Habari za Punde

Mapinduzi Cup Ashanti ya Tanzania na Tusker ya Kenya


              Wadau wa habari wakiwa na Waziri wa Michezo wakifuatilia michuano ya Mapinduzi Cup.
Mshambuliaji wa timu ya Ashanti akijaribu kumpita beki wa timu ya Tusker, katika mchezo wa Kombe la Mapinduzi.
                        Beki wa timu ya Ashanti akimkata mtama mshambuliaji wa timu ya Tusker

Mchezaji wa timu ya Tusker kushoto na wa Ashanti wakiwania mpira katika mchezo wa Kombe la Mapinduzi.
          Mshambuliaji wa timu ya Tusker akikokota mpira kujaribu kumpita beki wa timu ya Ashanti.
                                                                              Kazi kweli hapa
 Kocha wa timu ya Ashanti Abdalaa Kibadeni akiwa hatulii katika benchi akitowac maelekezo kwa wachezaji wake wakati wa mchezo wao wa kwanza wa michuano ya Mapinduzi Cup wamechukua nafasi ya Darv Young African iliojitowa katika michuano hiyo, ya kuadhimisha miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar.

 Benchi la wachezaji wa akiba wa timu ya Tusker wakifuatilia mchezo wao na Ashanti akiwa hawaamini matokeo hayo ya ushindi finyu.
 Mshambuliaji wa timu ya Tusker akimpita beki wa timu ya Ashanti ya Tanzania katika mchezo wa Mapinduzi Cup yanayofanyika katika uwanja wa Amaan usiku huu.
Mshambuliaji wa timu ya Ashanti akimpita beki wa timu ya Tusker ya Kenya katika mchezo wa Mapinduzi Cup, uliofanyika usiku huu katika uwanja wa Amaan, timu ya Tusker imeshinda. 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.