Habari za Punde

Dk Shein Aagana na Balozi Mdogo wa Oman Nchini

 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akisalimiana na Balozi Mdogo wa Oman Nchini Tanzania anaefanyia kazi zake Zanzibar  Saleh Suleiman Al
Harth,alipofika Ikulu Mjini Zanzibar kumuaga Rais baada ya kumaliza muda wake wa kazi Nchini

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akifuatana na  Balozi Mdogo wa Oman Nchini Tanzania anaefanyia kazi zake Zanzibar  Saleh Suleiman Al
Harth,alipofika Ikulu Mjini Zanzibar kumuaga Rais baada ya kumaliza muda wake wa kazi Nchini.[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]
 
Na  Said Ameir. Ikulu
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein amempongeza na kumshukuru Balozi Mdogo wa Oman anayemaliza muda wake Bwana Saleh Suleiman Al Harth kwa jitihada zake kubwa za kuimarisha ushirikiano kati ya Zanzibar na Oman wakati wote alipokuwa nchini.
 
Dk. Shein ametoa pongezi na shukrani hizo jana wakati alipokuwa akizungumza na Balozi mdogo huyo Ofisini kwake Ikulu ambako alikwenda kumuaga.
 
Mheshimiwa Rais alibainisha katika mazungumzo hayo kuwa katika kipindi ambacho balozi huyo amekuwepo nchini ushirikiano kati ya Zanzibar na Oman umeimarika na kumekuwepo na mafanikio makubwa katika ushirikiano huo kwa pande zote mbili.
 
“Kipindi kifupi ulichokuwepo hapa, tumeshuhudia mafanikio makubwa katika uhusiano na ushirikiano wetu wa kihistoria” alieleza Dk. Shein.
 
Aliongeza kuwa ni muhimu kwa ushirikiano huo kuimarishwa zaidi na zaidi sio tu kutokana na historia bali pia udugu na ukaribu wa watu wa Zanzibar na Oman.
 
Dk. Shein alimueleza Balozi Al Harth kuwa Serikali na wananchi wa Zanzibar wanathamini sana mchango unaotolewa na Serikali ya Oman kwa maendeleo ya Zanzibar na kwamba daima wataendelea kushirikiana kuimarisha uhusiano na ushirikiano uliopo kwa faida ya Serikali na wananchi wa nchi mbili hizo.
 
Mheshimiwa Rais alitumia fursa hiyo kutoa salamu za heri kwa Mfalme wa Oman Sultan Qaboos na viongozi  wengine wa nchi hiyo.
 
Kwa upande wake Balozi Al Harth alimueleza Mheshimiwa Rais kuwa anaondoka Zanzibar na kumbukumbu nzuri ya ukarimu na ushirikiano alioupata kutoka kwa Serikali na wananchi wa Zanzibar wakati wote alipokuwa nchini.
 
“Nimetekeleza majukumu yangu vizuri lakini nieleze ukweli nimesaidiwa sana na viongozi wa watendaji wa Serikali” alieleza Balozi Al Harth na kubainisha kuwa hali hiyo ilimfanya aifurahie kazi yake wakati wote

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.