Na Mwandishi Wetu.
BOTI ya abiria ya Kilimanjaro II yanusurika kuzama katika
mkondo wa Nungwi wakati ikitokea kisiwani Pemba na kuelekea kisiwani Unguja.
Akisimulia chanzo cha ajali hiyo
shuhuda mmoja ambae ni miongoni mwa wasafiri waliokuwemo ndani ya boto
hiyo,Sleiman Mohammed Said alisema wakati walipofika maeneo ya Nungwi hali ya hewa ilibadilika na
bahari kuwa na mawimbi makubwa.
Alisema boto hiyo ilipingwa na wimbi
zito na hatimae kusababisha kuingia maji ndani ya boti hilo na baadhi ya
abiria na mizigo kuburuzwa baharini.
Aidha alisema kutokana na ukali wa
mawimbi hayo hivyo mashine ya boto hiyo ilizima moto kwa muda,hali ambayo
ilizidisha taharuki na hofu kwa abiria waliokuwemo ndani ya boti hiyo huku
wachache kukimbilia ndani.
"Baadhi ya watu waliokuwa
wamekaa mbele ya boti hiyo wametumbukia baharini na baadhi ya mizingo mimi
nilikuwa na ndugu zangu wawili tumekaa pamoja mpaka sasa sijawaona na hadi boti imeshusha abiria wao hawamo"alisema
Sleiman.
Hata hivyo alisema mara tu ya kuwaka
kwa mashine boti iliendelea na safari.
"Ilivyowaka mashine boti ile
ilifanya safari na haikurejea nyuma kwa ajili ya kufanya utaratibu kwa wale
abiria walioingia baharini lakini walituwahisha sisi"alisema
Naye Ali Pandu mkaazi wa Mtoni ambae alifika bandarini hapo kwa kutaka kujua
hatima ya ndugu zake wawili aliowataja kwa jina moja Nahiri(17) na Ali(19)
ambao walikuwa wamesafiria boti ya
Kilimanjaro II, alilieleza gazeti hili kwamba hawaelewi kama wapo hai au
wameshafariki kwani inasemekana hawakuwemo ndani ya boti hilo baada ya kutokea
tukio hilo.
"Hawa jumla yao walikuwa watatu
mwenzao mmoja yupo lakini na yeye anasema baada ya kutokea kwa tokeo hilo
hakuwaona wenziwe mpaka sasa na walikuwa wamekaa mbele"alisimulia.
Kwa upande wa mwananchi Abdalla
Mohammed ambae watoto wake walikuwemo katika bato hiyo alisema mnamo majira ya
saa mbili hadi tatu alipokea simu kutoka kwa mtoto wake Mohammed Abdalla(17)
ambapo alimueleza kwamba hali iliyowafika katika safari yao.
Alisema baada ya kupata simu hiyo
alijaribu kuwapigia tena simu lakini alikosa mawasiliano yoyote kutoka kwa
watoto wake hadi anazungumza na gazeti hili.
"Watoto wangu walinipigia simu
wakanambia baba tunazama tunakufa sisi"alisema mzee huyo.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa
Mamlaka ya Usafiri Baharini Abdi Omar alikiri kujitokeza kwa msukosuko wa
mawimbi baharini na kusababisha kupotea kwa baadhi ya abiria na mizigo.
Alisema bado hawajakuwa na taarifa
kamili ya abiria waliopotea lakini hata hivyo wamekatika utaratibu wa kuelekea
eneo la tukio kwa ajili ya kusaka abiria pamoja na mizingo.
Mwenyezi Mungu awape subra wafiwa. Ni kazi yake Mungu haina makosa.
ReplyDeletena bakharesa nawe viboti vyako vidogo sana yakhe
ReplyDelete