Habari za Punde

Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balizi Seif Ali Afungua Mkutano wa 15 wa Jumuiya ya Wafanyabiashara wenye Asili ya Afrika.

 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akihutubia katika Mkutano wa 15 wa Jumuiya ya Wafanyabiashara wenye asili ya Afrika, wakati wa ufunguzi wa mkutano huo uliofanyika Mjini wa Seattle Marekani 
 Waziri wa Biashara, Viwanda na Masoko Zanzibar aiyevaa Kipkapa na Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Ali Khalid Mirza wakibadilishana mawazo na mmoja wa wafanyabiashara waliohudhuria mkutano wa 15 wa Jumuiya ya wafanyabiashara wenye asili ya afrika Mjini Seattle.
 Wajumbe wa Mkutano wa 15 wa Jumuiya ya Wafanyabiashara wenye asili ya Afrika ya Kaskazini Magharibi ya Pacif Mjini Seattle wakijiorodhesha Tayari kwa kuanza mkutano wao kwenye Hoteli ya Red Lion Mjini Settle.
 Mkuu wa Ofisi ya Kampuni ya Mtandao wa bidhaa za uwekezaji katika miradi ya usafiri wa anga Nchini Marekani akibadilishana mawazo na wafanyabiashara wa Zanzibar kushoto yake wa kwanza Mohamed Piyaral Bhaloo,Abdulsabad Said Ahmed na Javed Jafferji.
  Profesa Margeret Kihara Mshauri wa masuala ya wajasiri amali Mjini Seattle akizungumza na Mwenyekiti wa Chama cha wafanyabiashara wenye viwanda na wakulima Zanzibar Abdulla Abass wakati wa mapumziko wa Mkutano wa 15 wa Jumuiya ya wafanyabiashara wenya asili ya Afrika Mjini Settle.
 Mfanyabiashara wa chama cha wafanyabiashara kutoka Nchini Afrika Kusini Bwana Ndaba Cyril  akifurahia na kuridhika na vipeperushi vya mambo mbali mbali ya Zanzibar kwenye meza ya Wafanyabiashara wa Zanzibar katika maonyesho yaliyokuwa nje ya ukumbi wa Mikutano wa Red Lion ambao ulifanyika Mkutano wa 15 wa Jumuiya ya wafanyabiashara wenye Assili ya Afrika Mjini Seattle.
 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyabiashara waliohudhuria mkutano wa 15 wa Jumuiya ya wafanyabishara wenye asili ya Afrika,Kulia yake ni Jesse T. Tani Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mega Mjini Settle, kushoto yake ni Bwana Suleiman wa Ofisa wa Ubalozi wa Tanzania Nchini Marekani na Canada na Faouzi Sefrioui na  Kamishna wa Fedha wa Kampuni ya Nyumba Mjini Seattle.

Mwenyhekiti wa chama cha Wafanyabiashara wenye viwanda na wakulima Zanzibar Abdull Abass akimkabidhi zawadi maalum ya Picha inayoonyesha mandhari ya Zanzibar iliyosarifiwa kwa majani ya Gomba Mjumbe wa Baraza la Mji wa Seattle aliyemuwakilisha Meya wa Mji huo Bw. Bruce Harrel wakati wa chakula cha mchana kwenye Mkutano wa Jumuiya ya wafanyabiashara wenye asili ya Afrika Mjini Seattle.
Mwana Habari  wa Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Othman Khamis akiwa katika harakati za dondoo za kutafuta mambo mbali mbali kwa ajili ya kutuma habari kwenye mkutano wa Chama cha wafanyabiashara wenye asili ya Afrika Mjini Settle Nchini Marekani alipokuwa akizungumza na mmoja wa wanajumuiya hiyo Bibi Darla Muya wa Marekani.
 Msanii Koffi Anang na mwenzake Yawasare kutoka Nchini Ghana wakitumbuiza wajumbe wa Mkutano wa 15 wa Jumuiya ya Wafanyabiashara wenya asili ya Afrika ya Kaskazini Magharibi mwa Pacific Mjini Seattle kabla ya kuanza kwa mkutano huo.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.