Ndugu Wazanzibari, ndugu wageni wetu kutoka nchi mbali
mbali, mabibi na mabwana, vijana na
watoto wetu.
Asalaam
alaikoum warahamatu Allaah wabarakatuh (Meaning Peace be upon to you all.
We
equally feel honored to welcome our
guests ,brothers , sisters and friends from other communities who took their
precious time to come out and support us
tonight in this good cause - we do
say thank you very much. Asanteni sana !
We hope you will continue to repeat the
same in the near future. Also please feel free to give us your ideas, opinions
and any other valuable inputs or contributions. We are all proud to be part of
this great Canadian society.Your support is very important to us and to those whom
we are trying to help back home in Zanzibar, Tanzania.
Baada
ya kutoa salamu, sina budi kuwakaribisha na kuwapa shukrani kwa kuupokea na
kuitikia wito huu adhimu wa kuhudhuria katika mwaliko huu wa kuchangia watoto
wetu mayatima na wengine wengi sana wasio
jiweza huko visiwani Zanzibar na
kusaidia hali mbaya ya uchumi na maendeleo ya nchi yetu Zanzibar .
Kama
tunavyojuwa wengi wetu, kwamba serikali ya Zanzibar, baada ya kukaa na
kutafakari na kugundua kuwa nchi nyingi
sana duniani zimefanikiwa kwa kiasi kikubwa mno kutoka kwa
wanachi wake wanaoishi nchi za nje (Diaspora populations ) kwa kusaidia
kuingiza mamilioni ya fedha, misaada, utaalamu wao, foreign invetsments na kuanzisha biashara katika nchi zao za
asili au kuzaliwa, kuukuza uchumi wa nchi hizo na kunyayua hali za maisha ya
wanachi wao masikni na wasiojiweza kwa
kupunguza kiwango cha hali ya juu cha
umaskini na ufukara, ndio Serikali ya Zanzibar
ikaona iko haja ya kuiga mfano huo na
kutoa wito wa kuwashirikisha Wazanzibari
waishio nje ya Zanzibar ili kufaidika na
mbinu hiyo na hivyo ikaamua kuanzisha kitengo maaluum ndani ya ofisi ya
Rais wa Zanzibar ili kuchangia maendeleo
ya “Uchumi na Jamii,” ya nchi yetu ya Zanzibari
na watu wake.
Hivyo
basi, baada ya serikali kuunda kitengo hicho kwa jina la “ Diaposra Desk” chini
ya Ofisi ya Rais ya Wizara ya Nchi na Ushirikiano
wa Kimaifa Zanzibar, ilitoa wito kwa Wazanzibari walioko nchi za nje
kujikusanya na kuandaa mikakati itakayoweza kutumika kuipatia misaada Zanzibar
moja kwa moja, aidha kwa kushirikiana na taasisi nyengine za ndani ya Zanzibar au kwa
kushirikiana na serikali kwa baadhi ya sekta kubwa kubwa za uwekezaji.
Hapa
Canada wito huo ulipokewa na baadhi ya Wazanzibari waliokuwa tayari kulifanyia
kazi suala hili, walianza harakati za kujikusanya na kuunda chombo ambacho
kitawawakiliha wana Diaspora wa Wazanzibari nchini Canada na mwaka 2010 kikaanzishwa chombo chetu hiki huru
kinachojitwala wenyewe ambacho kinajulikana kwa jina la
“Zanzibar-Canadian Diaspora Association” kwa kifupi ZACADIA na kupata usajili
kwa jina la ZACADIA Foundation mnamo tarehe 12 April, 2012.
Nini
Zanzibar Canadian Diaspora Association?: Maana na Maumbile yake :Diaspora ni watu au
raia wanaoishi au kukulia nje ya nchi
yao ya kuzaliwa au ya asili. Kwa maana
hiyo Zacadia ni “outward looking International Organization” na
lengo lake kuu ni kujenga Daraja litalounganisha mataifa mawili ya Zanzibar na Canada kwa maslahi ya kuleta maendeleo ya kichumi na
kijamii kwa mashirikiano ya Wazanzibari
wa ndani ya Zanzibar na wale wanaoishi Canada.
Kwa maana hiyo mfano tofauti na Zancana
ambayo ni “inward looking local national organization”
na lengo lake kuu ni kuwasaidia Wazanzibari katika masula ya ukaazi
ya hapa Canada. Juu ya hivyo organizations zote hizi mbili zinachukua uhuru wa kuwasaidia Wazanzibari popote pale walipo mathalan Zancana kuwasaidia vile vile Wazanzibari wanoishi Zanzibar ili
kuonesha uzalendo kwa nchi yao na Zacadia vile vile tokea kuundwa kwake, mbali
na yale malengo yake mama ya kuisaidia nyumbani Zanzibar katika sekta ya “
kunyayua uchumi na jamii yetu ,” pia juhudi kubwa imefanywa kuwasaidia
Wazanzibari waishio ndani ya Canada katika kupata wepesi wa baadhi ya masuala yao
muhimu ya kiukaazi na uhamiaji .
