NAFASI ZA KAZI
Latif
Primary School ni skuli mpya ya kisasa inayotarajiwa kuanza kwa muhula wa
kwanza wa masomo mwaka 2014 inatangaza
nafasi za ajira kwa ngazi zifuatazo.
1 Mwalimu Mkuu
Sifa za
mwombaji
· Awe angalau na Diploma ya Ualimu.
· Awe si chini ya umri wa miaka 35
· Awe na uzoefu wa angalau miaka miwili katika nafasi ya Uwalimu mkuu, mkuu wa idara au nafasi yoyote ya
uongozi katika elimu.
· Awe na uzoefu wa kusomesha usiopungua miaka 5
· Mwombaji mwenye diploma ya uongozi (management)
atakuwa na kigezo cha nyongeza (added advantage)
· Awe ni mwenye tabia njema na mwenye
kuheshimika
· Awe na uwezo wa kutumia computer
hasa program za Microsoft Office
· Awe na uwezo wa kuzungumza,kusoma na
kuandika Kiswahili na Kiingereza kwa ufasaha
2 Walimu wa kawaida (darasa la kwanza mpaka la
tatu)
Sifa za
mwombaji
· Awe angalau na Diploma ya ualimu
msingi kati ya masomo ya Kiswahili English, Hesabati, Kiarabu, Dini, au Mazingira.
· Awe si chini ya umri wa miaka 25
· Awe na uzoefu wa kusomesha usiopungua miaka miwili
· Awe na uwezo wa kuzungumza,kusoma na
kuandika Kiswahili na Kiingereza kwa ufasaha
· Uwezo wa kutumia computer utapewa
kipaumbele
3 Msimamizi wa ofisi
Sifa za
mwombaji
· Awe angalau na Diploma ya uhasibu
· Awe si chini ya umri wa miaka 25
· Awe na uzoefu wa kazi usiopungua miaka miwili
· Awe na uwezo wa kuzungumza,kusoma na
kuandika Kiswahili na Kiingereza kwa ufasaha
· Uwezo wa kutumia computer ni lazima
Jinsi ya kutuma maombi
· Barua za maombi ziambatanishwe na
maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed C.V) pamoja na picha mbili za
Passport size za hivi karibuni moja iandikwe jina nyuma
· Kwa urahisi wa mawasiliano, waombaji
waonyeshe anwani na namba za simu za kuaminika, na barua pepe kama anayo
· Maombi yote yaambatane na nakala za
vyeti vya kidato cha nne na vyeti vya kuhitimu
mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika.
· Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 9
Disemba 2013 saa 11 jioni
· Maombi yanaweza kuandikwa kwa Lugha
ya Kiswahili au Kiingereza na mwombaji anaweza kuwasilisha maombi yake kwa
mkono kwa kufika jengo la skuli liliopo Malindi nyuma ya msikiti wa Ijumaa wa
malindi karibu na Pyramid Hotel.
· Pia yanaweza kutumwa kwa njia ya posta au barua pepe kupitia
anuani ifuatayo.
Mwenyekiti wa kamati
Latif Primary School
SLP 860
Zanzibar
Barua pepe
almdrasatullatif@gmail.com
Nambari za simu : 0777 416 723 au
0772 000 550
NAFASI ZA MASOMO
Pia skuli hii inapenda kuwatangazia wananchi
kuwa inaanza kupokea maombi ya wanafunzi wa darasa la kwanza mpaka la tatu kwa
masomo ya msingi kwa muhula mpya wa mwaka 2014.
Latif Primary School ni skuli mpya na ya kisasa
iliyopo Malindi, Zanzibar. Ni skuli
Inayozingatia maadili ya Kiislamu na pia yenye kutoa elimu ya kisasa ikiwemo
masomo ya computer
Fomu za uandikishaji zinapatikana katika jengo
la skuli.
Kwa maelezo zaidi, tafadhali wasiliana nasi
kupitia simu nambari 0777 416723 au
0772 000 550. Pia kwa kupitia barua pepe: almdrasatullatif@gmail.com
Pia unaweza kufika katika jengo la skuli
liliopo Malindi nyuma ya msikiti wa Ijumaa wa Malindi karibu na Pyramid Hotel
Ni bahati hiyo kwa ndugu zetu waalimu hasa wale ambao wamekua wakisubiri ajira kwa mda mrefu bila mafanikio.
ReplyDeleteHata hivyo sidhani kama sifa zilizotajwa zinaweza kupatikana miongoni mwa walimu wa kizanzibari. kutokana na sababbu zifuatazo:
1) Hapa kwetu Ualimu mkuu ni cheo ambacho mwalimu hukisubiri kwa mda mrefu na anapobahatika kukipata hawezi kuacha kazi mwenyewe labda afukuzwe.
2) Walimu wenye Diploma za uongozi, umri na uzoefu uliotajwa wengi wapo SMZ sidhani kama kuna mwl. mwenye ujasiri wa kuacha kazi na kwenda LATIF kwa utamaduni wetu hapa!
Wataishia tu kuwapata walimu wastaafu (washao choka) au wale ambao hawajaajiriwa!
Hapa ninapoishi ni kawaida kutajwa mshahara katika tangazo la kazi.
ReplyDeleteSasa nauliza mishahara ni kiasi gani kwa kulingana na nafasi hizo za kazi ?
Ni kweli kama ulivosema Anonymous wa kwanza kwamba ni ngumu kupata wenye viwango hivo ambao watakuwa tayari kujiunga na Latif.
ReplyDeleteAnonymous wa pili, kama unataka kujua zaidi kuhusu kazi au mishahara si uwapigie simu tu upate taarifa zaidi? Si kila kitu kinaendana na ulivyozowea wewe