Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba Mufti, Sheikh Thabit Noman Jongo akiongoza dua ya asubuhi ndani ya ukumbi wa Bunge leo Mjini Dodoma.
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba Askofu Mstaafu Donald Mtetemela akiongoza sala ya asubuhi ndani ya ukumbi wa Bunge leo Mjini Dodoma.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Mizengo Pinda akiwaeleza jambo wajumbe wa Bunge maalum la Katiba Edward Lowassa (mwenyeshati Jeupe) na Philemon Ndesamburo, Ndani ya Ukumbi wa Bunge leo Mjini Dodoma.
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba ambaye pia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Mahusiano na Uratibu Steven Wassira akiwaeleza jambo wajumbe wenzie Bi. Anna Makinda ambaye pia ni Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Richard Ndassa ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Sumve, kabla ya kuingia katika Ukumbi wa Bunge leo Mjini Dodoma.
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba ambaye pia ni Waziri wa Ujenzi John Magufuli akimweleza jambo Mjumbe mwingine ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Ubungo Bw. John Mnyika Mapema leo Mjini Dodoma.
Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba Bw. Ismail Aden Rage (mwenye kanzu) na Hashim Rungwe wakielekea katika ukumbi wa Bunge mapema leo Mjini Dodoma
wanasiasa ni watu wa ajabu sana, aina ya ndumilakuwili , husema watu wasichanganye dini na siasa , lakini wao wanaruhusiwa kuchanganya siasa na dini , sijui tuwaelewe vipi. Tunaambiwa serikali yetu ni ya kisekula lakini ukiingalia unaona wazi imebeza upande mmoja sina haja kutoa mifano , mwenye macho haambiwi atazame , kuna kundi la kidini limetoa waraka linalojiona lina wadhifa katika nchi kama vile hii nchi ni ya dini moja , msifanye hivyo ndugu zangu tutafika mahali pabaya tuumizane bure kwa faida ya wachache , tutatumbue nchi hii ni ya makabila, rangi na dini tofauti ingawa serikali na vyombo vyake vyote na mawizara na mashirika yake yote yamebeza upande mmoja wa dini , hali hii inatakiwa kurekebishwa ili tuepuke matatizo yanayowakuta wenzetu
ReplyDelete