Na Ali Issa na Miza Othman Maelezo.
Umoja wa Vijana wa CCM Wilaya ya Mfenesini Mjini Unguja
wameamua kuiunga mkono kwa makusudi hutuba ya Rais
wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania
Jakaya Mrisho Kikwete aliyoitoa Bungeni wiki iliyopita wakati wa uzinduzi
wa Bunge maalumu la Katiba huko Dodoma.
Hayo yamesemwa leo huko Bububu Wilaya ya
magharibi Mjini Unguja na Mwenyekiti wa Umoja wa vijana CCM (UVCCM) Mbarouk Mrakib
Mbarouk wakati alipokuwa akizungumza na
waandishi wa habari pamoja na Vijana wa chama hicho ofisini kwake Bububu.
Amesema
hutuba ya Rais kikwete ni hutuba ilio jaa hekima na busara juu ya
mustakabali mzima wa muundo wa serikali waitakayo Watanzania.
Amesema kutokana na kauli za Rais huyo hakuna budi kwao kuiunga mkono
kwani ndio muelekeo wao katika muundo wa serikali waitakayo wanaccm ambayo
yenye umoja na mshikamano kwa watanzania.
Aidha amesema alihamisha kuwa kwa wale wajumbe wanaohudhuria kikao cha Bunge la Katiba huko Dodoma hawana budi kuhakikisha wanatoa maoni ya wananchi wao ikiwa ni njia moja ya
kuwafanya wananchi hao kuleta umoja na mshikamano katika Taifa lao.
Mwenyekiti huyo alimpongeza kwa dhati
dkt. Kikwete kwa kulizungumzia suala la mipaka ya Tanzania, mito, maziwa,na
bahari ambalo lilisahauliwa ndani ya katiba hiyo.
Pia alimshukuru Rais huyo kwa kuyazingatia
masuala ya Zanzibar juu ya kujiunga na nchi za visiwa duniani ,umoja wa kiislamu
OIC, na suala la mafuta na gesi asilia.
Mwenyekiti huyo aliwakumbusha wabunge wa
Bunge maalumu wa CCM kuijadili katiba hiyo kwa kina ili lengo la kuwepo kwao
bungeni ni kufanikiwa kwa katiba wanayo itaka wanaCCM.
No comments:
Post a Comment