عَنْ ابْنِ عَبَّاسٍ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُمَا
قَالَ : مَا رَأَيْتُ النَّبِيَّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَتَحَرَّى
صِيَامَ يَوْمٍ فَضَّلَهُ عَلَى غَيْرِهِ إِلّا هَذَا الْيَوْمَ يَوْمَ
عَاشُورَاءَ وَهَذَا الشَّهْرَ يَعْنِي شَهْرَ رَمَضَانَ . " رواه البخاري
1867
Kutoka kwa Abdullah ibn ‘Abbaas,
Allaah awawie radhi yeye na baba yake, amesema:
Sijapatapo
kumuona Mtume Swalla Allaahu ‘Alayhi
Wasallam akiwa na hamu na shauku ya kufunga katika siku aliyoifadhilisha kuliko siku nyengine
isipokuwa siku ya ‘Aashuuraa na mwezi huu yaani mwezi wa Ramadhaan. Bukhaari 1867
Mtume Swalla Allaahu ‘Alayhi
Wasallam ametuhimiza waislamu kuifunga siku hii muhimu katika dini yetu kwani
kufunga siku ya ‘Aashuraa ambayo ni tarehe 10 Muharram (Mfunguo nne) Allaah
Subhaanahu Wata’ala hutusamehe madhambi yetu madogo madogo ya mwaka mzima uliopita.
Hii ni siku ambayo Allaah
Subhaanahu Wata’ala alimuokoa NabiyuLlaahi Mussa ‘Alayhi Ssalaam, kutoka katika
mikono ya Fir’aun aliyelaaniwa.
Ikiwa Mtume Swalla Allaahu ‘Alayhi
Wasallam ameonesha hima na hamu ya kufunga katika siku hii je mimi na wewe?.
Hivyo tuungane na Mtume wetu Swalla Allaahu ‘Alayhi Wasallam katika kuhakikisha
tunaifunga siku hii ya ‘Aashuuraa kwani huko ndiko kufuata mafundisho na
maagizo ya Ruwaza wetu , Swalla Allaahu ‘Alayhi Wasallam na kutekeleza Sunnah
zake alizotuachia.
No comments:
Post a Comment