Habari za Punde

Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na 

Michezo, bi Fatma Hamad Rajab ametia Saini Hati ya 

Makubaliano (MOU) na Kampuni Haryana State Electronics 

Development Corporation (Hartron) ya Nchini India, kwa 

ajili ya kuwasaidia Vijana wa Zanzibar kupata mafunzo na 

vifaa, makubaliano ambayo yamefanyika huko Ukumbi wa 

Wizara hiyo, Migombani Mjini.

 

Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Zanzibar  

imetiliana saini hati ya Makubaliano (MOU) na Kampuni ya 

Haryana State 

Electronics Development Corporation (Hartron) ya 

Maryana Nchini India kwa ajili ajili ya kuendeleza Vijana wa 

Zanzibar.


Utiaji Saini huo, umefanywa na Katibu Mkuu Wizara ya 

Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, imetiwa saini na 

Katibu Mkuu wake bi Fatma Hamad Rajab na kwa upande wa 

Kampuni ya Harton, imetiwa saini na Mkurugenzi Mtendaji 

wa Kampuni hiyo Dk. Ganesan Jagadesan.


Viongozi mbalimbali kutoka Wizara ya Habari, Vijana, 

Utamaduni na Michezo walihudhuria na Balozi wa India 

Nchini na Ujumbe wake ambao ulifanyika katika Ukumbi wa 

Wizara hiyo Migombani Wilaya ya Mjini.


Akizungumza katika Utiaji Saini wa Makubaliano hayo, Katibu 

Mkuu wa Wizara ya Habari Vijana, Utamaduni na Michezo 

Fatma Hamad Rajab amesema lengo ni kusaidia Vijana, 

kupata mafunzo ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano 

(ICT) na Vifaa mbalimbali.


Aidha amesema hali hiyo itatoa fursa mbalimbali kwa vijana 

ikiwemo kuwaunganisha pamoja, kupata ajira na kuweza 

kufanya kazi kwa Ufanisi.


Kwa uapande wake Mkurugenzi Mwendeshaji wa Kampuni 

ya Haryana State Electronics Development 

Corporation kutoka India Dk. Ganesan 

Jagadesan ameahidi kufuata maelekezo yalimo katika 

Mkataba huo wa Maridhiano ili kuwasaidia Vijana wa 

Zanzibar.

Imetolewa na Kitengo cha Habari, WHVUM.



No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.