Mpaka
sasa kuna mambo mengi ambayo Zacadia imeyafanya ili kufikia lengo lake
lakini si rahisi kuyataja hapa yote lakini baadhi yake ni haya yafuatayo :
1.
ZACADIA imeweza kusaidiana na
Benki ya Watu wa Zanzibar katika kutafuta taasisi ya huduma za fedha ili kuweza
kupata unafuu wa gharama za kutuma pesa Zanzibar. WorldRemit ni kampuni ambayo
imekubali kushirikiana na PBZ katika kuwasaidia Wazanzibari kuweza kutuma pesa
wakiwa ndani ya majumba yao kwa njia ya :online banking.
2.
ZACADIA imeweza kuwasiliana na
PBZ ili kukubali kwa wale ambao watahitaji kufungua account zao katika PBZ na
kuikubali ithbati ya ZACADIA kwa kuwagongea muhuri wa ZACADIA katika fomu zao
3.
ZACADIA imeshauriana na PBZ
kuandaa fomu maalum za wana Diaspora badala ya zile ambazo ziko sasa na ambazo
hazilingani na mazingira yetu ya huku Canada.
4.
ZACADIA imeweza kushirikiana na
PBZ na WorldRemit katika kuweza kuwarahisishia Wanaoishi nje kuweza kutumia
huduma za “online banking” ili waweze kufuatilia account na kuona harakati za
account zao wakiwa huku Canada.
5.
ZACADIA ikiongozwa na Board of Trustees na CEO wake , imeshaunda
structure yake hapa Canada, na Zanzibar.
Kulingana na mahitaji ya nchi yetu Idara kadhaa za Zacadia zimeanzishwa
zikisimamaiwa na Managers wake zikiwemo : Education, Health and Community
Safety, Business, Investment and Banking, Women and Seniors,Youth and Children,
Trade and Tourism, Fundraising and Resource Development, Spiritual Affairs, Treasury
and Administration.
6.
ZACADIA tayari imeanza kupeleka misaada mbali mbali ya wanaohitaji
kama vile nguo, vyombo vya nyumbani, baiskeli, mapipa ya kuhifadhia maji na
hata pesa taslim, kupitia mmoja wa manager wake amabye anasimamia wanawake na
wazee huko Zanzibar, picha na video za ugawaji wa misaada hiyo zitaoneshwa leo
hapa.
7.
ZACADIA imeshaandaa mradi wa
watoto mayatima ambao una lengo la kuwatafutia watoto hao wadhamini
watakaowashughulikia kwa huduma za elimu, afya, chakula bora na hata kuweza
kuwasaidia wazee wao kwa kuwapatia huduma muhimu kama vile vyakula na
kuwaelimisha namna ya kujienedeleza kwa kujitayarishia bustani zitakazoweza
kuwapatia mahitaji yao madogo madogo.
8.
Tukiwa leo hii tuko hapa,
ZACADIA inashughulikia kupeleka vitanda vya wagonjwa katika hospitali zinazohitaji
sana, na tayari vitano vinatarajiwa kufika katika kituo cha afya cha Kiwani
huko Pemba.
9.
Pia, tumeanza kuanzisha mashirikiano (patnerships)
na Jumuia mbali mbali za kijamii
zilizoanzishwa huko Zanzibar katika kuifanyia utafiti miradi ambayo inahitaji kipau
mbele katika kushughulikiwa na kufanya kazi pamoja
10.
Zacadia imeashaonana na vile
vile kufanya uhusiano na mazungumzo na
mashirika kadhaa na tumeahidiwa ushirikiano na misaada mabali mbali ili kutimiza malengo yetu. Mashirika haya
yakiwemo East African Chamber of Commerce of Canada, Rotary Club, Islamic
Relief Organization,Youth Challenge International, Zanzibar Diaspora
Association of America (ZADIA)
Fisabililah, wabunge, Zanzibar Ministries of Education, Ministry of
Health, Business and Commerce, Zanzibar Investment Promotion (ZIPA), Zanzibar
Insurance, Peoples Bank of Zanzibar, Zanzibar Trade and Tourism, Zanzibar
Social Security Fund, Zanzibar Institute of Research and Policy (ZIRP) na mengineyo .
11.
ZACADIA imeshawasiliana na
mashirika mbali mbali ambayop tayari yameonesha moyo wao wa kutaka kuisaidia
Zanzibar na karibuni mwakilishi wetu huko Zanzibar atakutana na wawakilishi wa
taasisi moja ya kimataifa ya Canada katika kutekeleza ushirikiano.
12.
Kuhusu Kadi ya
Mzanzibari Mkaazi; Zacadia imewasiliana na idara inayohusika na ushirikiano wa
Kimataifa huko Ikulu Zanzibar ili kulishughulikia suala hili kwa ajili ya wana
Diaspora. Hata hivyo, suala hili limo kufanyiwa bill yake ili liingizwe katika
Katiba kwani linahusiana na sheria na hivyo lazima kwanza lipitishwe na Baraza
la Wawakilishi. Hata hivyo, kwa kusubiri vitambulisho hivyo, serikali ya
Zanzibar kwa sasa inatoa vibali maaluum kwa wana Diaspora ili kuweza
kurahisishiwa masuala yao huko Zanzibar kuanzia Uwanja wa ndege hadi katika
masuala ya ukaazi na uendeshaji miradi yao binafsi.
