Habari za Punde

BREAKING NEWSS::MADEREVA WA BODA BODA NA BAJAJ WAANDAMANA MPAKA OFISI ZA CHADEMA KINONDONI,WAKIPINGA KUZUIWA KUINGIA MJINI

Madereva Bajaj wakiwa nje ya ofisi za chadema makao makuu kinondoni wakipinga tamko la kuzuiwa kuingia kati kati ya mji na maeneo ya mjini.



 Mmoja wa Madereva Bajaj Akiongea na vyombo vya habari mda huu makao makuu ya chadema kinondoni.
Polisi wakiwa wamefika eneo la tukio muda mfupi ili kuweza kuweka hali ya amani na  usalama ili kuzuiya vurugu

 Waendesha bodaboda na bajaj jijini dar mda huu wameandamana mpaka Ofisi za chadema makao makuu kinondoni ,Nia ya maandamano yao hayo ni kupinga tamko linalowataka kutopeleka abiria maeneo yote ya kati kati ya jiji la dar.Mmoja wa madereva hao akiongea na mtandao wetu anasema kwamba wameamua kuandamana mpaka ofisi za chadema kwa kuwa wanaamini ndio watapata msaada.Taarifa kamili na picha zaidi zitakujia inakujia hivi punde.HABARI NA DJ SEK BLOG

2 comments:

  1. Sawa kabisa, bajaj na boda boda wasiende katikati ya mji, wanasababisha ajali, kwa uendeshaji wao wa hovyo!

    ReplyDelete
  2. Naamini kabisa ili kuwa na amani, utulivu na usalama, bodaboda na bajaji zisiingie mijini; sio tu katika jiji la Dar bali pia miji YOTE ya Tanzania. Serekali isiyumbishwe kwa maandamano hayo.

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.