Habari za Punde

BLW Washerehekea Ubingwa wao kumkabidhi Kikombe Meneja wa Timu


 
 Meneja wa Timu ya BLW Nassor Salim Jazira akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kukabidhiwa kombe hilo na Nahodha wa timu hiyi Ussi Jecha Simai Mwakilishi wa Chaani.
 Meneja wa timu ya BLW Nassor Salim Jazira Mwakilishi wa Rahaleo akimkabidhi zawadi za fedha taslim shilingi milioni mbili kwa ajili ya wachezaji wa timu hiyo Nahodha wa timu hiyo Ussi Jecha Simai.ushoto.
 Wachezaji wa timu ya BLW wakimsikiliza Meneja wao wakati wa kuipongeza timu hiyo baada ya kunyakuwa Ubingwa wa Michuano yaKombe la Mabenki Zanzibar baada ya kuifunga timu ya PBZ.
 Kocha wa timu ya BLW Juma Yussuf Sumbu akitowa shukrani kwa Uongozi wa BLW na wachezaji wa timu yake kwa ushirikiano wa kuweza kulitowa Kombe hilo kwa mara ya kwanza kuazisha hapa Zanzibar chini ya Ufadhili wa Benki ya Watu wa Zanzibar
 Wachezaji wa timu ya BLW wakiwa na Kombe lao la Ubingwa wa Michuano ya Mabenki Zanzibar.


 Kocha wa timu ya TASWA Zanzibar Ali Cheupe, akimpongeza kocha mwezake Juma Yussuf Sumbu kwa timu yake kulitowa Kombe hilo la Mabenki Zanzibar lilliloshirikisha timu za Mabenki na Taasisi za Fedha Zanzibar,
 Wachezaji na Viongozi wa timu ya Baraza la Wawakilishi wakiwa katika picha ya pamoja na Kombe lao wakiwa nje ya Jengo la Baraza la Wawakilishi Chukwani Zanzibar.
 Viongozi wa timu ya Baraza la Wawakilishi na Makocha wakiwa katika picha ya pamoja wakiwa na Kombe lao jipya walilolitowa dhidi ya timu ya PBZ kwa kuwafunga kwa peneti 4-3.na kuibuka mshindi wa michuano hiyo kwa mwaka huu, likiwa ni mara ya kwanza kuazishwa kwa michuano hiyo chini ya Ufadhili wa Benki ya Watu wa Zanzibar.
                                      Wachezaji wa timu ya BLW wakiwa na Meneja wao Dau.
 Jopo la Wachezaji wa timu ya BLW wakiwa katika picha ya pamija katika picha ya kumbukumbu na Kombev lao.


No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.