Habari za Punde

Mambo ya Soko la Samaki Zenj

Wachuuzi wa Samaki katika Marikiti Kuu ya Darajani wakichuna ngozi ya Samaki aina ya Chewa aliyevuliwa katika ukanda wa Pwani ya Nungwi, na kufikishwa katika mnada huo na kuuzwa kwa shilingi laki mbili na nusu, Ngozi hiyo huchunwa na kuuzwa kwa Wachina baada ya kukauka kwa kilo moja huuzwa karibu shilingi laki mbili za kitanzania   

5 comments:

  1. Umefika wakati wa kuondokana na tabia ya kutupa samaki chini. Masoko yetu yaondokane na tabia hii isiyopendeza.

    Haji Rajab Haji. USA

    ReplyDelete
  2. Hivi jamani hebu tujiulize sisi wanzanzibari, pamoja na kuwa na uzoefu wa kufanya biashara kubwa na ndogo kwa karibu karne tano sasa, hivi tunashindwa nini kuweza mazingira safi na ya kupendeza katika biashara zetu. Hivi kweli hatuoni? hatuhisi? Hatujuwi?? kama mazingira haya machafu ya kufanya kbiashara mbali na kuleta hofu wa maradhi kwa walaji wa bidhaa zenyewe lakini pia hutoa picha halisi ya sisi tulivyo, (yaani ni watu wachafu). Hivi tunatoa ujumbe kwa wageni mbalimbali wanaotembelea mji wetu hasa hapo Darajani.? Tujirekebishe jamaani!!!!!!!!

    ReplyDelete
  3. Shame, shame on us (wazanzibari), mazingira mabovu na machafu ya kufanyia biashara. Hivi wahusika wa masuala ya vyakula na mazingira hawapo? viongozi wa serikali hawaoni. Darajani ni uso wa mji wa Zanzibar, kila ajae Zanzibar lazima apite Darajani. Hii inatoa taswira halisi ya sisi tulivyo. NI watu tusiojali usafi wa mazingira. Aibu kubwa kwetu, hasa ukizingatia kuwa majority ni waislam, na kwa mujibu wa hadithi ya mtume " Uislam ni usafi......." Kinachotushinda mimi sikielewi hadi kufika kuuza samaki chini kabisa. Ukienda pale Malindi soko la Samaki, utakuta soko ndani halina wauzaji wa samaki, liko empty kabisa watu wanauza samaki nje tena katika mazingira ya ajabu. Jamani tubadilike hebu,
    Abu India

    ReplyDelete
  4. He jamani Zanzibar tupo karne ya ngapi??? Hadi leo tunauza bidhaa kama samaki chini. Sijui tumesibiwa na nini. Ukienda Nungwi, utaona watu wameacha soko jipya zuri kabisa wanafanya mnada wa samaki chini mkungu chini kabisa kwenye michanga, ukienda Malindi utakuta watu wametoka ndani ya soko zuri jipya kabisa wanafanya biashara nje, ukija hapo Darajani (Zanzibar Down Town) ndio hiyo picha tunayoiona. Hivi tuna nini wazanzibari. Hawa Manispaa hawapo?? Mimi sioni mantiki ya kuwaondosha wauza biashara ndogondogo (juakali store) na kuwaacha hawa wanaouza samaki chini, uchafu mtupu. Kama kuharibu haiba ya mji basi hawa nao wamo. Manispaa , hebu jikurupusheni kidogo, inatia aibu hasa ukiwa na mgeni, fedheha hata kumepeleka sokoni wallahi.

    ReplyDelete
  5. Aibu, kwanini tufanye biashara chini?? mimi namuombwa bwana Othmani Maulid, pamoja na juhudi kubwa za kutujuza habari mbalimbali kupitia blog hii, tunaomba ufanye juhudi za makusudi za kuziweka au kuwafikishia wakubwa wa nchi picha kama hizi, huenda wakawa hawajui kwamba kuna mazingira kama haya (machafu) huenda wakazinduka na kutoa makaripio yenye faida kwa jamii

    Mdau wa mazingira, Zanzibar

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.