Ninapata
taabu kuamini kwamba waandishi wengi na wanataaluma ya habari wanashindwa kutumia matumizi sahihi ya visiwa vya Unguja, Pemba na Zanzibar.
Utaona
wakati mwengine mwandishi anatumia jina la Zanzibar akimaanisha Unguja,wakati
mwengine hutakiwa kutumika jina la Pemba lakini litatumika la Zanzibar. Ingawa kimaana huweza kuwa ni sawa lakini kimatumizi inawezekana kuwa na makosa
Tatizo
hili nimeliona kwa waandishi wengi wa nyumbani, wa kigeni na kutoka upande wa pili wa Muungano
wakijikuta wakiingia katika mtego huu.
Sehemu ambayo huwa nasikia kutajwa kama ni Unguja au Pemba ni pale panapotajwa mikoa ya Kusini/Kaskazini kama ni Unguja au Pemba na wilaya zake.
Mkanganyiko
huu, kwa uoni wangu mdogo, umepelekea kwa kiasi kikubwa kufa
kidogo kidogo kwa jina la Unguja na badala yake kutumika Zanzibar kama ni Unguja
na ukiangalia kwa jicho pevu itapelekea
uonevu tutakaowafanyia wana wa Kizanzibari ambao hujulikana hivyo kwa sababu ya
kutoka katika Visiwa viwili vikuu vya Pemba na Unguja.
Tutafute
njia muwafaka ya kutumika kwa majina haya mawili bila ya kuathiri jengine
katika matumizi na mafhuum (maana) yake pia kabla ya kulipoteza jina la asili
la Unguja kama hatujaanza sasa.
Na
Mdau anaelienzi jina la Unguja
Usilete utata na wewe Zanzibar inatumika kuainisha visiwa vya Unguja na Pemba pamoja na visiwa vidogo vidogo kama vile Tumbatu, Uzi, Kojani, Kisiwapanza na vinginevyo. Kwa maana ya nchi ya Zanzibar. Pia Zanzibar inaweza ikatumika kama ni mji wa Unguja.
ReplyDeletehata kwa wenzetu pia hutumia Tanzania kama ni Tanganyika na ilhali Tanzania =Tanganyika+Zanzibar
ReplyDeletemtoa mada napenda kukutoa hofu. Kwanza jua kuwa, kila chombo cha habari kina house style yake ya kuandishi hasa kwa namna hii kwa wandishi wao juu ya kuweka eneo kinapotoka chanzo cha habari ama alipo mwandishi?.
ReplyDeleteMfano: Karafuu yakamatwa Chakechake
mwandishi ataandika: Na Sulumuni S. Sulumuni, Pemba.
Mfano: Darajani machinga wagoma tena kufunga maduka
mwandishi ataandika; Na Salma Hame Razu,Unguja
au
Umeme wakosekana kwa miaka 45
Na Ali Swahiba Ahmed, Tumbatu
kwa nini ameweka tumbatu? ameweka tumbatu kwa sababu ni eneo ambalo linatambulisha kwa moja kwa moja
ama anaweka; Na Ali Swahiba Ahmed, Tumbatu,Unguja.
ama anaweka;: Na Sulumuni S. Sulumuni, Chakechake, Pemba.
kwaTanzania Bara; Na Andrew Chale, Bagamoyo ama Na Andrew Chale, Bagamoyo, Pwani
au Na Andrew Chale, Pwani hii itakuwa tu endapo chanzo cha habari kimetoka ndani ya mkoa wa Pwani na hii ndio na sawa na kusema; Na Andrwe Chale, Unguja, lakini pia unaweza kusema Na Andrew Chale, Kizmkaz, Unguja.
by Andrew Chale, mwandishi wa habari 0719076376.
asante, usipagawe na uzuri wa picha ya kava, bali tazama filamu yenyewe..... na usiangalie by line by soma habari yenyewe.. ndani!