MWENYEKITI wa
kikundi cha ‘Jambo Group’ cha shehia ya Wambaa Mkoani Pemba, Hafidh Juma Ali,
ambacho hivi karibu samaki wao zaidi ya 200 walikufa kutokana na kuingia na
maji ya mvua, akiwaonyesha waandishi wa habari bwawa lao la kufugia samaki (picha na Haji Nassor, Pemba)
MKULIMA wa bonde
Vualeni Wilaya ya Micheweni Pemba, Fatma Issa akivuna mpunga katika bonde hilo,
ambalo walilihama kwa miaka zaidi ya 20, kutokana na kuingia maji ya chumvi,
ambapo mwaka juzi walijengewa tuta la kuzuia maji hayo (kinga maji) na mfuko wa
maendeleo ya jamii Tanzania TASAF, awamu ya pili (picha na Haji Nassor, Pemba)
WANAKIKUNDI cha
kutengeneza bidhaa za usumba kilichopo Wingwi njuguni wilaya ya Micheweni Pemba,
wakiwa kazini kuchambua sumba kabla ya kuipeleka kwenye kiwanda chao kwa ajili
ya kutengeneza kamba na bidhaa nyengine (picha
na Haji Nassor, Pemba)
No comments:
Post a Comment