Habari za Punde

Kutoka Bungeni la Katiba asubuhi Mjini Dodoma


 
  Wabunge wa Bunge Maalum la Katiba wakitoka Bungeni Mjini Dodoma leo baada ya Bunge hilo kusitishwa  kwa muda kufuatia Sintofahamu iliyotokea.
  Katibu wa Bunge Thomas Kashilillah akitoa maelezo kwa Waziri Mkuu Mizengo Pinda  pamoja na Waziri  wa Nchi,Ofisi ya  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mohammed Abood, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Stephen Wasira,  Waziri wa Katiba na Sheria  wa Zanzibar,  Abubakar  Khamis Bakari  na Mwanasheria  Mkuu wa Tanzania, Frederick Werema. 
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Idd  (wapili kushoto) wakijadili jambo na wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba baada ya Bunge hilo kusitishwa kwa  muda leo kufuatia sintofahamu ilitokea. Kutoka kushoto ni Katibu wa Bunge Thomas Kashilillah, Waziri  wa Nchi,Ofisi ya  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mohammed Abood, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Stephen Wasira,  Waziri wa Katiba na Sheria  wa Zanzibar,  Abubakar  Khamis Bakari  na Mwanasheria  Mkuu wa Tanzania, Frederick Werema. 
 Mjumbe wa Bunge Maalum la katiba Mhe Halima  Mdee   akitafakari baada ya wenzake kuondoka bungeni wakati Bunge hilo lilipositishwa  kwa muda mjini Dodoma leo  kufuatia sintofahamu iliyokea.
 Mjumbe wa Bunge Maalum la katiba Mhe Halima  Mdee   akitafakari baada ya wenzake kuondoka bungeni wakati Bunge hilo lilipositishwa  kwa muda mjini Dodoma leo  kufuatia sintofahamu iliyokea.
 Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba,Mhe. Ole Sendeka akizungumza na waandishi wa habari kuhusu tuhuma za baadhi ya wajumbe kuwa Mwenyekiti anampendelea kwa kumpa nafasi nyingi za kuchangia hoja katika semina ya kanuni za bunge maalum
 Mjumbe wa Bunge la Katiba na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo,Mhe. Freeman Mbowe akiongea na waandishi wa habari nje ya Ukumbi wa Bunge mjini Dodoma leo,mara baada ya kuahirishwa kwa kikao.
Mjumbe wa Bunge la Katiba,Mhe. Kajubi Mkajanga kutoka taasisi ya vyombo vya Habari akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya mwemyekiti kulazimika kiuahirisha semina ya kujadili kanuni hadi saa kumi na moja (11:00) jioni.

1 comment:

  1. Aaaaaah,hiyo picha hapo juu ya waziri Mkuu , Ndugu Seif Idi na wenzake yanikumbusha kitu katika ile muvi ya TITANIC, pale meli ilipokwishapatwa na mawahibu wakaitana nahodha,injinia,mmiliki wengine wengine na kutoa makaratasi ya michoro na kujadili kama meli itazama au la.Hata hivyo naliombea jahazi hili la Bunge la katibalivuke salama na litie nanga salama u salimini katika bandari ya muafaka na matumaini. Mungu ibariki Tanzania.

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.