WAZIRI
wa Nchi ofisi ya Rais, tawala za Mikoa na Idara maalum za Serikali ya Mapinduzi
ya Zanzibar ,
Mhe. Haji Omar Kheir akihutubia katika kilele cha wiki ya walipa kodi
iliyofanyika katika Hoteli ya Bwawani mjini Zanzibar ,
kushoto Naibu Kamishna wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ofisi ya Zanzibar , Mcha Hassan na
Mwakilishi wa Jumuia ya Wafanyabiashara, wenye viwanda na wakulima, Mbarouk
Omar.
Naibu Kamishna wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ofisi ya Zanzibar , Mcha Hassan akitowa maelezo ya maadhimisho ya Saba ya Mlipa Kodi Tanzania wakati wa kutowa Vyeti kwa Walipakodi Bora kwa mwaka 2013, hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa hoteli ya Bwawani Zanzibar.
WAZIRI
wa Nchi ofisi ya Rais, tawala za Mikoa na Idara maalum za Serikali ya Mapinduzi
ya Zanzibar, Mhe. Haji Omar Kheir (kushoto) akimkabidhi cheti cha mshindi wa
kwanza katika mchango mkubwa wa ulipaji wa kodi Zanzibar, Mwakilishi kutoka
kampuni ya Zanzibar Communication (ZANTEL), Aziz Said Ali. Cheti hicho
kilitolewa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ofisi ya Zanzibar katika kilele
cha wiki ya walipa kodi iliyofanyika katika Hoteli ya Bwawani
MWAKILISHI wa Shirika la Magazeti ya Serikali
Zanzibar (SMS) wachapishaji wa Magazeti ya ‘Zanzibar
leo’, ‘Zanzibar leo jumapili’ na Zaspoti, Haroub
Hussein Khamis (kulia) akipokea cheti maalum kutoka kwa Waziri wa Nchi ofisi ya
Rais , Tawala za Mikoa na Idara maalum za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar , Mhe. Haji Omar
Kheir baada ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ofisi ya Zanzibar
kulizawadia Shirika hilo
kwa utoaji wa habari za ulipaji wa kodi. Cheti hicho kilitolewa katika kilele
cha wiki ya walipa kodi iliyofanyika katika Hoteli ya Bwawani
No comments:
Post a Comment