Mkurugenzi wa Wizara ya Afya Zanzibar ambae pia ni Daktari
Bingwa wa Upasuaji, Dkt. Malik Abdalla Juma amelazwa katika Hospitali ya
Agakhan ilioko Nairobi nchini Kenya baada ya
kushambuliwa na watu wasiojulikana.
Tukio la kujeruhiwa Mkurugenzi huyo limetokea jijini Nairobi wakati alipokuwa
akihudhuria Mkutano wa Elimu endelevu ya Udaktari.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Dkt. Saleh Jidawi aliyasema
hayo alipokuwa akizungumza na waandishi ofisini kwake Mnazi mmoja mjini Unguja.
Alisema Daktari huyo amejuruhiwa katika sehemu ya kichwa na
macho na kumsababishia kupata maumivu mwilini mwake.
Aidha alisema mara tu ya kutokea kwa tukio hilo Daktari huyo alikuwa amelazwa katika
hospitali ya Kenyatta kwa matibabu ya awali lakini hivi sasa amehamishiwa
katika hospitali hiyo kwa ajili ya kupata matibabu zaidi.
Hata hivyo alisema Serekali kwa kushirikiana na Wizara ya
Afya itahakikisha kwamba Dkt.Malik anaangaliwa chini ya maandalizi ya madaktari
mabingwa wa upasuaji wa ubongo (Neuro Surgeons) ili waweze kujua athari
zilizojitokeza baada ya kupata mara
majaraha na kupatiwa huduma zinazofaa kwa wakati muwafaka.
Sambamba na hayo alisema kwamba serekali itagharamia gharama
zote za matibabu yake zinazostahiki huku na kupeleka ujumbe wa watu wane ambao
utaongozwa na Katibu Mkuu na Mkurugenzi na watu wawili kutoka katika familia
yake.
Katibu Jidawi amesema hivi sasa ni mapema kueleza jambo
lolote katika hatua ya zinazoendelea katika kupatiwa matibabu, hivyo baada ya
kufika huko na kurejea kwao ndio watatoac taarifa zaidi.
Mbali na hayo baadhi ya watu waliosafiri nchini Kenya ambao hawakupenda kutaja majina yao walisema wao wakati walipokuwa Nairobi
nchini Kenya
walipewa tahadhari na madereva wa texi, kuwa hivi sasa kumekuwa na matukio ya
kihalifu.
Walisema miongoni mwa tahadhari waliopewa za kutembea
nyakati za jioni katika baadhi ya mitaa, pia asiwe mtu mmoja pekee yake katika
matembezi yake.
No comments:
Post a Comment