Habari za Punde

Mchezo wa Nusu Fainal KCCA imeshinda 3--2 dhidi ya Azam

Mchezaji wa timu ya Azam na KCCA wakiwania mpira katika mchezo wa Nusu Fainali ya Kombe la Mapinduzi timu ya KCCA imeshinda 3--2
Hapa hupiti ndivyo inavyoonekana beki huyu wa timu ya Azam akimuekea mwara mchezaji wa timu ya KCCA. 


Rais Mstaaf Mzee Ali Hassan Mwinyi akifuatilia mchezo wa Nusu fainali kati ya Azam na KCCA ya Uganda uliofanyika uwanja wa Amaan, timu ya KCCA imeshinda kwa mabao 3--2 


Wachezaji wa timu ya Uganda ya KCCA ikishangilia bao lao la tatu na laushidhi dhidi ya Azam wakati wa mchezo wa Nusu Fainali ya Kombe la Mapinduzi. mchezo uliofanyika uwanja wa Amaan. 

Kocha wa timu ya Azam akiwa hatulii katika benchi baada ya timu yake kuongoza na kuzawazishiwa na kufungwa bao la tatu na kutolewa na katika michuano hiyo ambayo timu ya ilikuwa Bingwa Mtetezi.

 


2 comments:

  1. Hapa sijafahamu hebu tupatie habari kwa ufasaha kwa uandishi Wako ni kwamba Azam imeshinda?

    ReplyDelete
  2. Binafsi nimependa picha unazoweka kwenye blog yako hii.hususan picha za mpira.
    nimekuwa nikizifuatilia na bila ya kuficha ni picha zinazoonyesha zinapigwa na mtu mwenye kujuwa na kupenda akifanyacho.
    Ningependelea zaidi kama upo uwezo basi ungetumia wide apperture lens.kama 2.0 au kubwa yake .ili kutupatia uhondo zaidi sisi wapenzi wa blog yako.
    ahsante.

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.