13.
Zacadia imeshazungumza na
SMZ Kupata support katika mradi wowote
wa kusaidia Zanzibar ili usimbuliwe kwa vifaa na michango utayopeleka Zanzibar.
14.
Kuwapeleka vijana na watu wazima wa ki Zanzibari na nchi
nyengine kwenda kujitolea Zanzibar.
15.
Zacadia Hivi sasa tunaandaa container(s) ya kupeleka Zanzibar itakayokuwa
na vitu na vifaa mchanganyiko kwa miradi ya ZACADIA ya elimu, afya kwa watoto mayatima na wa kawaida, wazee
wasiojiweza na vijaana wasio na ajira. Kwa hili tumeahidiwa na shirika moja
kubwa kusaidiwa kulipia ushuru wa container kwenda Zanzibar hadi kiwango cha
Dola Elfu Sita.
16.
Kwa kutimiza hilo hapa juu Tumeiomba itupatie
sehemu ya kuanzisha Zacadia Community Center
in Zanzibar ili kuendesha program zetu mbali kupitia Ofisi zetu za Managers wetu wa
Unguja na Pemba.
17.
Tuna Lengo kuanzisha Umbrella Organisation ya kuunganisha Diaspora associations zote za Kizanzibari
duniani ZAIDI (Zanzibar Alliance of International Diaspora
Institutions) kuwa na sauti, nguvu na
umoja na kutafuta nyenzo/misaada za
kutekeleza malengo yetu kwa ufanisi zaidi
kwa pamoja.
18.
Kwa vile Diaspora organisation
zinaweza kuiingizia Serikali ya Zanzibar
rasilmali mbali mabli za missada yenye
thamani kubwa na vifaa vya aina mbali mbali
kutoka nchi za nje ikiwemo Canada
kama vile nchi nyengine duniaini zinavyofaidika, tunaishauri serikali ya Zanzibar ianzishe Zanzibar Diaspora Institute in Zanzibar
ili itoe utaalamu na elimu ya hali ya
juu katika mambo na masuala ya Diaspora kwa
idara, wizara, watu, jumuiya za ndani na nje ya Zanzibar ili ziweze
kufanikiwa kuleta utendaji na tija kwa
nchi yetu na watu wetu na kupata misaada
nchi za nje.
19.
Kwa vile Zacadia ni international organisation
inayohusisha utaifa wa Zanzibar hapa Canada, Zacadia imeweza kuwasaidia Wazanzibari katika masula
na matatizo ya Immigration na ukaazi na kuthibitisha identity na sifa za Wazanzibari
wenzetu kwa aajili ya maombi mbali mbali.
20.
BAADA YA MAELEZO
MAFUPI TUNAWAOMBA NYOTE
BILA KUJALI JUMUIYA ULIYOTOKA KUJIUNGA NA SISI KUYATIMIZA MALENGO HAYO
KWANI WITHOUT YOU, YOUR FAMILY MEMBERS AND SOCIAL NETWORKS
KUNA HATARI YA KUZIDIWA NA KAZI HII NZITO AMBAYO JAZA YAKE ITATOKA KWA
ALLAAH SUBHANAHU WA TAALA.
Kuna
mambo mengi mengine ya kuzungumza lakini wakati hauturuhusu, kwa hiyo mikutano
ya aina hii itazidi kufanyika na ni matumaini yetu kwamba baada ya kusikia haya
machache, itakuwa ni changamoto ya kuzidi kushiriki katika kuichangia ZACADIA
ili iweze kufikia malengo haya. Timu yetu ni ya kujitolea na hakuna
anayetarajia cho chote kutoka mfuko wa maendeleo wa ZACADIA, bali tunamtegemea
Allaah kupata malipo kwa kuwasaidia ndugu zetu walioko katika shida huko
Zanzibar.
Kwa
haya machache, ZACADIA INAWASHUKURU SANA
kwa kufika kwenu na kuweza kusaidia
kuwachangia watoto wetu waliopoteza wazee wao kwa njia tafauti ikiwa ni pamoja
na wale waliopotea kwa kuzama kwa meli iliyopoteza roho kadhaa na kuachwa
mayatima kadhaa na vile vile kuwasAadia mamia ya ndugu zetu wa kila umri wanaoteseka katika maisha yao ya kila siku huko nyumbani Africa.
ZACADIA IS THINKING BIG…
Ahsanteni
Mungu
awabariki nyote muliohudhuria na chi zenu pia kwa kutuunga mkono
Mungu
ibariki Zanzibar na Watu wake
Mungu Ibariki Canada –Amin
Hongereni zcadia mmeonesha moyo huko tunako toka waznz, wingi waliyo pata bahati ya kukimbia haya mazila ya hapa znz wamejisahau, hawakumbuki kama kuna nduguzao na wa zee wao wako kwenye, mazila walotiwa na waafrika wenzao
ReplyDelete