuru (Kariakoo) na kuanza matayarisho ya ujenzi wa kiwanja cha kufurahishia watoto cha Umoja (Tibirinzi).63. Mheshimiwa Spika, kwa mwaka wa fedha 2013/2014 Mfuko unatarajia kufanya kazi zifuatazo:

i) Kuongeza wigo wa kusajili wanachama kwa kutumia Mfumo wa uchangiaji wa hiari (Zanzibar Voluntary Social Security Scheme) pamoja na kuimarisha ukaguzi wa Taasisi mbali mbali za binafsi;

ii) Kufanya mageuzi ili kuufanya Mfuko uwe endelevu kwa kukamilisha zoezi la mageuzi ya Sheria ya Mfuko;

iii) Kuwekeza jumla ya TZS 39,000 milioni katika maeneo ya muda mrefu na yale ya muda mfupi, zikiwemo dhamana za Serikali, hati fungani za Serikali, hesabu za muda maalum, ununuzi wa hisa pamoja na mikopo. Jumla ya TZS 18,200 milioni zinategemewa kukusanywa kama mapato ya uwekezaji;

iv) Kukamilisha ujenzi wa kiwanja cha kufurahishia watoto cha Uhuru (Kariakoo) pamoja na kuanza ujenzi wa kiwanja cha kufurahishia watoto cha Umoja (Tibirinzi);

v) Kuendelea na ujenzi wa kumbi za mikutano, nyumba za kisasa na jengo la biashara huko Mbweni;

vi) Kuwapeleka wafanyakazi 20 masomoni, kati ya hao wafanyakazi saba (7) kwa mafunzo ya muda mrefu na 13 kwa muda mfupi katika fani za Uhasibu, Ununuzi na Ugavi, TEHAMA na usimamizi wa kumbukumbu na nyaraka.64. Mheshimiwa Spika, Katika kutekeleza kazi hizo, kwa mwaka wa fedha 2013/2014 Mfuko umetenga jumla ya TZS 13,500.00 milioni kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya uwekezaji, kati ya hizo TZS 7,000.00 milioni kwa kuendeleza ujenzi wa kiwanja cha kufurahishia watoto cha Uhuru kwa Unguja TZS 4,000 milioni kwa kuanza ujenzi wa kiwanja cha Umoja kwa Pemba na TZS 2,500 milioni kwa mradi wa ujenzi wa kiwanja cha Mbweni. Aidha, Mfuko umepanga kutumia TZS 3,216 milioni kwa ajili ya shughuli za uendeshaji.D8. BENKI YA WATU WA ZANZIBAR (PBZ)

65. Mheshimiwa Spika, Jukumu kubwa la Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ) ni kupokea amana za wateja wake na kukopesha kwa wanaohitaji pamoja na kuwapatia wateja huduma mbalimbali za kibenki. Kwa mwaka 2012 Benki imetekeleza yafuatayo:

i) Kupokea amana za wateja zenye kiwango cha TZS 212,937.00 milioni ikiwa ni asilimia 96 ya lengo lililowekwa la TZS 220,191.11 milioni;

ii) Kutoa mkopo wa jumla ya TZS 109,424.16 milioni sawa na asilimia 112 ya lengo lililowekwa la TZS 97,265.11 milioni kwa mwaka;

iii) Kuongeza kiwango cha rasilimali ya Benki kufikia TZS 247,838.00 milioni ikilinganishwa na lengo la TZS 252,691.62 milioni;

iv) Kukusanya mapato ya TZS 21,667.17 milioni yanayotokana na huduma mbalimbali za kibenki ambayo ni sawa na asilimia 104 ikilinganishwa na makadirio ya TZS 20,983.88 milioni;

