Habari za Punde

Wizara yakana Wabunge kulipwa 160m/-

Na Mwandishi wetu
WIZARA ya Fedha na Uchumi imekanusha taarifa za vyombo vya habari kwamba waziri wa wizara hiyo ameidhinisha ongezeko la malipo ya pensheni ya Wabunge hadi kufikia shilingi milioni 160 baada ya kustaafu.
Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu wizara hiyo, Ramadhan Mussa Khijjah, alisema taarifa hizo ni za upotoshaji zenye lengo la kuwachonganisha Wabunge na wananchi wao.
Taarifa hiyo imesema waziri hajawahi kuzungumza na mwandishi wa habari yeyote kuhusu suala la nyongeza ya pensheni ya Wabunge na maelezo kwamba alithibitisha taarifa za ongezeko hilo sio na kwamba suala hilo halipo serikalini wala bungeni.
Taarifa hiyo iliwataka waandishi wa habari kufanya kazi kwa kuzingatia maadili ya taaluma yao.


1 comment:

  1. bwana waziri usifikiri kuwa utaishi milele , usiseme uwongo, wanasiasa mnapendeleana , mnawanyonya wananchi wakati nyinyi mnapeana mishahara minono nk usiwaambie waandishi waangalie maadili wakati nyinyi hamna hata adili moja achilia mbali maadili

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.