Habari za Punde

Waziri wa Habari Utamaduni Utalii Michezo Atowa Taarifa ya Serikali kuhusu Wageni waliomwagiwa Tindi Kali Jana Usiku.

 Waziri wa Habari Utamaduni Utalii na Michezo Said Mbarouk, akitowa Taarifa ya Serekali kuhusu Tukio la kumwagiwa Tindi Kali Watalii kutoka Uingereza na Watu wasiojulikana usiku wa jana katika maeneo ya shangani Mji Mkongwe wa Zanzibar, Serekali imelani kitendo hicho na kutoa Taarifa kwa Wananchi kushirikiana na Serekali kuwataja Watu waliohusika na tukio hilo.na kutoa Shilingi Milioni Kumi kwa mtu atakayetowa Taarifa hiyo kwa Serikali.
 Waandishi wa habari wakuifuatilia maelezo ya Serekali kuhusiana na Tukio hilo.


Mwenyekiti wa Jumuiya ya Utalii Zanzibar ZATO Mr Abdulsamad Said Ahmeid, akilaani kitendo cha Watu wasiojulikana kuwamwagia Tindi Kali Watalii wakiwa katika matembezi yao katika mji mkongwe.Jumuiya hiyo imelaani kitendo hicho na kutowa kauli ya kulaani kwa hatua zote kuhusiana na kitendo hicho wakati wa kuzungumza na Waandishi wa Habari katika ukumbi wa Habari Maelezo Zanzibar.

1 comment:

  1. Haya ndiyo matokeo ya uongozi wa kuoneana aibu na kutokuwajibishana!

    Kwa kweli inauma sana, wakati naandika maoni haya kuna mpaka !Breaking news" kwenye BBC na AL-JAZEERA kuhusu tukio hili!

    Kutokana na mlolongo wa matukio kama vile: kupigwa risasi na kujeruhiwa Padri, kuuwawa kwa Padri Mushi, kumwagiwa tindi kali kwa Sheha kidevu na sheikh Soraga, inatosha kabisa kwa ndugu yetu cOMMISSIONER MUSSA kuhamishiwa SUMBAWANGA!

    Visiwa hivi mambo hayaeendi kabisa! pamoja na udogo wake na uchache wa watu!

    Haya angalia namna uzembe unavyotaka kutugharimu, huu ndio msimu wa utalii, vijana wetu, wameshajipanga kutafuta riski..lkn wapi?

    Jeshi la polisi limeshindwa kazi kabisa!..siku 10 tu zilizopita yakitokea karibia matukio matano ya watu kukabwa, kujeruhiwa na kunyang'anywa mali ndani ya siku moja na hakukua na taarifa yoyote ya Polisi!

    Tulisema wakati ule...'jamani vikundi hivo, mnavilea vitakuja kutiletea maafa' sasa nadhani mtatukumbuka!

    Visiwa vya ajabu hivi, hata tukio likitokea hapo jang'ombe linaweza kushindwa kuripotiwa...gazeti lenyewe moja, Tv moja..yaani ni zama za maweeee!!

    Waziri husika..sijda kubwaaa, utendaji hafifu...hawa ni watu walitakiwa waachwe kule kule kwenye uwalimu, hana 'exposure' wala hajui utalii ni nini...maafa matupu!!

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.