v) Kuanzisha uhusiano na Benki ya Viwanda na Biashara ya China “Industrial and Commercial Bank ya China” (ICBC) kwa nia ya kurahisisha biashara kati ya pande hizi mbili.66. Mheshimiwa Spika, Kuhusu maendeleo ya Benki ya Kiislamu hadi kufikia tarehe 30 Juni, 2013, Benki imeweza kujipatia wateja 26,588 wenye amana zinazofikia jumla ya TZS 25,592.56 milioni. Kwa upande wa mikopo inayofuata misingi ya shariah za kiislamu, benki imeshatoa mikopo yenye thamani ya jumla ya TZS 8,191.00 milioni, ambapo wakopaji ni wafanyakazi wa Serikali, taasisi za Serikali na mashirika binafsi.67. Mheshimiwa Spika, Katika kipindi cha mwaka 2012/2013, Benki imeweza kuanzisha njia mpya ya kuwafikia wateja kupitia mtandao wa simu na mtandao wa Internet (PBZ Mobile Banking na PBZ Online Banking) pamoja na kufungua vituo vya huduma za Benki huko Makunduchi na Mazizini kwa upande wa Unguja na Wete na Mkoani kwa Pemba. Benki tayari imeshatengeneza sera ya mikopo ya nyumba pamoja na sera ya mikopo ya wateja wadogo wadogo na wateja wa kati.68. Mheshimiwa Spika, Katika kujiimarisha zaidi, Benki imejiunga na huduma ya kusafirisha fedha ya (World Remit) ambayo inarahisisha usafirishaji fedha kwa Watanzania wanaoishi nje ya nchi (Tanzania Diaspora). Huduma hii itarahisisha na kuweka mfumo wa kuaminika zaidi kwa usafirishaji Fedha kati ya Watanzania wanaoishi nje na ndugu zao wanaoishi Zanzibar na Tanzania bara.69. Mheshimiwa Spika, Katika mwaka wa fedha 2013/2014, PBZ imekusudia kutekeleza yafuatayo:

i) Kuendeleza majukumu yake makuu ya kukusanya amana TZS 262,182 milioni hadi kufikia Disemba 2013 za wateja na kutoa mikopo TZS 119,370 milioni hadi kufikia Disemba 2013;

ii) Kuongeza mapato ya TZS 24,958 milioni yanayotokana na vianzio mbalimbali;

iii) Kuzindua tawi la Benki ya Kiislamu ya PBZ, katika jengo la BIMA lililoko mtaa wa Mpirani Unguja;

iv) Kuanza matayarisho ya ujenzi wa jengo jipya la Makao Makuu ambalo litaendana na hadhi ya Benki ya Watu wa Zanzibar Ltd;

v) Kueneza huduma za ATM katika maeneo mbali mbali ya Zanzibar ikiwemo Tunguu (SUZA), Michenzani (Majenzi) na Bandarini Malindi;

vi) Kufungua matawi mengine zaidi Tanzania Bara katika mikoa ya Mtwara na Mwanza baada ya kukamilika utafiti juu ya mahitaji ya huduma za kibenki katika maeneo hayo;

vii) Kuanzisha vituo vya huduma za kibenki Kaskazini Unguja na Dar es Salaam;

viii) Kujiunga na mitandao ya VISA na Master Card ambayo itawawezesha wateja wa Benki ya Watu wa Zanzibar kupata huduma za kibenki popote pale duniani na pia Benki kuwa na uwezo wa kutoa huduma kwa wageni wanaokuja Zanzibar.V. MAMBO YALIYOJITOKEZA KATIKA KIKAO HIKI CHA BARAZA

70. Mheshimiwa Spika, Katika mijadala ya mapendekezo ya bajeti za Wizara na Taasisi mbalimbali, Waheshimiwa Wajumbe wa Baraza walihoji mambo ambayo yaliweza kupatiwa majibu. Hata hivyo kuna mambo machache ambayo walihitaji maelezo zaidi likiwemo suala la utekelezaji wa mradi wa “E–government”. Naomba nitumie fursa hii na mimi kutoa maelezo machache ya ziada.71. Mheshimiwa Spika, Kimsingi dhamira ya Serikali ya kuimarisha matumizi ya Teknohama Serikali ipo siku nyingi ambapo chimbuko la Mradi wa sasa wa “E-government” ni Mradi wa Usajili wa Wazanzibar Wakaazi. Mandalizi ya mradi huu yalibainisha haja ya kuimarisha na kuunganisha matumizi ya Teknohama Serikalini kwa upana mkubwa zaidi. Maeneo yaliyobainishwa katika waraka wa Mradi wa mwaka 2004 ni pamoja na Daftari Kuu (Core Registry) na Madaftari (Registries) zinazohusisha masuala ya utambulisho wa Ardhi na Makaazi. Wakaazi wa Manispaa, Wanafunzi, Wasimamizi wa mipaka, Bandarini na Viwanja vya Ndege, Leseni za udereva, Daftari la Wapiga Kura na Huduma za Afya. Kama lilivyo, hili ni suala pana sana na linahitaji kujengwa kwa awamu.

