Habari za Punde

Makamo wa Rais wa ZFA Unguja AlHajjj Haji Ameir Aifanyia tafrija Timu ya Taifa ya Zanzibar.

 Makamo wa Mwenyekiti wa Chama cha Mpira Zanzibar AlHajj Haji Ameir (Boss Mpakia) akizungumza na Waandishi wa habari na Wachezaji wa Timu ya Taifa ya Zanzibar baada ya kumaliza kupata chakula cha mchana alichowaandalia wachezaji hao nyumbani kwake, kuiaga timu hiyo na kuitakia safari njema na ushindi katika michuano ya Kombe la Chalenji yanayotarajiwa kufanyika Nchini Kenya mwishoni mwa mwezi huu. 
 Katibu wa Chama cha Waamuzi Zanzibar Issa Ahmada Jongoo, akizungumza na waandishi wa habari baada ya kumalizika kwa tafrija hiyo na kuwataka wachezaji wa Zanzibar kuwa kitu kimoja na kutojali nani hayupo katika timu hiyo. Wawe na ari ya kujituma katika mchezo wao. 
 Mjumbe wa Kamati ya Maandalizi ya timu ya Taifa ya Zanzibar Juma Sunday akizungumza katika tafrija hiyo jinsi timu ilivyojianda na michuano hiyo na kuahidi kurudi na ushindi Zanzibar.
 Nahodha wa timu ya Taifa ya Zanzibar akizungumza wakati wa tafrija hiyo walioandaliwa na Makamo wa Mwenyekiti wa ZFA Unguja Al Hajj Haji Ameir, nyumbani kwake,akitowa shukrani na kuahidi kuiletea ushindin Zanzibar katika michuano hiyo inayotarajiwa kufanyika nchinin Kenya mwishoni mwa mwezi huu.

                                     Mambo ya Biriani hayo mdau naona unajiramba hapo
Wachezaji wa Timu ya Taifa ya Zanzibar wakikata mpunga katika mnuso walioandaliwa na Makamo wa Rais wa ZFA Zanzibar Al hajj Haji Ameir nyumbani kwake na kuzungumza nao wakiwa katika maandalizi ya Kombe la Chaleji yanayotarajiwa kufanyika Nchini Kenya mwishoni mwa mwzi huu.  

5 comments:

  1. Hii ni aibu yaani makamu mwenyekiti wa zfa anaona ufahari kuwalisha biriani eti timu ya taifa ya zanzibar.kwa hili hatufiki popote ,baada ya kuwapeleka restaurant wakapata balance diet unawalisha biriani ,we are not serious ,tubadilike tuache mambo ya kizamani.hii sio timu ya jambiani.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Tujaribu kuwa ni wenye kushukuru

      Delete
    2. dah hamna like apaa hahah..jamaa wanatundika biriani na ndizi sio kazi kweli..aah kajitahid lkn sio mbaya kizenj zenj

      Delete
  2. Tuwe wenye kuwa na shukrani

    ReplyDelete
  3. Nawatakia kila laheri wakashiriki vyema na kutuletea ushindi

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.