Habari za Punde

Naibu Kadhi afungua Madrasah Amir Bweleo

 Jengo jipya la Al-Madrasat Amir lililofunguliwa leo na naibu Kadhi Mkuu wa Zanzibar katika kijiji cha Bweleo Wilaya ya Magharibi Unguja.

Mkuu wa Madrasa za Unguja na Pemba Shekh. Khamis Abdulhamid akitoa nasaha kwa wanafunzi kabla ya ufunguzi wa Al-Madrasat Amir katika kijiji cha Bweleo Wilaya ya Magharibi Unguja.


Naibu Kadhi Mkuu wa Zanzibar Shekh. Hassan Othman Ngwali akikata utepe kuashiria ufunguzi wa Al-Madrasat Amir iliyopo Bweleo Wilaya ya Magharibi Zanzibar.
(Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar).
Na Miza Kona  Maelezo Zanzibar   
Vijana wametakiwa kushikamana na kujikuza kwenye ukweli ili wapate kuongoka katika maisha yao ya dunia na akhera .
Hayo yameelezwa leo na Naibu Kadhi Mkuu Shekhe Hassan Othman Ngwali wakati alipokuwa akifungua madrasa Amir ya Bweleo.
Amesema kuwa ukweli na uaminifu ndio unaomkuza mja kuongoka katika misngi iliyomema na kuachana na tabia mbaya inapelekea kujiingiza katika vikundi viovu.
Aidha amesema vijana wakijitahidi kujifunza katika misingi ya dini na kishirikiana katika ukweli na uaminifu na kuyafanyia kazi wataweza kuepukana na vishawishi vibaya na kuogopa kufanya maovu. 
 Aidha amewasitiza vijana kusoma kwa bidii na kuacha kufanya mchezo katika kutafuta elimu ili wasije kuijutia baabae.
Hata hivyo amewataka vijana hao kufufuata mwenendo wa Mtume SAW ili kuweza kuendeleza mbele dini ya kiislam.
Aidha amewahimiza wazazi kuwakuza watoto wao katika misingi ya kiislamu kwa kuitafuta elimu hiyo kwani vijana ndio taifa la kesho na kupata viongzi wazuri wa baadae.  
Aidha ameuomba uongozi wa madrasa hiyo kuwa na umoja,  imani na kujiepusha na  makundi kwa kuwa na maamuzi ya pamoja  ili ipate kuendelea vizuri na kuongeza watoto wenye misingi ya dini na imani.
Zaidi ya shilingi milioni 20 zimetumika hadi kukamilika ujenzi wa madrasa hiyo ambayo yenye madarasa manne.


No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.