72. Mheshimiwa Spika, Mradi uliotekelezwa na unaotakiwa kutolewa maelezo umehusisha maeneo makubwa matano ambayo ni:

i) Miundo mbinu (fibre optic);

ii) “Intranet na Internent”;

iii) Maeneo ya matumizi (Application and Potray);

iv) Elimu;

v) Masuala ya Usalama (Security).73. Mheshimiwa Spika, Mradi ulikadiriwa na hatimae kuidhinishiwa jumla ya Dola za Kimarekani Milioni 20 (USD 20.00 milioni) ambazo zilipatikana kama mkopo nafuu kutoka Serikali ya Watu wa China kupitia Benki ya Exim ya China. Kampuni ya ZTE Corporation ya China ndio iliyopendekezwa na hatimae kuhusika na ujenzi wa miundombinu hiyo. Kimsingi maeneo makuu yaliyotekelezwa na mradi ni pamoja na haya yafuatayo:

i) Uwekaji wa mkonge wa fibre optic Unguja na Pemba ambapo jumla ya kilomita 352 zikiwemo (266 kwa Unguja na 86 kwa Pemba) zilihusika pamoja na ununuzi wa vifaa vyake;ii) Ujenzi wa jengo lililopo Mazizini na uwekaji vifaa katika kituo hicho cha taarifa (Data Center) ikiwemo “hard ware” Software na basic applications” masuala ya mtandao na usalama wa kituo. Kituo hiki kimeimarishwa kwa kuwekewa:

• Mitambo ya usalama kwenye milango yake,

• Vifaa vya kutambua ishara za moto (Fire Alert and Smoke detector),

• Vifaa vya kuzimia moto vya automatic,

• Mitambo ya mawasiliano ya CCTV,

• Uzio wa umeme (Elecrtic fence),

iii) Mafunzo kwa timu ya TEHAMA;

iv) Ujenzi wa minara miwili ya Microwave Unguja na Pemba;

v) Kununua transforma mbili (2) kwa kuhudumia minara na towers;

vi) Kununua standby generators (13) kwa kuhudumia viunganisho vya waya (pops);

vii) Kununua standby generator moja (1) kwa ajili ya kitua cha mashine (Data Center).74. Mheshimiwa Spika, Juu ya kwamba gharama zinaelezwa kuwa ni kubwa, kiasi hicho cha gharama kimefikiwa baada ya kupunguzwa upeo wa mradi kwa kuondoa uwekaji wa mkonga chini ya bahari baina ya Unguja na Pemba. Makisio yaliyowasilishwa awali ni Dola za Kimarekeni Milioni 36 kwa Kampuni ya Huawei na Dola 33 milioni kwa kampuni ya ZTE ambayo ilibarikiwa.75. Mheshimiwa Spika, Wakati mradi ukitekelezwa, kumefanyika pia mazungumzo na kampuni ya Zantel kwa ajili ya ubia katika uwekezaji na uendeshaji. Chini ya makubaliano yaliyofikiwa, Zantel inatarajiwa kuwekeza kwa kuunganisha ofisi zote za Serikali kwa kumalizia (Last mile) na mkonga (Fibre optic) na hivyo kuleta ufanisi zaidi kuliko njia ya “Wireless” iliokusudiwa kutumika hapo awali. Kwa bahati mbaya mazungumzo na Zantel yalichukua muda mrefu kuliko ilivyotarajiwa na hivyo kuathiri kuanza rasmi kunufaika na mtandao huo zikiwemo ufanisi katika mawasiliano na kupata huduma za Internet bila ya malipo kwa Serikali yote. Mkataba wa Zantel umetiwa saini tokea mwezi Febuari mwaka huu na kwa sasa matayarisho ya mwisho ya utekelezaji yamekamilika. Kukamilika kwa uwekezaji wa Zantel kutaunganisha visiwa vya Unguja na Pemba kwa njia ya kupitia mikonga ya umeme (Dar-Unguja na Pemba-Tanga).76. Mheshimiwa Spika, Natumai baada ya maelezo hayo sasa Waheshimiwa Wajumbe wamepata, japo kwa muhtasari maelezo ya mradi huo. Nia ya Serikali ni kuendelea na kuimarisha maeneo mengine ya TEHAMA kama vile katika kuimarisha huduma za afya, usimamizi wa mapato na mengineyo.E. HITIMISHO

