Kwa niaba ya Taasisi ya Wahitimu wa Lumumba (Lumumba Alumni Association - Zanzibar - LUAZA) tunasikitika kutangaza kifo cha Mwalimu Mkuu wetu Mstaafu wa Lumumba kwa mwaka 1981-1983, Maalim Ali Rajib Juma Katibu Mkuu Mstaafu Ofisi ya Waziri Kiongozi na Kamishna Mstaafu wa Tume ya Utumishi wa Umma Zanzibar , kilichotokea jana Jumapili 13 Julai, 2025 katika Hospitali ya Lumumba, Hospitali ya Mkoa wa Mjini Magharibi.
Maziko yatafanyika leo Jumatatu, Saa Saba Mchana (Adhuhuri), Maiti ataondokea Mlandege na Kuswaliwa katika Msikiti wa Masjid Assalam, Mlandege na kuzikwa Kijini Makunduchi.
اللَّهُمَّ اغْفِرْ لَهُ وَارْحَمْهُ، وَمَسْكَنَهُ فِي الْجَنَّةِ
Hakika sisi ni wa Mwenyezi Mungu na kwake Yeye tutarejea.
Visiwani tumepata pigo na pengo kubwa kwa kuondokewa na mmoja katika majabali na majemadari waliojenga nchi yetu na kuwafunda vijana wetu.
Huyu ni Maalim Ali Rajab Juma ambaye jana tarehe 13 Julai 2025 alivuta Pumzi zake za mwisho katika hospitali ya Lumumba, Hospitali ya Mkoa wa Mjini Magharibi, Unguja Zanzibar.
Marehemu alikuwa miongoni mwa walimu mahiri wa somo la Jiografia nchini, na aliwahi kusomesha skuli ya Haile Sellasie miaka ya 70's na anasifika kuwa aliwahi mwandishi hodari na mahiri wa miradi ya maendeleo.
Katika historia yake ya kitaaluma, Maalim Ali Rajab alibahatika kuwa sehemu ya Skuli ya Lumumba…
No comments:
Post a Comment