Na Khamisuu Abdallah
WAJUMBE wa Baraza la Wawakilishi wameiomba Serikali kuhakikisha kifaa
cha DNA kinapatikana ndani ya muda mfupi kwa lengo la kuondoa changamoto
iliyokuwepo sasa kwa kukosekana kwa kifaa hicho
ambapo kesi nyingi za udhalilishaji hazipatiwi ufumbuzi.
Hayo yameelezwa na Mwakilishi wa viti maalum ambae pia ni Mwenyekiti
wa Baraza la Wawakilishi Mhe: Mgeni Hassan Juma wakati akifanya majumuisho ya
hoja binafsi aliyoiwasilisha barazani hapo.
Aidha alisema wajumbe hao walipendekeza kutokana na kuongezeka kwa mimba za utotoni
kifaa hicho kitaweza kusaidia kuwatambua
wahusika wa matukio hayo bila ya usumbufu wa aina yoyote.
Aidha Mhe. Mgeni alisema wajumbe hao walisema suala la rushwa ndilo
linachangia kwa kiasi kikubwa katika kuendeleza vitendo hivyo ndani ya jamii na
watahakikisha kushirikiana kwa pamoja ili kuhakikisha swala hilo linapigwa vita
na kupatikana haki ya kisheria.
Alisema wajumbe hao pia
walipendekeza sulala la udhalilishaji lisiachiwe serikali pekee na badala yake
wajumbe, taasisi mbalimbali zina uwezo wa kupeleka miswaada barazani ambayo
itaweza kuisaidia serikali katika kulifanyia kazi swala la udhalilishaji hapa
nchini.
Hata hivyo wajumbe hao walipendekeza azimio namba 7 kuwa serikali ifanyie mapitio sheria ya mtoto kwa
utekelezaji wa hoja za jamii kwa matatizo ya watoto yanayowakwaza ili vitendo
hivyo viweze kuondoka hapa nchini.
Wajumbe hao walisema suala la upatanishi linalofanywa na wazee pamoja
na wafanyaji wa vitendo hivyo katika kumaliza kesi kwa kumalizana wenyewe bila kufika katika vyombo
vya mahakama watu wamelipiga vita na
kuomba kuwekwa kwa sheria maalum ambayo itamchukulia hatua mzee yoyote
atakaepinga sheria hiyo.
Alisema kuwa katika majumuisho hayo pia wajumbe hao walipendekeza
kuingizwa kwa elimu ya udhalilishaji katika mitaala sambamba na kuelimisha
jamii juu ya mambo hayo.
Hata hivyo wajumbe hao waliiomba Serikali kundosha vipindi
vilitakavyoweza kuondoa maadili kwa wazanzibari hasa kwa watoto katika
televisioni na redio.
Sambamba na hayo alisema
wajumbe hao waliiomba serikali kutoa ripoti ya udhalilishaji kwa kila
mwaka ambapo itawasilisha kutoka Wizara ya Ustawi wa jamii vijana na watoto.
Pia wajumbe hao waliiomba serikali kuziimarisha mahakama kwa kuzitilia
mkazo kesi za watoto kwa kusikiliza kwa muda mfupi.
wajumbe wote walimunga mkoni mazimio yote ambapo azimio moja kuwepo
kwa vikao kati ya mwanasheria mkuu waziri wakatiba na sheria ili kuweka
No comments:
Post a Comment