Habari za Punde

Foleni katika barabara ya michezani kituo cha daladala.

 Zanzibar ni Njema Atakae Aje,mji wa Unguja unazidi kukuwa kwa kuengezeka kwa magari na kusababisha kuongezeka kwa foleni barabarani kama inavyoonekana barabara hii ya michezani kuwa na foleni kubwa ya magari kuelekea Michezani  

4 comments:

  1. Kwa sisi wajinga, limbukeni, na serikali isiokua na ushirikiano na Wapinzani wake katika kuimarisha na kuongeza barabara za kisasa ..tunaona wingi wa magari ni utajiri... kumbe ni kuzidisha Corbon immunation na global warming ambazo zinasababishwa na Conjuction... Nchi haina mpango mpya wakupanua barabara au kujenga barabara nyengine ambazo zingepunguza msongamano..hii nikwasababu CCM Seifu Ali Iddi ndie anae amua nini wazanzibari wapatiwe... Kisiwa cha unguja kimepoteza haiba ya pepo za bahari ambazo tlikua nazo miaka ya 70-90..sasa ni humidy, joto, na maskani kujengwa mpaka barabarani... Kisiwa kinavamiwa na wageni na wimbi la immigration bila yakumjua anaeingia hukaa wapi na siku ngapi... wengine wanapewa kipa umbele kuliko wenyeji..na ajali zinaongezeka kutokana na uongozi mbovu wa ccm smz

    ReplyDelete
  2. Well! nakubaliana nawe mdau kwa mengi uliyoyasema ya muelekeo wa kuifanya zanzibar nusu pepo.Waonaje chini ya kipengele kipya kijacho cha katiba cha mgombea wa kujitegemea ukajitokeza kugombania nafasi ya Uraisi. Najuwa utashinda kwa mawazo ya busara kama haya vyenginevyo mie nakusihi yaachie tu mana hakuna wa kukusikiliza..

    ReplyDelete
  3. Assalaam alaykum. Mimi naona pamoja na hilo ongezeko la magari, lakini haijafikia Zanzibar tuwe na msongamano wa hiivyo kutokana na ongezeko la magari. Tatizo ni lile lile hatuna town planning, mji umejengwa ovyo kabisa na unaendelea kujengwa ovyo kila kukicha. Hivi umeona wapi kituo cha magari ya abiria kikwawekwa barabani kabisaa. Hivi unategemea nini zaidi ya msongamano hata kama utakuwa na magari 100 tu basi msongamano utakuwwepo.
    Jamani hebu tujirekebishe,, tuupange mji wetu, tuwe na town planning na tuzifuate, tuongeze barabara za ndani ya mitaa, tutanue zilizopo. Inasikitisha kweli kwamba mpaka leo Zanzibar hatuna hasa pahala pakutambulika panapostahiki kuitwa MJI au JIJI, aibu aibu, ukija na mgeni wako Zanzibar kwa kweli ni aibu tupu. Kama si huo mji mkongwe sijui hata tungeziweka wapi sura zetu, na huo mji mkongwe una sifa kwa hiyo hadhi yake ya ukongwe tuu, lakini vyenginevyo ni aibu sana Zanzibar hatuna Mji kabisaa.
    Kuna rafiki yangu mmoja alitembelewa na marafiki zake kutoka Marekani/Ulaya, akenda kuwapokea airport, moja kwa moja akaelekea nao hapo tunapopaita "mjini" maeneo ya Darajani, Stone town n.k baadae wakawapeleka kwake MOmbasa, baada ya muda wale wageni wakamwambia Jioni watataka wakatembee mjini wakaone mandhar ya Mji wa Zanzibar, akaanza kujiuliza hawa wanataka mji gani tena mjini si tayari tumerudi, akabaki hajui la kufanya.
    Zanzibar tunahitaji Mabadiliko ya mindset zetu fikra za viongozi tulionao naona zimefikia ukomo au ubinafsi mwingi. Mtu akishaona yeye ana PRADO zuri anakula vizuri yeye na watoto wake, ana ushirika katika Hoteli fulani za kitalii na wageni basi hajali chochote, watu wakifa njaa, wakipata taabu barabarani, hashughuliki kabisaa yake yanamwendea na akistaafu ana mamilioni ya fedha na huduma pamoja na ulinzi. Hana habari na shida na kero za watu, hivyo ndivyo tulivyo Zanzibar. Tunahitaji mapinduzi mengine si ya kumuondoa mtawala bali ya kifikra.

    Namuomba ndugu Othman: Hebu jaribu kuifanyia modification kidogo hii blog yako kwa kututengenezea "Forum" fulani ndani hii blog yako ili tukaweza kujadili na kutoa mawazo yetu kuhusu maendeleo ya nchi yetu ya Zanzibar. Yaani utuwekee topic zihusuzo Maendeleo tuu sio za KIsiasa maana Wazanzibar kwa siasa (kama tumerogwa vile), sisi wengine ni wakerekwetwa wa maendeleo ya nchi yetu tunaona choyo tunapokwenda nje ya Zanzibar na kukuta wenzetu wanakwenda mbele sisi bado tunarudi nyuma. Tunashindwa hata kuwa na mabustani ya maaana katika mji wetu licha ya kuwa ardhi yetu ni kama dhahabu, wenzetu wanatenegeza mabustani kwenye ardhi ya majangwa kabisa na miji yao inapendeza.
    Kwa hiyo ombi langi Sheikh Othman tuwekea mada za kujadili kuhusu maondeleo, mfano uboreshaji/utengenezaji wa miji yetu, utengenezaji wa mabustani katika miji, barabara za ndani ya mji na mfano wa huo.
    Nakutakia kila la kheri katika hili nikiamini utafanikisha wala usiwe na khofu labda watu watashambulia serikali, laa hasha, sometime lazima ukosolewe ndipo uweze kujirekebisha kwani hakuna mkamilifu serikali inahitaji michango mbali mbali ya kifikra kutoka kwa watu raia zake mbalimbali.
    KIla la kheri, Mungu ibariki Zanzibar na watu wake amiiin.

    ReplyDelete
  4. Assalam alaykum.
    Zanzibar hakujakuwa na magari mengi ya kufanya msongamano.
    Ila tu ni ukosefu wa mpangilio wa mji.
    Hizo barabara za michenzani ni pana za kutosha kuwa na njia 3 (three lanes) hii inatosha kwa magari kutembea vizuri.
    Pia hili round about ni pana sana kiasi kwamba hata kama kuna three lanes basi hapo kwenye round about huwezi kuzipata hizo lane tatu.
    Na hichi kituo cha madaladala viereje kuwekwa njiani ? Hii inafanyika nchi zilizoendelea lakini ni kwa kushusha na kupakia tu sio kusubiri , tena huwa njia imeingia kwa ndani kidogo kufanya kijia pembeni kidogo na hizo barabara kuu.
    Pia madereva wajifunze uzuri jinsi ya kutumia round about , unamkuta dereva anatumia muda kuingia na kutoka round about na kufanya walio nyuma kusubiri.
    Na pia madereva wakipewa leseni wakifanya mitihani ya vitendo (practical test ) wasitihaniwe jinsi ya kujuwa kudhibiti gari tu katika uendeshaji ila na usalama (safety ) pia katika uendeshaji. Road scanning ya madereva wengi ni mbaya sana .
    Pia wapanda wa vyombo vya maringi mawili , baskeli ,pikipiki , wapewe umuhimu , katika highway code wanahaki ya kujaaliwa kama gari ili wapewe nafasi ya kutosha wakati wa kuwa overtaken.

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.