77. Mheshimiwa Spika, Naomba kumalizia kwa kukupongeza tena jinsi ulivyo endesha kikao hichi na kuendelea kulijengea heshima Baraza letu hili ambalo ni nguzo muhimu kwa ustawi wa Zanzibar na Wazanzibari. Naomba pia kuwashukuru Waheshimiwa Wajumbe kwa kufanikisha kazi zetu hadi leo hii tunakaribia kukamilisha kikao hichi cha Bajeti kwa kumalizia na Ofisi hii ambayo ndio moyo wa Serikali.78. Mheshimiwa Spika, Kufikia hatua hii leo, ni dhahiri kuwa tumekuwa na safari ndefu sana. Ni matumaini yangu kuwa Waheshimiwa wajumbe wataidhinisha mapendekezo ya Bajeti kwa ofisi yangu bila ya vikwazo. Kwa hivyo, kwa heshima na taadhima kwa mwaka wa fedha wa 2013/14, naomba Baraza lako Tukufu liidhinishe ukusanyaji wa mapato ya TZS 409,892.4 milioni na matumizi ya jumla ya TZS 160,773.20 milioni kati yake ikiwa TZS 44,794.00 milioni ni kwa kazi za kawaida, (zikiwemo TZS 28,695.00 milioni kwa matumizi ya Idara zake Kiambatisho VII) na TZS 42,438.40 milioni kwa ajili ya kazi za maendeleo kwa Ofisi ya Rais Fedha, Uchumi na Mipango ya Maendeleo. Fedha hizi ni kukidhi pia matumizi ya Tume ya Mipango ya Zanzibar ya TZS 2,564 millioni kwa kazi za kawaida na TZS 4911.80 millioni kwa matumizi ya kazi za maendeleo. Aidha, ofisi inaomba iidhinishiwe jumla ya TZS 66,065.00 milioni kwa matumizi ya Mfuko Mkuu wa Serikali kama uchambuzi unavyoonesha hapo chini.

G. MWELEKEO WA BAJETI YA MWAKA 2013/2014

VOTE 19 (OR) FEDHA, UCHUMI NA MIPANGO YA MAENDELEO TZS Bilioni

I Matumizi ya Kawaida 44,794.00

Mishahara 3,414.00

Matumizi mengineyo (O/C) 6,517.00

Ruzuku kwa Taasisi 17,363.00

Marekebisho ya Mishahara 17,500.00

II Matumizi ya Kazi za Maendeleo 42,438.40

Mchango wa Serikali 7,950.00

Ruzuku na Mikopo 17,488.40

Ununuzi wa Meli mpya ya abiria 17,000.00

VOTE 49 TUME YA MIPANGO

III Matumizi ya Kawaida 2,564.00

Mishahara 866.50

Matumizi mengineyo (O/C) 397.50

Ruzuku kwa Taasisi (OCGS) 1,300.00

Matumizi ya Maendeleo 4,911.80

Mchango wa Serikali 985.00

Ruzuku na Mikopo kutoka Nje 3, 926.80

VOTE 45 MFUKO MKUU WA SERIKALI

IV Gharama za Mfuko Mkuu wa Serikali 66,065.00JUMLA KUU (VOTES 19, 49 na 45) 160,773.20

79. Mheshimiwa Spika, Uchambuzi wa utekelezaji wa Bajeti iliyopita pamoja na mapendekezo ya mapato na matumizi ya Bajeti ya mwaka 2013/2014, pamoja na muhtasari wa maelezo mengine unaonekana katika Viambatanisho (Nam. I-VIII).80. Mheshimiwa Spika, Pamoja na hotuba hii naomba kuwasilisha muhtasari wa maelezo ya bajeti inayozingatia programu maalum ya Program Based Budget (PBB) ya Ofisi ya Rais Fedha, Uchumi na Mipango ya Maendeleo.81. Mheshimiwa Spika, Baada ya maelezo haya sasa naomba kutoa hoja.1 comment:

  1. Ahsante.....kazi nzuri othman mapara kwa kurusaidia sisi kupata habari mtandaoni

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.